Upinzani wahofia vita na Malawi; Wadai chanzo ni uchimbaji mafuta mpakani

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=3][/h]

*Wadai chanzo ni uchimbaji mafuta mpakani
*Yashauriwa leseni itolewe kwa nchi mbili

Na Godfrey Ismaely

IKIWA imepita miaka kadhaa baada ya Tanzania kuingia vita kati yake na Uganda kwa ajili ya kuwania
mpaka mkoani Kagera, hofu ya vita nyingine imejitokeza kati ya Malawi na Tanzania kwa ajili ya kuwania Ziwa Nyasa.

Hofu hiyo ilielezwa bungeni mjini Dodoma jana na Waziri Kivuli wa kambi ya Upinzani ambaye pia ni Msemaji Mkuu kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji Bw. Highness Kiwia (CHADEMA) wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2011 na 2012.

"Mheshimiwa mwenyekiti, hivi sasa nchi yetu ipo hatarini kuingia kwenye mgogoro mkubwa na nchi jirani ya Malawi, katika kugombania eneo la Ziwa Nyasa," alisema Bw. Kiwia.

Alisema kambi hiyo ina taarifa kwamba serikali ya Malawi imepanga kutoa leseni ya kutafuta mafuta katika kitalu ambacho kipo ndani ya Tanzania.

"Tuna taarifa kuwa Serikali ya Malawi inapanga kutoa leseni ya kutafuta mafuta kwa kampuni ya Surestream Petroleum Limited,eneo ambalo 'block' (kitalu) hiyo imeenea inahusisha sehemu ya Tanzania,' alisema Bw. Kiwia

Alisema maamuzi hayo yanaweza kuleta vurugu ya kimpaka ikiwamo vurugu zitakazopelekea vita baina ya nchi hizo mbili.

"Mheshimiwa Mwenyekiti, uamuzi huu wa Serikali ya Malawi unaweza kuleta vurugu ya kimpaka na hata vita kati ya nchi hizi mbili. Wakati Serikali yetu inasema mpaka wa Ziwa Nyasa ni katikati ya maji ya ziwa hilo, Serikali ya Malawi inasema mpaka ni ufukweni na kwa mantiki hiyo Ziwa lote wanalichukulia kuwa ni lao," alisema Bw. Kiwia.

Bw. Kiwia alisema kuwa kutokana na mkanganyiko huo Wizara ya Maji ndiyo inayohusika na usimamizi wa Bonde la Ziwa Nyasa hivyo inapaswa kuwa na taarifa zote juu ya uvamizi huo.

"Kambi rasmi ya Upinzani tunahoji, je ni hatua gani Serikali yetu imechukua kulinda Ziwa Nyasa na maji yake?, kwa kuwa kipindi hiki ni kipindi ambacho kampuni za mafuta duniani zinahaha kutafuta maeneo ya kuwekeza. Hata kuingilia maeneo ya maji, Kambi ya Upinzani inashauri kwamba Serikali ifanye mazungumzo ya haraka na Serikali ya Malawi na kuunda 'joint development zone' na hivyo kutoa leseni hii kwa pamoja, ili utafutaji uendelee kwa kusimamiwa na nchi zote mbili wakati utatuzi wa mpaka huu unaendelea," alisema Bw. Kiwia.

Alisema kambi hiyo inaitaka serikali itoe tamko kwamba kuendelea kutoa leseni kwa kampuni ya Surestream itakuwa ni sawa na kuvamia eneo la Tanzania na kwamba Tanzania itachukua hatua stahili kulinda mipaka yake.

Tuhuma za ubadhirifu


KAMBI ya upinzani kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji Bungeni imeanika ubadhirifu wa zaidi ya dola za Marekani milioni 39 sawa na takribani sh. bilioni 63 za Tanzania zilizofanywa ndani ya wizara hiyo kati ya mwaka 2007 na 2010.

"Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema, “ufisadi na rushwa ni adui mkubwa zaidi wa maslahi ya wananchi wakati wa amani kuliko vita”," alisema Waziri kivuli wa Wizara hiyo Bw. Highness Kiwia (CHADEMA) ambaye pia ni Mbunge wa Ilemela na kuongeza;

"Kwa nasaha hii, ni ukweli usiopingika kuwa jitihada zozote zinazofanyika katika taifa hili, za kujaribu kuondoa kero na matatizo ya wananchi, ikiwemo shida kubwa ya maji, kamwe hazitafanikiwa bila kwanza kuupiga vita ufisadi," aliongeza.

Bw. Kiwia alisema hayo Bungeni jana, mjini Dodoma wakati akiwasilisha hotuba ya kambi ya upinzani kwa Makadirio ya Mapato na Matumizi katika mwaka wa fedha 2011 na 2012 huku akisema kuwa wanao ushahidi wa ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG" juu ya hayo wanayoyasema.

Alisema katika ripoti hiyo, Wizara imebainika kufanya ubadhirifu wa zaidi ya dola za Marekani milioni 39 (sawa na takribani shilingi bilioni 63 za Tanzania) kwenye mazingira ya utata, bila kuzingatia miradi na kiasi cha fedha zilizotengwa kwenye mpango kazi wa mwaka wa wizara hiyo.

Aidha alisema kutokana na hali hiyo, ni dhahiri kuwa fedha nyingi zinazoingia Serikalini kutokana na kodi za wananchi, mauzo ya raslimali mbalimbali kama madini, na misaada mingi iliyotolewa na nchi Wahisani kwa miaka yote 50 tangu uhuru, zimekuwa zikifujwa ndani ya Wizara ya Maji na idara zake mbalimbali.

Pia msemaji huyo wa kambi ya upinzani alisema kupitia ukaguzi huo, ilibanika kuwa fedha nyingi za umma zilifujwa katika ununuzi wa mashangingi (Toyota Land Cruiser) yapatayo 68, ununuzi uliofanyika mwaka 2009 kwa 'Yen za Japan' milioni 235.4 sawa na takribani shilingi bilioni tano za Kitanzania huku akisema ni kinyume na Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2004.

"Aidha, imegundulika kuwa ununuzi huo wa mashangingi umeisababishia nchi yetu hasara ya zaidi ya shilingi milioni 218, kutokana na tofauti ya viwango vya ubadilishaji wa pesa za kigeni kutozingatiwa," alisema Bw. Kiwia.

Wabadhirifu wasimamishwe kazi


Wakati huo huo Bw. Kiwia alisema kuwa ili kukomesha tabia ya ubadhirifu wa fedha za umma uliokithiri, Kambi hiyo inataka viongozi na watendaji wote wakuu waliokuwa na dhamana ya kuisimamia wizara kwa kipindi hicho wasimamishwe kazi akiwemo waziri.
di ya shilingi bilioni 63," alisema Bw. Kiwia.

Aliongeza kuwa wanataka uchunguzi huru na wa haraka ufanyike ili kubaini uhusika wa kila mmoja wao katika ufisadi huo, hatimaye watakaobainika wachukuliwe hatua kali za kinidhamu na kushitakiwa kwa mujibu wa Sheria Namba 200, ya Uhujumu Uchumi ya mwaka 2002.

"Ni lazima Bunge la Kumi limalize utamaduni mbaya wa kulindana na kujenga utamaduni mpya wa kuwajibishana," alisema Bw. Kiwia.
 
Back
Top Bottom