Upinzani wa Tanzania ni wa vimatukio, Rais Samia ameumaliza kisayansi

Ndugu zangu upinzani wa Tanzania Ni mwepesi Sanaa, Ni Rahisi Sana kuupoteza na kuufifisha , Ni Rahisi Sana kuumaliza, kuudhoofisha , kuusambalatisha, kuuvuruga, kuugawa na kuuweka mikononi mwako na kuutumia unapohitaji kufanya Jambo fulani, Hii Ni kutokana na kwamba upinzani wa Tanzania haunaga Sera Wala ajenda Wala hoja zenye kugusa hisia za watanzania, hauna vitu vyenye kugusa maisha ya Watanzania hasa wanyonge Kama ifanyavyo CCM miaka yote kuwagusa watanzania wanyonge,

Upinzani wa Tanzania Ni Kama mkanda uliokatika katika ambao hauwezi kupita kwenye rukusi na kufunga suluali, Hauna unachokisimamia Wala kupigania, hauna malengo ya muda mfupi wa Kati na muda mrefu, Hauna hata mikakati ya miaka mitano, Hata kuandaa mgombea Urais tu hauwezi, maana Ni upinzani unakwenda na mdundo wa vijana wake, Ni upinzani unaokwenda kimizuka, Ni upinzani unaokwenda kiharakati harakati kwa kila Jambo, Ni upinzani ambao hauelewi unataka Nini na unapigania Nini zaidi ya kuona kapu la Ruzuku yao likituna,

Ni upinzani unaodaka na kusubili vimatukio vya mpito tu ili uende navyo, Ndio sababu tukio likizimwa kimaridadi na serikali hii shupavu ya mama Samia unaona nao wanapoteana na kuzima, kwa hiyo Ni Rahisi Sana kuwachezesha ngoma wanachama wa kawaida Hadi Mwenyekiti wao Taifa Ndugu Mbowe

Hapa ndipo Rais wetu mpendwa Mama Samia gwiji wa Siasa, mwana mikakati aliyeiva, kiongozi shupavu, mwanadiplomasia nguli, mwenye macho ya kuona mbali, Sauti na mikono ya kupenya popote, Mwenye Akili kubwa na upeo wa mbali, Mtulivu na mwenye kwenda na muda na kusubiri wakati sahihi, mwenye Shabaha na maono ya Mbali,Anayejuwa mbinu na mikakati ya kiuongozi , Rais aliyepikwa ,aliyeiva kimbinu na kimkakati, Mwamba usiyoteteleka Wala kuteteleshwa na mtu yoyote yule, Jemedari shupavu aliyefuzu mafunzo ya kila aina, Tumaini na Tagemeo la watanzania aliyewaweza wapinzani na kuwamaliza upinzani ambao siku zote umekuwa ukitegemea vimatukio

Hakika Rais Samia ameuumbua Sana upinzani wa Tanzania, ameonyesha kuwa Tanzania hakukuwa na upinzani Bali wababaishaji waliokuwa wanategemea mianya kupata ajenda zao, Upinzani umeonyesha kuwa ulikuwa Ni Kama mti uliokosa mizizi, Ni gari lisilo na injini japo limepakwa Rangi nje, Ni mwisho wa upinzani Sasa,

Upinzani wa Tanzania Hauta simama Tena, Hautashamiri Tena, Hautatusumbua Tena, Hautaaminika Tena, Hauta kuwa na mvuto Tena, Haitakuwa Kama 2015, Hautatubabaisha Tena, Hautatulaza macho Tena, Hautavuna Tena wanachama wetu, Hautapata Tena wanachama wenye akili na wenye kujitambua, Hakuna Atakaye toa hela zake kuwapa upinzani Tena, Hakuna Atakaye tokwa jasho kuutetea upinzani tena maana ulishatoka katika mioyo ya watanzania, ulishapuuzwa na vijana ambao n

dio ilikuwa nguzo yake kuu, ilikuwa ndio ngao yake kuu na Tumaini lake

Lakini Sasa CCM chini ya Nahodha shupavu Rais Samia ,vijana Wana Imani na matumaini makubwa Sana na Rais wetu mpendwa, vijana wameyaelekeza macho yao kwa mama Samia, watanzania wameamua kuwa bega kwa bega na mama Samia, watanzania wameamua kufanya kazi kwa bidii ili kumuunga mkono mama Samia, watanzania wanamuona Rais Samia Kama mama yao, kiongozi wao, mlezi wao, mzazi wao ndio sababu unaona namna mh Rais Samia anavyoheshimima na kila mtanzania, anapendwaa na kukubalika na kila mtanzania, anasikilizwa na kufuatiliwa na kila mtu,

Rais Samia songa mbele mama yetu,chapa kazi ,tutumikie watanzania, tuhudumie watanzania, tunakuamini, Tunakutegemea,tuna Imani na wewe, usikatishwe Tamaa na wachache maana tunao kuunga mkono Ni mamilioni ya watanzania, Tunazidi kukuombea Afya njema na nguvu za Kuendelea kututumikia watanzania,

Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Lucas Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
Samia yupo kisayansi zaidi, leo kafanya kitu kikubwa kule Kigoma lakini kimeanza na kumalizika kimya kimya tu.

Hakutakuwa na kishindo cha vyombo vya habari kuelezea mazingira ya uwekezaji yaliyowezeshwa leo hii huko Kigoma, suala la nishati ya umeme linakwenda kuufungua mazima ule mkoa.
 
Rais Samia Ni mchapa kazi Sana, Ni kiongozi aliyejitoa na kujitolea kuwatumikia watanzania kwa Dhati ya moyo wake na kwa nguvu zake zote, Ndio maana unaona muda wote yupo kazini kuwatumikia watanzania
 
Na wewe muda wote uko wapi na unafanya nini?
Nipo shambani naandaa mashamba kwa ajili ya msimu mpya hasa baada ya Rais wetu kutupatia matumaini makubwa sisi wakulima kutokana na kushuka kwa Bei ya mbolea kulikotokana na uamuzi wake wakutoa Ruzuku ya mabillioni ya Fedha na uwepo wa soko la uhakika kwa mazao yetu
 
Kama anakubalika, kwanini mnatumia nguvu kubwa hivyo kutuaminisha?
Wala hatutumii nguvu Bali tunaelezea Yale aliyoyafanya mh Rais wetu ndani ya muda mfupi tangia aapishwe kuwa Rais wetu na Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama
 
Nipo shambani naandaa mashamba kwa ajili ya msimu mpya hasa baada ya Rais wetu kutupatia matumaini makubwa sisi wakulima kutokana na kushuka kwa Bei ya mbolea kulikotokana na uamuzi wake wakutoa Ruzuku ya mabillioni ya Fedha na uwepo wa soko la uhakika kwa mazao yetu
Tangu asubuhi upo JF kusifia uozo muda wa kwenda shambani utaupata wapi?
 
Hicho ndio ulichofanya?
Mbona 90% ya bandiko lako unaongelea upinzani?
Mambo aliyoyafanya mh Rais wetu mpendwa nimeyaeleza Sana humu na nitaendelea kuyaelezea Sana tu maana mh Rais anafanya kazi kila siku na muda wote katika kuwatumikia watanzania wanyonge wasio na sauti

Ukienda kwa wakulima utaona na kukuta Alama za mh Rais wetu namna alivyo wasaidia wakulima wa nchi hii, utaona namna mbolea ilivyoshuka Bei baada ya kutoa Ruzuku ya mabillioni

Ukienda katika Elimu utaona namna alivyo Jenga shule nyingi mpya, ujenzi wa vyumba vya madarasa, utoaji wa Elimu bure Hadi kidato Cha sita, Hali hii imesaidia Sana wanafunzi Kuendelea na masomo yao na kupata Elimu bila shida hata Kama wametoka familia duni

Ukienda secta binafsi utaona namna mh Rais wetu mpendwa alivyoimarisha na Sasa inatoa mchango mkubwa katika uchumi wetu na hata fursa za ajira kwa vijana,lakini pia wawekezaji na uwekezaji umeongezeka Sana hapa nchini,bila kusahau mafuriko ya watalii yameongezeka kutokana na ubunifu wa mh Rais kupitia royal Tour,
 
Sasa kwann bado anazuia uhuru wa upinzani kufanya vikao?
 
Back
Top Bottom