Upinzani wa kweli tuliushuhudia kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 1995 baada ya hapo Wapinzani walichakachuliwa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,599
141,415
Kwa wale tulioshiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 tutakumbuka namna wagombea wa upinzani walivyokuwa makini na wasioyumba.

Wagombea wale waliweza kujenga hoja bila matusi wala kejeli hali iliyopelekea hata mwalimu Nyerere kuwasupport katika baadhi ya majimbo likiwemo la Iringa mjini ambapo Dr Hassy Kitine wa CCM aligombea na mwalimu Kibassa wa NCCR mageuzi aliyeibuka kidedea.

Wapinzani wa leo ni kama vile " wamelewa" ruzuku maana hata uwezo wa kujenga hoja za kudai Tume huru ya uchaguzi na dunia ikawasikia hawana tena.

Wapinzani mamboleo wanategemea zaidi Huruma ya CCM kuliko kujituma.

Ni hayo kwa uchache

Maendeleo hayana vyama!
 
Tunaomjua huyo Mwl Nyerere yaliyo anza kujitokeza uchaguzi wa 2000 na kukithiri 2015 hakika hangeyakubali.

Alikuwa anaweza kuingilia uchaguzi kupindua matokeo sio sababu ya uchama bali usalama wa nchi.
Na hizi tabia za kibedui hangekubali hata kidogo.

Huyu mlie naye angewaambia/wauliza palepale Dodoma "nyie wanaccm hivi bado MNA akili au mumeehuka?"
Uhuni unaouona unasababishwa na ubovu wa ccm

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa yangu anzisha basi chama ujenge hoja maana inaonekana vyama vyote hata kile cha Mzee Rungwe havijakukuna.

Unapoona upinzania hauko sawa, ni vyema ukatumia hiyo kama fursa ya wewe kuingia na kuujenga huo upinzani.
 
Kwa wale tulioshiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 tutakumbuka namna wagombea wa upinzani walivyokuwa makini na wasioyumba.

Wagombea wale waliweza kujenga hoja bila matusi wala kejeli hali iliyopelekea hata mwalimu Nyerere kuwasupport katika baadhi ya majimbo likiwemo la Iringa mjini ambapo Dr Hassy Kitine wa CCM aligombea na mwalimu Kibassa wa NCCR mageuzi aliyeibuka kidedea.

Wapinzani wa leo ni kama vile " wamelewa" ruzuku maana hata uwezo wa kujenga hoja za kudai Tume huru ya uchaguzi na dunia ikawasikia hawana tena.

Wapinzani mamboleo wanategemea zaidi Huruma ya CCM kuliko kujituma.

Ni hayo kwa uchache

Maendeleo hayana vyama!
Nakumbuka nilikuwa Mza mwaka huo uwanja wa Nyamagana ulijaa .Gari la Agustine Mrema lilisukumwa toka nyamagana mpaka iko hotel Capripoint.
 
Back
Top Bottom