Upinzani usipochukua Nchi 2015, hautaweza kuchukua nchi tena kamwe!

hippocratessocrates

JF-Expert Member
Jul 1, 2012
3,598
1,539
Wasalam wanajamvi!

Heka heka za viongozi kutoka chama kimoja cha siasa kwenda kingine zinaendelea.

Tofauti na miaka ya uchaguzi iliyopita mwaka kuanzia mwaka1995 hadi mwaka 2010, mwaka huu umekuwa wa aina yake. Pamoja na miaka mingi chini ya utawala wa CCM, Upinzani umeonekana ukijidhatiti vilivyo na hii ikifanya chama tawala kuwa katika wakati mgumu. Nionavyo mimi, Endapo kwa mwaka huu Upinzani hutaweza kushika dola pengine hautaweza kabisa katika miaka ya usoni.


1. Muungano wa vyama vya siasa:
Umoja wa Katiba ya Wananchi(UKAWA) ukiunda na vyama vinne yaani CHADEMA, NCCR-Mageuzi, NLD na CUF ni mojawapo ya tishio kubwa kwa chama tawala (CCM). Mpango mkakati wao uliotumika wa kumpigia kura mgombea mwenye 'kukubalika zaidi' ni jambo ambalo CCM wenyewe hawakulitarajia(wengi walitegemea kuwa muungano uwe wa chama kimoja cha siasa), kumbuka NARC-Kenya 2004. Ingawa viongozi wa juu wa 'mchakato' wameonyesha kusita mwishoni, 'moto' waliouwasha miongoni mwa wanachama si rahisi kuuzima.

2.Mpasuko ndani ya CCM:
Ingawa katika Mkutano mkuu pale Dodoma, Mwenyekiti wa CCM alisema hakuna makundi na hakuna timu nyingi, ila ni wamoja na kuna timu moja tu timu CCM, ni dhahiri alikuwa mkaidi kukubali au kabisa hajui hali ya chama anachokiongoza. Mpasuko ndani ya chama ulikuwepo hata kabla ya watangaza nia kusema yao ya moyoni! Na udhaifu huu umeonyeshwa kwa chama hiki komavu(kiumri) kushindwa kumuandaa watakaomrithi Mh. JK Mrisho, matokeo yake kuwa na utitiri wa watangaza nia ndani ya chama kimoja kwa kile wanachookiita ni "demokrasia imekua ndani ya chama!" lakini pia kauli mbaya pia kama "Makapi" bado zinaendekea kuleta ufa mkubwa.


3. Uelewa wa Wananchi:
Tofauti na miaka ya nyuma, elimu ya uraia imeeleweka kwa kiasi chake mijini na vijijini. Hii inafanya pia mwananchi mbali na kujua wajibu wake kutambua kujua haki yake na umuhimu wa nafasi aliyonayo katika kuleta mabadiliko katika Taifa. Mwamko umekuwa mkubwa katika midahalo na takribani mikutano ya vyama vyote vya siasa.

4. Nafasi ya vyombo vya habari:
Tofauti na miaka ya nyuma kidogo, ambapo tulitegemea Redio na magazeti, upatikanaji wa habari kupitia mitandao, luninga/televisheni, n.k kumefanya taarifa zinazokusudiwa kuwafikia wananchi. Ingawa kumekuwa na vyombo vya habari(magazeti, televisheni) vilivyo/vinavyoegemea upande fulani tu, (kwa sababu ya namba tatu hapo juu), mwananchi ameweza kujua wapi pa kupata habari kwa wakati na kwa usahihi tofauti na miaka ya nyuma.

5. Uandikishwaji wa wapiga kura.
Kujitokeza kwa wananchi wengi katika zoezi la kupata kitambusho cha mpiga kura ingawa muda kuwa mfupi mikoani, na ugumu wa zoezi lenyewe bado wananchi wali/wameonyesha jitihada binafsi (hata kwa kulala vituoni). Wengi wa waliojitokeza ni vijana(likiwepo kundi kubwa la wasio na ajira, waliokata tamaa na Serikali).

6. Migomo:
Tofauti na miaka ya nyuma Serikali iliyokuwa madarakani ilikuwa na sauti na kuweza kusikika ikitoa suluhu kwa matatizo nchini, Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita tumeshuhudia migomo mingi (kwa kada na tasnia mbalimbali), hii ikitatuliwa na viongozi wa Upinzani (Ingawa baadhi walidhani /waliamini kuwa Upinzani ndiyo wako nyuma ya migomo hii.)


Mkuu wa nchi amesema 'maarifa' wanayo na wapinzani watakiona cha 'mtema kuni' bado kuna sababu nyingine nyingi zenye kuonyesha nguvu kubwa ya Upinzani na udhaifu wa chama tawala. Ni hakika CCM imejeruhiwa vibaya na iko hatarini kupoteza 'uhai' lakini kama ikijinasua kamwe Upinzani wasitegemee kushika nafasi.
 
Kwa mwenendo huu wa kulazimisha matokeo(ucheleweshwaji wa makusudi, kutowalipa mawakala hadi pale watakapotangaza matokeo ya chama fulani ndiyo washindi, kufunga barabara, kuwatawanya wananchi kwa mabomu wakiwa wanasubiri matomeo bila fujo na kisha kutangaza matokeo, nk)

Haya yote kutokea, tutegemee ASSASSINATION nyingi kutokea.Na watu kutofautiana kwa kila hali makazini, mitaani(watu kuogopana kwasababu ya tofauti za vyama wakionana kama maadui na si watu wenye tofauti katika kuleta maendeleo kwa taifa).
 
Mbaya zaidi...! Roho na vitendo vya kikatili vitaongezeka kwa wale waliolazimisha ushind,i maana wanajua hawakuungwa mkono na wapiga kura ; hivyo hawatawaonea huruma ...!! Watajiona wako juu ya kila kitu ! Kwa ukatili huo, kulipizana kisasi kutakuwepo na hapo ndipo ninapoona kwa mbali ukweli kwenye bandiko lako namba mbili. Kuepusha hili ni wenye mamlaka ya kutangaza matokeo watangaze matokeo halisi...!
 
Back
Top Bottom