Upinzani wa Kenya vs Upinzani wa Tanzania


C Programming

C Programming

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2011
Messages
2,856
Likes
1,941
Points
280
Age
28
C Programming

C Programming

JF-Expert Member
Joined Nov 11, 2011
2,856 1,941 280
JAMANI WADAU LEO NILIPITA SEHEMU NIKAKUTA KUNA SEHEMU WATU WAKIBISHANA WAKIZUNGUMZA KATI YA UPINZANI ULIOPO KENYA NA TANZANIA NA TOFAUTI ZA KISIASA NI UNAUKUBALI ,

LAKINI WAPI KUNA UPINZANI ULIO BORA
 
G

gm manyafu

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2016
Messages
234
Likes
77
Points
45
G

gm manyafu

JF-Expert Member
Joined May 19, 2016
234 77 45
Kenya kwasababu ya katiba yao
 
M

Musoma

Senior Member
Joined
Oct 12, 2010
Messages
137
Likes
165
Points
60
M

Musoma

Senior Member
Joined Oct 12, 2010
137 165 60
T
JAMANI WADAU LEO NILIPITA SEHEMU NIKAKUTA KUNA SEHEMU WATU WAKIBISHANA WAKIZUNGUMZA KATI YA UPINZANI ULIOPO KENYA NA TANZANIA NA TOFAUTI ZA KISIASA NI UNAUKUBALI ,

LAKINI WAPI KUNA UPINZANI ULIO BORA
Tanzania hakuna Upinzani bali kuna "wahemukaji" wa mihemuko!

Utamlinganisha Ababu Namwamba na nani hapa?! Jakoyo Midiwo utamlinganisha na nani hapa? Mwanasheria/Mwanasiasa gani utamlinganisha na James Orengo?!

Profesa gani Mwanasiasa utamlinganisha na Profesa Peter Anyang'i Nyong'o.Hapa hakuna wapinzani bali wengi ni wachumia tumbo walioshindwa maisha kupitia maeneo mengine! HASIRA na KUSUSA muda wote na strategies zingine za kijinga kabisa!

Utasemaje kuhusu strategy ya kijinga ya akina Patrick Sosopi wa BAVICHA ya kwenda Dodoma kuwasaidia eti Polisi kuisimamia CCM kutii sheria bila shuruti!
Mbona hatukuwahi kuwaona wakienda kuwasaidia Polisi kuwatuliza wale majambazi /Al-shababu kwenye mapango kule Amboni- Tanga!

Hali ni mbaya Nchini tangu Rais Magufuli ameingia Madarakani!
1. TRA wanakusanya kodi kwenye MITAJI ya watu badala ya FAIDA.
2.Wafanyabiashara wote wanaonekana ni wezi.
3.Serikali inakusanya fedha lakini haitaki kufanya matumizi!
4.Kwenye kila mradi mkubwa wa ujenzi Rais Magufuli anazo BOQ zake kichwani (Rejea Nyumba za Mahakama na Ujenzi wa Majengo ya Tume ya Uchaguzi NEC).
5.Rais Magufuli hajui tofauti kati ya kazi za Siasa na kazi za Taaluma katika utumishi wa Umma (Civil service) -Rejea hivi karibuni "Baa maid" kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri na watu kibao kuokotwa "vijiweni" kupewa Ukurugenzi na U-DAS bila hata kupitia mfumo wa Utumishi wa Umma (Civil Service system).
Katika udhaifu wote huo Wapinzani wanajadili Mkutano Mkuu wa CCM Dodoma! Upinzani UCHWARA!!!!
 
B

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Messages
5,394
Likes
3,078
Points
280
B

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined Jan 14, 2010
5,394 3,078 280
Kenya hakuna vyama halisi vya kisiasa

Upinzani wa ''kisiasa'' Kenya ni mvutano wa ''Kikabila'' hakuna upinzani wa kweli wa kisiasa kati ya chama tawala na upinzani.

Pia Kenya hakuna vyama vya ''kisiasa'' vyenye mfumo halisi kama idara za propaganda, uenezi, Sekretariati ya halmashauri n.k za kuchagua viongozi kuanzia mashinani mpaka ngazi ya kitaifa katika kaunti (wilaya/mkoa/jimbo).

Vyama vya siasa iwe upinzani au tawala ni vyama vya ''msimu'' ndiyo maana utasikia mwaka huu ''Orange party mwaka mwingine wa uchaguzi ni ODM au Jubilee Alliance ilikuwa KANU.

Vyama hivi vya kikabila a.k.a vyama vya upinzani/tawala huwa vinaangalia wafanye ''muungano'' gani wa makabila mawili au matatu ili kupata namba kubwa ya wapiga kura toka makabila hayo nia ikiwa kushinda kura za uchaguzi.

Pia ''wanasiasa'' wa Vyama hivi vya ''kisiasa'' hutumia muda mwingi katika majukwaa ya ''kampeni'' kwa kushindana kuonesha ufundi wa kucheza ngoma za asili au nyimbo za Bongo ''flava'' kutoka Tanzania badala ya kuuza sera. Ukiweza kucheza ngoma kwa umahiri katika kabila uliloamua kujiunga nao ''kisiasa'' wazee wa mila wanakutangaza ''unatosha'' na wananchi wa eneo hilo bila hiyana watakupa kura kwa asilimia 95%

Vyama hivi vya siasa (Kikabila) hubebwa zaidi na kuwekwa pamoja na ''wazee'' maarufu wa kikabila ambao hutoa maamuzi nani anafaa kutetea ''ulaji'' wa kabila lao na kusimikwa kama viongozi wa ''kisiasa''.
 
S

sombrelo

New Member
Joined
Jul 12, 2016
Messages
2
Likes
0
Points
3
S

sombrelo

New Member
Joined Jul 12, 2016
2 0 3
Wapendwa wiki ijayo kiongozi wa upinzani Raila Odinga atafanya jumla ya mikutano 31 ya hadhara jimbo/mkoa wa western kenya kipindi cha wk 1. Kwa mujibu wa katiba yao hawahitaji kuomba kibali na ulinzi wa polisi ni guaranteed. Sikukuu ya Madaraka Day wapinzani kenya waliendesha sherehe zao nairobi. unapolinganisha hali ya upinzani zingatia katiba na utashi wa kisiasa baina ya kenya na tanzania.
 
comrade igwe

comrade igwe

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2015
Messages
7,268
Likes
3,768
Points
280
comrade igwe

comrade igwe

JF-Expert Member
Joined Jan 12, 2015
7,268 3,768 280
JAMANI WADAU LEO NILIPITA SEHEMU NIKAKUTA KUNA SEHEMU WATU WAKIBISHANA WAKIZUNGUMZA KATI YA UPINZANI ULIOPO KENYA NA TANZANIA NA TOFAUTI ZA KISIASA NI UNAUKUBALI ,

LAKINI WAPI KUNA UPINZANI ULIO BORA
Mlete uzi hapa ungeanza kunyambulisha sana kuanzia dhana nzima ya Upinzani, Malengo na nia ya upinzani pande zote ndio na mm student niangalie pa kuanzia then unatuachia swali
 

Forum statistics

Threads 1,235,909
Members 474,863
Posts 29,240,266