Upinzani wa Tanzania ni wa vimatukio, Rais Samia ameumaliza kisayansi

Lucas mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
4,672
2,046
Ndugu zangu upinzani wa Tanzania Ni mwepesi Sanaa, Ni Rahisi Sana kuupoteza na kuufifisha, ni rahisi sana kuumaliza, kuudhoofisha, kuusambalatisha, kuuvuruga, kuugawa na kuuweka mikononi mwako na kuutumia unapohitaji kufanya jambo fulani, hii ni kutokana na kwamba upinzani wa Tanzania haunaga Sera Wala ajenda Wala hoja zenye kugusa hisia za watanzania, hauna vitu vyenye kugusa maisha ya Watanzania hasa wanyonge Kama ifanyavyo CCM miaka yote kuwagusa watanzania wanyonge.

Upinzani wa Tanzania ni kama mkanda uliokatika katika ambao hauwezi kupita kwenye rukusi na kufunga suluali, Hauna unachokisimamia Wala kupigania, hauna malengo ya muda mfupi wa Kati na muda mrefu, Hauna hata mikakati ya miaka mitano, Hata kuandaa mgombea Urais tu hauwezi, maana ni upinzani unakwenda na mdundo wa vijana wake, Ni upinzani unaokwenda kimizuka, ni upinzani unaokwenda kiharakati harakati kwa kila Jambo, ni upinzani ambao hauelewi unataka Nini na unapigania Nini zaidi ya kuona kapu la Ruzuku yao likituna.

Ni upinzani unaodaka na kusubili vimatukio vya mpito tu ili uende navyo, Ndio sababu tukio likizimwa kimaridadi na serikali hii shupavu ya mama Samia unaona nao wanapoteana na kuzima, kwa hiyo ni rahisi sana kuwachezesha ngoma wanachama wa kawaida Hadi Mwenyekiti wao Taifa Ndugu Mbowe

Hapa ndipo Rais wetu mpendwa Mama Samia gwiji wa Siasa, mwana mikakati aliyeiva, kiongozi shupavu, mwanadiplomasia nguli, mwenye macho ya kuona mbali, Sauti na mikono ya kupenya popote, Mwenye Akili kubwa na upeo wa mbali, Mtulivu na mwenye kwenda na muda na kusubiri wakati sahihi, mwenye Shabaha na maono ya Mbali, anayejuwa mbinu na mikakati ya kiuongozi, Rais aliyepikwa ,aliyeiva kimbinu na kimkakati, Mwamba usiyoteteleka Wala kuteteleshwa na mtu yoyote yule, Jemedari shupavu aliyefuzu mafunzo ya kila aina, Tumaini na Tagemeo la Watanzania aliyewaweza wapinzani na kuwamaliza upinzani ambao siku zote umekuwa ukitegemea vimatukio.

Hakika Rais Samia ameuumbua Sana upinzani wa Tanzania, ameonyesha kuwa Tanzania hakukuwa na upinzani Bali wababaishaji waliokuwa wanategemea mianya kupata ajenda zao, Upinzani umeonyesha kuwa ulikuwa Ni Kama mti uliokosa mizizi, Ni gari lisilo na injini japo limepakwa Rangi nje, ni mwisho wa upinzani sasa.

Upinzani wa Tanzania Hauta simama Tena, Hautashamiri Tena, Hautatusumbua Tena, Hautaaminika Tena, Hauta kuwa na mvuto Tena, Haitakuwa Kama 2015, Hautatubabaisha Tena, Hautatulaza macho Tena, Hautavuna Tena wanachama wetu, Hautapata Tena wanachama wenye akili na wenye kujitambua, Hakuna Atakaye toa hela zake kuwapa upinzani Tena, Hakuna Atakaye tokwa jasho kuutetea upinzani tena maana ulishatoka katika mioyo ya watanzania, ulishapuuzwa na vijana ambao ndio ilikuwa nguzo yake kuu, ilikuwa ndio ngao yake kuu na Tumaini lake.

Lakini Sasa CCM chini ya Nahodha shupavu Rais Samia ,vijana Wana Imani na matumaini makubwa Sana na Rais wetu mpendwa, vijana wameyaelekeza macho yao kwa mama Samia, watanzania wameamua kuwa bega kwa bega na mama Samia, watanzania wameamua kufanya kazi kwa bidii ili kumuunga mkono mama Samia, watanzania wanamuona Rais Samia Kama mama yao, kiongozi wao, mlezi wao, mzazi wao ndio sababu unaona namna Mh Rais Samia anavyoheshimima na kila mtanzania, anapendwaa na kukubalika na kila mtanzania, anasikilizwa na kufuatiliwa na kila mtu.

Rais Samia songa mbele mama yetu,chapa kazi tutumikie Watanzania, tuhudumie watanzania, tunakuamini, Tunakutegemea, tuna Imani na wewe, usikatishwe Tamaa na wachache maana tunao kuunga mkono ni mamilioni ya watanzania, Tunazidi kukuombea Afya njema na nguvu za Kuendelea kututumikia Watanzania.

Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Lucas Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
 
Izia maji

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
1,106
1,836
Ndugu zangu upinzani wa Tanzania Ni mwepesi Sanaa, Ni Rahisi Sana kuupoteza na kuufifisha , Ni Rahisi Sana kuumaliza, kuudhoofisha , kuusambalatisha, kuuvuruga, kuugawa na kuuweka mikononi mwako na kuutumia unapohitaji kufanya Jambo fulani, Hii Ni kutokana na kwamba upinzani wa Tanzania haunaga Sera Wala ajenda Wala hoja zenye kugusa hisia za watanzania, hauna vitu vyenye kugusa maisha ya Watanzania hasa wanyonge Kama ifanyavyo CCM miaka yote kuwagusa watanzania wanyonge,

Upinzani wa Tanzania Ni Kama mkanda uliokatika katika ambao hauwezi kupita kwenye rukusi na kufunga suluali, Hauna unachokisimamia Wala kupigania, hauna malengo ya muda mfupi wa Kati na muda mrefu, Hauna hata mikakati ya miaka mitano, Hata kuandaa mgombea Urais tu hauwezi, maana Ni upinzani unakwenda na mdundo wa vijana wake, Ni upinzani unaokwenda kimizuka, Ni upinzani unaokwenda kiharakati harakati kwa kila Jambo, Ni upinzani ambao hauelewi unataka Nini na unapigania Nini zaidi ya kuona kapu la Ruzuku yao likituna,

Ni upinzani unaodaka na kusubili vimatukio vya mpito tu ili uende navyo, Ndio sababu tukio likizimwa kimaridadi na serikali hii shupavu ya mama Samia unaona nao wanapoteana na kuzima, kwa hiyo Ni Rahisi Sana kuwachezesha ngoma wanachama wa kawaida Hadi Mwenyekiti wao Taifa Ndugu Mbowe

Hapa ndipo Rais wetu mpendwa Mama Samia gwiji wa Siasa, mwana mikakati aliyeiva, kiongozi shupavu, mwanadiplomasia nguli, mwenye macho ya kuona mbali, Sauti na mikono ya kupenya popote, Mwenye Akili kubwa na upeo wa mbali, Mtulivu na mwenye kwenda na muda na kusubiri wakati sahihi, mwenye Shabaha na maono ya Mbali,Anayejuwa mbinu na mikakati ya kiuongozi , Rais aliyepikwa ,aliyeiva kimbinu na kimkakati, Mwamba usiyoteteleka Wala kuteteleshwa na mtu yoyote yule, Jemedari shupavu aliyefuzu mafunzo ya kila aina, Tumaini na Tagemeo la watanzania aliyewaweza wapinzani na kuwamaliza upinzani ambao siku zote umekuwa ukitegemea vimatukio

Hakika Rais Samia ameuumbua Sana upinzani wa Tanzania, ameonyesha kuwa Tanzania hakukuwa na upinzani Bali wababaishaji waliokuwa wanategemea mianya kupata ajenda zao, Upinzani umeonyesha kuwa ulikuwa Ni Kama mti uliokosa mizizi, Ni gari lisilo na injini japo limepakwa Rangi nje, Ni mwisho wa upinzani Sasa,

Upinzani wa Tanzania Hauta simama Tena, Hautashamiri Tena, Hautatusumbua Tena, Hautaaminika Tena, Hauta kuwa na mvuto Tena, Haitakuwa Kama 2015, Hautatubabaisha Tena, Hautatulaza macho Tena, Hautavuna Tena wanachama wetu, Hautapata Tena wanachama wenye akili na wenye kujitambua, Hakuna Atakaye toa hela zake kuwapa upinzani Tena, Hakuna Atakaye tokwa jasho kuutetea upinzani tena maana ulishatoka katika mioyo ya watanzania, ulishapuuzwa na vijana ambao ndio ilikuwa nguzo yake kuu, ilikuwa ndio ngao yake kuu na Tumaini lake

Lakini Sasa CCM chini ya Nahodha shupavu Rais Samia ,vijana Wana Imani na matumaini makubwa Sana na Rais wetu mpendwa, vijana wameyaelekeza macho yao kwa mama Samia, watanzania wameamua kuwa bega kwa bega na mama Samia, watanzania wameamua kufanya kazi kwa bidii ili kumuunga mkono mama Samia, watanzania wanamuona Rais Samia Kama mama yao, kiongozi wao, mlezi wao, mzazi wao ndio sababu unaona namna mh Rais Samia anavyoheshimima na kila mtanzania, anapendwaa na kukubalika na kila mtanzania, anasikilizwa na kufuatiliwa na kila mtu,

Rais Samia songa mbele mama yetu,chapa kazi ,tutumikie watanzania, tuhudumie watanzania, tunakuamini, Tunakutegemea,tuna Imani na wewe, usikatishwe Tamaa na wachache
Unajikomba mpaka unatia kinyaa!
Pumbavu
 
DolphinT

JF-Expert Member
Mar 9, 2016
755
1,041
Nilitaka kuandika nikujibu kwa hoja mujarabu Ila nimeona na kugundua kuwa una shida sehemu Fulani na kama wewe ndio aina ya vijana tulio nao katika Taifa hili kwakweli kama Taifa nachelea kusema kwamba tumepoteza mwelekeo!

Katika aya zote ukizoandika hakuna hoja yoyote uliyoitoa inayoonesha kupevuka kwako kielimu na kisiasa.
Nina hakika hata mheshimiwa Rais akisoma ulichoandika atatikisa kichwa na kucheka mwenyewe kwa ujinga huu uliondika ukijazia na makosa ya kisarufi na kiuandishi uliyoyaweka.

Badala ya kutumia muda mwingi kuandika kwa kumpaka mama Mafuta kwa mgongo wa chupa Huku ukishindwa kutanabaisha maadui wakubwa wa nchi hii ambayo na ujinga maradhi na umaskini na sio upnzani kama ulivyokaririshwa, ungetumia muda huu kuainisha maeneo ambayo bado serikali ya mama inapaswa kuyaangalia kwa muktadha mzima wa kuwaletea wananchi maisha Bora kijamii na kiuchumi.

Labda nikwambie tu adui wa Tanzania sio upnzani kwa maana ya hivyo vyama visivyokua CCM, adui wa Tanzania ni mfano wewe unayesifia hata nadharia.

Mwalimu alitutaka vija kuwa jeuri na kuhoji huu ya mstakabali wa nchi yetu. Na sio kukaaa na kusifia hata ambavyo havipo. Elimu uliyo nayo ungetumia kuadress cross cutting issues ambazo watanzania wengi wanapitia ungeheshimika zaidi au hata ungeandika juu ya mafanikio ya serikali ya awamu ya Tano pamoja na mapungufu yaliyopo na namna ya kuaproach hayo mapungufu ungekua sehemu ya bunge la wananchi!

Huwezi kusema wapinzani au vyama mbadala havina sera wakati unajua KABISA Kuna unbalanced political platform Kati ya ruling party na upnzani!

Mtaji wa chama ni wanachama na wanachama ndio wasikiliza sera na ndio wanaoamua!

Kwa mujibu wa Sheria ya vyama vya siasa na kanuni zake Ili chama kiwafikie wanachama aumbao ni wananchi yafaa kifanye mikutano ya hadhara, makongamano na midahalo.

Je, huoni kila wakati havipewi fursa hiyo na jeshi la polis? Wakifanya kwa lazima wanaishia kuawa na kuwekwa gerezani?

Media haziruhusiwi kutumika Ili kueneza propaganda, agenda, milpango na sera za vyama vingine isipokua Ccm! Unataka usikie wapi sera hizo!

Vyama mbadala viliwekwa maksudi Ili kuisaidia serikali iliyoko madarakani kujitazama na kujitathmini pamoja na kujirekebisha Ili isalie madarakani na kukidhi matakwa ya wananchi!

Kwa uandishi wako unaonesha una chuki ya wazi wazi na vyama hivyo na kusahau kwamba Wewe pia ni mtanzania na hao wanachama wasio Ccm ni watanzania ambao ni Ndugu zako rafiki zako nk. Ila kutofautiana ideology kumekufanya uweke tumbo mbele kwa kivuli Cha uzalendo!

Jitathmini Tanzania ni kubwa kuliko wewe
 
Lucas mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
4,672
2,046
Lakini ukumbuke kuwa kwenye CCM hii hii unayoipamba kuna Sukuma gang wengi tu,tunza maneno hata kama teuzi zipo kwa waramba viatu vya watawala.
CCM Ni moja ,wanaccm ni wamoja, chama Ni kimoja chini ya Mwenyekiti wetu shupavu mama Samia suluhu Hassani, Kwa hiyo usitegemee mipasuko ndani ya CCM ukazani utaupa mwanya upinzani, Hakuna aliye mkubwa ndani ya CCM, Sote tunapendana, kuheshimiana na kushirikiana sana
 
DolphinT

JF-Expert Member
Mar 9, 2016
755
1,041
Unajikomba mpaka unatia kinyaa!
Mwashambwa: majina mengine yanasadifu uwezo wa mtu kufikiria.

Kijana kama huyu nilitarajia angetoa Hoka za nguvu ambazo zitaleta mabadiliko chanya katika maisha ya watanzania Ila amebaki kulamba viatu kwa mgongo wa Upinzani.

Nchi hii tuna mambo mengi ya kuiambia serikali na tujivunie inavyoyafanyia kazi badala ya kubweka na kuweka majina kutafuta kutambuliwa na kupewa uteuzi, mama mwenyewe amekataa uchawa.

Tuna mambo anuwai kama:

1. Ukosefu wa Ajira kwa wimbi kubwa la wahitimu wa vyuo vikuu na vya Kati, na kuielekeza serikali namna Gani itengeneze mazingira Bora ya vijana kujiajiri na kuongeza Ajira

2. Ubora wa elimu usioakisi mazingira ya Sasa na Baadae na elimu Hiyo kushindwa kumkwamua mwananchi.

3. Sera za kilimo na biashara.

4.Tozo zisizoakisi kipato halisi Cha mtanzania

5.kupaa kwa gaharama za bidhaa muhimu hasa vyakula.

6. Huduma za afya ikiwemo bima ya afya kwa wote

7. Kikokotoo kwa watumishi wa umma wanaostaafu na kupunjwa pensheni.

8. Miundo mbinu ya usafirishaji ikiwemo maeneo kutofikika hasa wakati wa mvua, pamoja na huduma za maji na umeme!

Hayo ni machache tu ambayo kama kijana ambae unataka mustakabali Bora wa kesho ulipaswa kuiambia serikali na sio Kuja kutupa Habari za Upinzani ambao umefungiwa stoo.

Arudi shule ulksome indicators of development kama ipo inayoitwa kuuwa Upinzani kisayansi aje andike tena hapa.

Villa aibu unaisifu serikali kuuwa Upinzani badlaa ya kuisifu serikali kwa kuleta maendeleo chanya kwa wananchi wake.
 
DolphinT

JF-Expert Member
Mar 9, 2016
755
1,041
Ukweli usipingika huyu ni shabiki na sio hata mwanachama wa ccm
Kwanini:

Hajui katiba na kanuni za chama Cha mapinduzi
Hajui ilani ya chama Cha mapinduzi
Hajui Dira ya maendeleo ya Taifa
Hajui katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na provision zake.

lakini pia hajui wajibu wake kama kijana wa kitanzania na nafasi yake katika nchi hii.
kiufupi ni chawa, anayetafuta kutambuliwa na uteuzi.

Lakini ukumbuke kuwa kwenye CCM hii hii unayoipamba kuna Sukuma gang wengi tu,tunza maneno hata kama teuzi zipo kwa waramba viatu vya watawala.aneno
 
Lucas mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
4,672
2,046
Nilitaka kuandika nikujibu kwa hoja mujarabu Ila nimeona na kugundua kuwa una shida sehemu Fulani na kama wewe ndio aina ya vijana tulio nao katika Taifa hili kwakweli kama Taifa nachelea kusema kwamba tumepoteza mwelekeo!
Katika aya zote ukizoandika hakuna hoja yoyote uliyoitoa inayoonesha kupevuka kwako kielimu na kisiasa.
Nina hakika hata mheshimiwa Rais akisoma ulichoandika atatikisa kichwa na kucheka mwenyewe kwa ujinga huu uliondika ukijazia na makosa ya kisarufi na kiuandishi uliyoyaweka.
Badala ya kutumia muda mwingi kuandika kwa kumpaka mama Mafuta kwa mgongo wa chupa Huku ukishindwa kutanabaisha maadui wakubwa wa nchi hii ambayo na ujinga maradhi na umaskini na sio upnzani kama ulivyokaririshwa, ungetumia muda huu kuainisha maeneo ambayo bado serikali ya mama inapaswa kuyaangalia kwa muktadha mzima wa kuwaletea wananchi maisha Bora kijamii na kiuchumi.
Labda nikwambie tu adui wa Tanzania sio upnzani kwa maana ya hivyo vyama visivyokua ccm, adui wa Tanzania ni mfano wewe unayesifia hata nadharia.
Mwalimu alitutaka vija kuwa jeuri na kuhoji huu ya mstakabali wa nchi yetu. Na sio kukaaa na kusifia hata ambavyo havipo. Elimu uliyo nayo ungetumia kuadress cross cutting issues ambazo watanzania wengi wanapitia ungeheshimika zaidi au hata ungeandika juu ya mafanikio ya serikali ya awamu ya Tano pamoja na mapungufu yaliyopo na namna ya kuaproach hayo mapungufu ungekua sehemu ya bunge la wananchi!
Huwezi kusema wapinzani au vyama mbadala havina sera wakati unajua KABISA Kuna unbalanced political platform Kati ya ruling party na upnzani!
Mtaji wa chama ni wanachama na wanachama ndio wasikiliza sera na ndio wanaoamua!
Kwa mujibu wa Sheria ya vyama vya siasa na kanuni zake Ili chama kiwafikie wanachama aumbao ni wananchi yafaa kifanye mikutano ya hadhara, makongamano na midahalo.
Je huoni kila wakati havipewi fursa hiyo na jeshi la polis? Wakifanya kwa lazima wanaishia kuawa na kuwekwa gerezani?
Media haziruhusiwi kutumika Ili kueneza propaganda, agenda, milpango na sera za vyama vingine isipokua Ccm! Unataka usikie wapi sera hizo!
Vyama mbadala viliwekwa maksudi Ili kuisaidia serikali iliyoko madarakani kujitazama na kujitathmini pamoja na kujirekebisha Ili isalie madarakani na kukidhi matakwa ya wananchi!
Kwa uandishi wako unaonesha una chuki ya wazi wazi na vyama hivyo na kusahau kwamba Wewe pia ni mtanzania na hao wanachama wasio Ccm ni watanzania ambao ni Ndugu zako rafiki zako nk. Ila kutofautiana ideology kumekufanya uweke tumbo mbele kwa kivuli Cha uzalendo!
Jitathmini Tanzania ni kubwa kuliko wewe
Nimejitahidi kusoma andiko lako lotee Kama ilivyo kawaida yangu kusoma maandiko ya watu bila kuchoka, pili ningekushauri uwe unaweka Aya ili iwe Rahisi kusoma kwa mtiririrko mzuri

Lakini pia napenda kukwambia kuwa yote uliyoyaandika Ni upotoshaji mtupu na nitajibu hapa ili uelewe vipi imefanya upotoshaji

Suala la kupambana na maadui watatu wa ujinga umasikini na maradhi Ni kuwa serikali hii ya mama Samia imekuwa ikipambana na kufanya juhudi kubwa Sana katika kukabiliana nao, Ndio juhuzi hizi unazoona za serikali kuamua kujenga zahanati kila Kijiji na vituo vya Afya kila eneo la nchi yetu ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi, Kama ambavyo majuzi tu hapa vituo 234 vimejengwa nchini kwote,

Lakini pia hospitali za rufaa na hata za Kanda zimekuwa zikiboreshwa na hata huduma za kibingwa zimekuwa zikipatikana kwa urahisi tofauti na zamani ambapo huduma hizo ilikuwa Ni mpaka mgonjwa apelekwe nchi za nje, Hali hii imesaidia Sana watanzania kupata huduma hapa Hapa nchini na kuokoa maisha yao kwa msaada wa Mwenyezi Mungu,

Siyo hivyo tu lakini pia vifaa Tiba na dawa zimekuwa zikipatikana na kupelekwa katika hospitali za umma ili watu wasisumbuke kwenda kununua maduka ya mitaani,

Vile vile unaona namna serikali ilivyofanya maboresho katika secta ya Elimu ikiwepo kuongeza shule mpya, ujenzi wa madarasa na hata utoaji wa Elimu bila malipo mpaka kidato Cha sita, hii imesaidia kuongeza uandikishaji wa wanafunzi mashuleni na hata vyuo vikuu mikopo inatolewa vyema na kwa usawa, pia wanafunzi wengi wanapata fursa ya kupata elimu bila kikwazo chochote kile hata Kama wanatoka katika familia za kipato Cha chini

Lakini pia miradi hii imekuwa ikitoa fursa za ajira kwa vijana za moja kwa moja na watu wengine suala linalosaidia hata katika mzunguko wa fedha mitaani hasa kwetu tuliopo mitaani

Ukienda katika kilimo secta Ambayo Ni pumzi ya watanzania walio wengi utaona namna serikali hii ilivyo fanya juhudi kubwa za kuwainua kiuchumi wakulima kwa uamuzi wake wakuongeza bajeti katika kilimo kufikia billioni Mia Tisa na point kutoka billioni Mia mbili huko, lakini pia takribani billioni Mia moja hamsini zimetolewa Kama ruzuku, Hali hii imepelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni na hivyo kumsaidia mkulima kumudu Bei

Kila secta imeguswa na mh Rais wetu mpendwa ambapo matumaini makubwa yamekuja na kunaa katika mioyo ya watanzania, Hakuna anayeachwa nyuma Wala kusahaulika, hapo bado sijazungumzia juhudi za mh Rais kuimarisha secta binafsi, juhudi za mh Rais wetu kuvutia wawekezaji nako imekuwa Ni matumaini makubwa na mafanikio makubwa yaliyo patikana huko

Nitaendelea
 
Nimesoma kila mstari na kila Hoja;
Ukiacha ule uchafu ulioandika katika Uzi wako haya ndio mambo ambayo anagalau ungeandika ili angalau watanzania wakuelewe.

Nilitamani kuwa ungetoa Hoja kama hizi ili kuisifia serikali yako na chama chama Cha mapinduzi!
 
Lucas mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
4,672
2,046
Nas
Nimesoma kila mstari na kila Hoja;
Ukiacha ule uchafu ulioandika katika Uzi wako haya ndio mambo ambayo anagalau ungeandika ili angalau watanzania wakuelewe.

Nilitamani kuwa ungetoa Hoja kama hizi ili kuisifia serikali yako na chama chama Cha mapinduzi!
Nashukuru Kama umenielewa
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Top Bottom