Upinzani wahofia vita na Malawi; Wadai chanzo ni uchimbaji mafuta mpakani

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,871
Points
1,225

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,871 1,225
*Wadai chanzo ni uchimbaji mafuta mpakani
*Yashauriwa leseni itolewe kwa nchi mbili

Na Godfrey Ismaely

IKIWA imepita miaka kadhaa baada ya Tanzania kuingia vita kati yake na Uganda kwa ajili ya kuwania
mpaka mkoani Kagera, hofu ya vita nyingine imejitokeza kati ya Malawi na Tanzania kwa ajili ya kuwania Ziwa Nyasa.

Hofu hiyo ilielezwa bungeni mjini Dodoma jana na Waziri Kivuli wa kambi ya Upinzani ambaye pia ni Msemaji Mkuu kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji Bw. Highness Kiwia (CHADEMA) wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2011 na 2012.

"Mheshimiwa mwenyekiti, hivi sasa nchi yetu ipo hatarini kuingia kwenye mgogoro mkubwa na nchi jirani ya Malawi, katika kugombania eneo la Ziwa Nyasa," alisema Bw. Kiwia.

Alisema kambi hiyo ina taarifa kwamba serikali ya Malawi imepanga kutoa leseni ya kutafuta mafuta katika kitalu ambacho kipo ndani ya Tanzania.

"Tuna taarifa kuwa Serikali ya Malawi inapanga kutoa leseni ya kutafuta mafuta kwa kampuni ya Surestream Petroleum Limited,eneo ambalo 'block' (kitalu) hiyo imeenea inahusisha sehemu ya Tanzania,' alisema Bw. Kiwia

Alisema maamuzi hayo yanaweza kuleta vurugu ya kimpaka ikiwamo vurugu zitakazopelekea vita baina ya nchi hizo mbili.

"Mheshimiwa Mwenyekiti, uamuzi huu wa Serikali ya Malawi unaweza kuleta vurugu ya kimpaka na hata vita kati ya nchi hizi mbili. Wakati Serikali yetu inasema mpaka wa Ziwa Nyasa ni katikati ya maji ya ziwa hilo, Serikali ya Malawi inasema mpaka ni ufukweni na kwa mantiki hiyo Ziwa lote wanalichukulia kuwa ni lao," alisema Bw. Kiwia.

Bw. Kiwia alisema kuwa kutokana na mkanganyiko huo Wizara ya Maji ndiyo inayohusika na usimamizi wa Bonde la Ziwa Nyasa hivyo inapaswa kuwa na taarifa zote juu ya uvamizi huo.

"Kambi rasmi ya Upinzani tunahoji, je ni hatua gani Serikali yetu imechukua kulinda Ziwa Nyasa na maji yake?, kwa kuwa kipindi hiki ni kipindi ambacho kampuni za mafuta duniani zinahaha kutafuta maeneo ya kuwekeza. Hata kuingilia maeneo ya maji, Kambi ya Upinzani inashauri kwamba Serikali ifanye mazungumzo ya haraka na Serikali ya Malawi na kuunda 'joint development zone' na hivyo kutoa leseni hii kwa pamoja, ili utafutaji uendelee kwa kusimamiwa na nchi zote mbili wakati utatuzi wa mpaka huu unaendelea," alisema Bw. Kiwia.

Alisema kambi hiyo inaitaka serikali itoe tamko kwamba kuendelea kutoa leseni kwa kampuni ya Surestream itakuwa ni sawa na kuvamia eneo la Tanzania na kwamba Tanzania itachukua hatua stahili kulinda mipaka yake.

Tuhuma za ubadhirifu

KAMBI ya upinzani kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji Bungeni imeanika ubadhirifu wa zaidi ya dola za Marekani milioni 39 sawa na takribani sh. bilioni 63 za Tanzania zilizofanywa ndani ya wizara hiyo kati ya mwaka 2007 na 2010.

"Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema, "ufisadi na rushwa ni adui mkubwa zaidi wa maslahi ya wananchi wakati wa amani kuliko vita"," alisema Waziri kivuli wa Wizara hiyo Bw. Highness Kiwia (CHADEMA) ambaye pia ni Mbunge wa Ilemela na kuongeza;

"Kwa nasaha hii, ni ukweli usiopingika kuwa jitihada zozote zinazofanyika katika taifa hili, za kujaribu kuondoa kero na matatizo ya wananchi, ikiwemo shida kubwa ya maji, kamwe hazitafanikiwa bila kwanza kuupiga vita ufisadi," aliongeza.

Bw. Kiwia alisema hayo Bungeni jana, mjini Dodoma wakati akiwasilisha hotuba ya kambi ya upinzani kwa Makadirio ya Mapato na Matumizi katika mwaka wa fedha 2011 na 2012 huku akisema kuwa wanao ushahidi wa ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG" juu ya hayo wanayoyasema.

Alisema katika ripoti hiyo, Wizara imebainika kufanya ubadhirifu wa zaidi ya dola za Marekani milioni 39 (sawa na takribani shilingi bilioni 63 za Tanzania) kwenye mazingira ya utata, bila kuzingatia miradi na kiasi cha fedha zilizotengwa kwenye mpango kazi wa mwaka wa wizara hiyo.

Aidha alisema kutokana na hali hiyo, ni dhahiri kuwa fedha nyingi zinazoingia Serikalini kutokana na kodi za wananchi, mauzo ya raslimali mbalimbali kama madini, na misaada mingi iliyotolewa na nchi Wahisani kwa miaka yote 50 tangu uhuru, zimekuwa zikifujwa ndani ya Wizara ya Maji na idara zake mbalimbali.

Pia msemaji huyo wa kambi ya upinzani alisema kupitia ukaguzi huo, ilibanika kuwa fedha nyingi za umma zilifujwa katika ununuzi wa mashangingi (Toyota Land Cruiser) yapatayo 68, ununuzi uliofanyika mwaka 2009 kwa 'Yen za Japan' milioni 235.4 sawa na takribani shilingi bilioni tano za Kitanzania huku akisema ni kinyume na Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2004.

"Aidha, imegundulika kuwa ununuzi huo wa mashangingi umeisababishia nchi yetu hasara ya zaidi ya shilingi milioni 218, kutokana na tofauti ya viwango vya ubadilishaji wa pesa za kigeni kutozingatiwa," alisema Bw. Kiwia.

Wabadhirifu wasimamishwe kazi

Wakati huo huo Bw. Kiwia alisema kuwa ili kukomesha tabia ya ubadhirifu wa fedha za umma uliokithiri, Kambi hiyo inataka viongozi na watendaji wote wakuu waliokuwa na dhamana ya kuisimamia wizara kwa kipindi hicho wasimamishwe kazi akiwemo waziri.
di ya shilingi bilioni 63," alisema Bw. Kiwia.

Aliongeza kuwa wanataka uchunguzi huru na wa haraka ufanyike ili kubaini uhusika wa kila mmoja wao katika ufisadi huo, hatimaye watakaobainika wachukuliwe hatua kali za kinidhamu na kushitakiwa kwa mujibu wa Sheria Namba 200, ya Uhujumu Uchumi ya mwaka 2002.

"Ni lazima Bunge la Kumi limalize utamaduni mbaya wa kulindana na kujenga utamaduni mpya wa kuwajibishana," alisema Bw. Kiwia.
 
Kinyungu

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2008
Messages
7,536
Points
2,000

Kinyungu

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2008
7,536 2,000
[h=3][/h]

Hapo kwenye red ina maana wapinzani wanajua nchi jirani imegawa eneo la nchi yetu ambalo sio lake kwa wawekezaji bila usalama wa taifa hili kuwa na habari? Kweli hii nchi imeuzwa long time.

Hata mimi nagawa block kwenye shamba langu la urithi kwa anayetaka kuchungulia kama kuna madini/mafuta
 
Buchanan

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2009
Messages
13,206
Points
1,500

Buchanan

JF-Expert Member
Joined May 19, 2009
13,206 1,500
Hapo kwenye red ina maana wapinzani wanajua nchi jirani imegawa eneo la nchi yetu ambalo sio lake kwa wawekezaji bila usalama wa taifa hili kuwa na habari? Kweli hii nchi imeuzwa long time. <br />
<br />
Hata mimi nagawa block kwenye shamba langu la urithi kwa anayetaka kuchungulia kama kuna madini/mafuta
Magamba yanafikiria tu uchaguzi mdogo wa Igunga, hayana taarifa na mipaka!
 
Lukolo

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Messages
5,148
Points
1,250

Lukolo

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2009
5,148 1,250
Naomba sana Mungu hiyo vita isubiri kwanza hadi nchi itakapokuwa imepata rais mwingine. Maana kama rais atakuwa ni huyuhuyu Kikwete, tutakula mkong'oto wa mbwa mwizi. Kwa sasa ni kama nchi inajiongoza yenyewe.
 
mashikolomageni

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2010
Messages
1,567
Points
1,195

mashikolomageni

JF-Expert Member
Joined Jan 5, 2010
1,567 1,195
Mgogoro huo wa mpaka ni wa siku nyingi kwani ukiangalia ramani za zamani unaona Tanganyika haina eneo la maji katika ziwa Nyasa(Malawi). Hoja za Banda Kamuzu miaka ya 70-80 ilikuwa kwamba ziwa lote ni mali yao.
 
Ibrah

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2007
Messages
2,721
Points
1,225

Ibrah

JF-Expert Member
Joined Mar 22, 2007
2,721 1,225
Kwa mujibu wa ramani ya Malawi, hakuna Ziwa linaloitwa Nyasa bali Lake Malawi! Hii ina maanisha kuwa watu wa Kyera, Mbambabay, Liuli, Manda na Mbinga Tanzania wanafanyia uvuvi wao nje ya nchi (Malawi).

Kuna haja ya kushughulika na hawa Wamalawi; kama tunapenda amani na nchi jirani. Ama tuingie vitani ingawa (jambo ambalo kwa uzalendo wetu ulivyoporomoka) hatuwezi, au twende Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi kama walivyofanya Cameroun dhidi ya Nigeria kuhusu Ghuba ya Bakasi.
 
Arafat

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2009
Messages
2,581
Points
0

Arafat

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2009
2,581 0
hili tatizo la miaka mingi sana toka nikiwa mdogo, wengine wanasema nyerere alichua kwa mabavu siyo eneo letu wengine wanasema letu, baya zaidi wamalawi ndio wengi sana kwenye system yetu ya Usalama wa Taifa sasa sijui kama tuta waweza.

Hii mipaka ya wakoloni imeleta tabu sana africa, tokea wakati huo kwanini hawaja kaachini kuanisha mpaka upo wapi? ili tatizo liishe maana ukiangalia hata atlas ambazo watoto wetu wanafundishwa nazo mashuleni leo zinaonyesha hilo ziwa lipo Malawi, mbaya zaidi hadi serikalini kuna watu wanatengeneza report zinazoonyesha hilo ziwa lipo Malawi! na wanazituma hadi international offices na katika instituations za nje ya nchni.
 
Nikupateje

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2009
Messages
1,325
Points
1,250

Nikupateje

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2009
1,325 1,250
Kama Nyerere alikabidhiwa nchi bila hata tone moja la Lake Malawi, nyinyi hoja yenu ina msingi gani.

Vita haipiganwi kwa kuonyeshana ni taifa gani lina uzalendo kuzidi jingine kwani hata wamalawi wanaujua uzalendo kwa mali walizorithi toka kwa mwingereza.

Ni lini Malawi iliidhulumu Tanganyika mpaka kwa kumega sehemu yote ya ziwa hilo!
 
Fblukuwi

Senior Member
Joined
Dec 8, 2010
Messages
131
Points
170

Fblukuwi

Senior Member
Joined Dec 8, 2010
131 170

Kaka kwa mujibu wa Mkataba wa BERLIN wa 1884 Ziwa NYASA liligawanywa katikati ya Germany Osteoafrica (Tanganyika) na malawi ila baada ya vita ya kwanza ya dunia Ziwa nyasa liliwekwa kuwa chini ya UTAWALA wa Nyasaland(Malawi) kiutawala na si kweli kuwa mpaka ulibadilishwa. na kwa taarifa kama ukifika ziwani utaona huo ugumu wa mpaka kuwa ufukweni kwani watu wamezaliwa hapo ufukweni na maisha yao yote wanavua humo na hawajawahi kukutana na wamalawi waliowakataza kulitumia hilo Ziwa!
Sasa kama Nyie watanganyika mnataka kuligawa hilo ziwa kwa Malawi Basi MIMI mwenyewe Nitalilinda hilo Ziwa kwani sina mahali pengine pa kwenda nami najijua kuwa ni MTANGANYIKA.
 
ndetichia

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2011
Messages
27,725
Points
2,000

ndetichia

JF-Expert Member
Joined Mar 18, 2011
27,725 2,000
Kaka kwa mujibu wa Mkataba wa BERLIN wa 1884 Ziwa NYASA liligawanywa katikati ya Germany Osteoafrica (Tanganyika) na malawi ila baada ya vita ya kwanza ya dunia Ziwa nyasa liliwekwa kuwa chini ya UTAWALA wa Nyasaland(Malawi) kiutawala na si kweli kuwa mpaka ulibadilishwa. na kwa taarifa kama ukifika ziwani utaona huo ugumu wa mpaka kuwa ufukweni kwani watu wamezaliwa hapo ufukweni na maisha yao yote wanavua humo na hawajawahi kukutana na wamalawi waliowakataza kulitumia hilo Ziwa!<br />
Sasa kama Nyie watanganyika mnataka kuligawa hilo ziwa kwa Malawi Basi MIMI mwenyewe Nitalilinda hilo Ziwa kwani sina mahali pengine pa kwenda nami najijua kuwa ni MTANGANYIKA.
<br />
<br />
kwa hiyo baada ya vita ya kwanza ya dunia wamalawi walisema la kwao na je sisi kama watanganyika tulichukua hatua gani kulilinda hilo ziwa kwa mipika yetu?

hapa mi naona kuna kitu wanataka kukukwepa ilitusishtukie kwa nini wawe na hofu ya kiasi cha vita..
 
Njowepo

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
9,469
Points
2,000

Njowepo

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
9,469 2,000
Ilo suala ata wamalawi wanajua kuwa ilo ziwa ni la wote ndo maana toka enzi na enzi watu wa pande mbili za ziwa hawakorofishani!
Watu wa manda,ritui kwa komba pale,mbambabay,itungi wanaishi kwa amani na utulivu wala hakuna malumbano!
 
Fblukuwi

Senior Member
Joined
Dec 8, 2010
Messages
131
Points
170

Fblukuwi

Senior Member
Joined Dec 8, 2010
131 170
Baada ya vita ya kwanza ya Dunia Waingereza walitawala nchi zoteMalawi na Tanganyika. ILi watawale effectively walitoa usimamizi kwa malawi na SI KUBADILISHA MPAKA. Wazo lolote la kubadiliosha mpaka au kuwanyima wananchi kando ya Ziwa udhibiti wa maji yao kiuchumi ni UKIUKAJI MKUBWA wa HAKI ZA BINADAMU na wananchi wa huko ziwani wako Tayari kulilinda ziwa lao.
Ulizeni kulitokea nini ile miaka ya mwishoni mwa 1970 na mwanzoni mwa miaka ya 1980!!! hadi leo nakumbuka zile nyimbo za kumshutumu BANDA na wananchi kule walishawekwa tayari kupambana na mvamizi! Sasa nyie MAGAMBA mkinegotiate kugawa hilo ziwa kinyume na inavyoeleweka sisi huku hatutotambua hayo makubaliano yenu!!!
 
kichomiz

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2011
Messages
15,212
Points
2,000

kichomiz

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2011
15,212 2,000
Ingekuwa zama za nyerere hata wasingethubutu ilo ila izi zama legelege ndo maana wanadhubutu!
<br />
<br />
We unadhani wao hawajui kama TZ ya sasa ni legelege,wanajua sana ndio maana wameamua kufanya hivyo,mwisho watajimegea na kyela sasa si hatuna serikali,watatuchapa sana hawa jamaa.
 
Forum statistics

Threads 1,353,225
Members 518,297
Posts 33,075,281
Top