G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,874
Huenda hata wenzetu Uganda wakaja kufanikiwa katika harakati zao dhidi ya dola mapema zaidi kwa kuangalia kuliko Tanzania.
Mbali na upinzani wa Tanzania kuwepo kwa takribani miaka 24 sasa, haujawahi kufanikiwa katika jambo lolote lile ulilopigania dhidi ya dola. Achilia mbali kumbukumbu kuwa upinzani wa Tanzania umekuwa katika harakati nyingi kwa muda mrefu kupita nchi nyingi za ukanda huu.
Kenya walianza wakaweza, na sasa pengine ndilo taifa lenye demokrasia pana zaidi baada ya mataifa kama Ghana na Afrika kusini. Wenzetu Uganda, DRC, Burundi wanaonekana kuwa ni wapinzani thabiti kuliko sisi Tanzania.
Je, ndani ya upinzani wa Tanzania kumepandikizwa virusi? Hata katiba na tume huru tu ya uchaguzi wameshindwa kudai kweli? Wanaonekana kuwa na dira kwa sasa? Waweke wapi uthabiti na waanze na lipi? Kina nani wawe msitari wa mbele?
Mbowe na viongozi wengine wa upinzani waelewe kuwa mengi ya wanayodai hawatapewa kama pipi. Ni lazima wao walale kwanza rumande tena isiyo ya kitoto.Wapewe virungu vya kutosha bila kukata tamaa na wapitie msoto kama wenzao kina Raila na wengine! Wakiogopa hilo basi wasubiri kizazi chenye uthubutu kije kufanya hayo ila wasitarajie badiliko lolote bila kutoka jasho tena jasho litakaloonekana hata na mtoto mchanga aliyezaliwa leo!!