Upinzani unaweza kuwa imara zaidi ndani ya utawala wa Magufuli

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,157
Tangu serikali ya tano ishike hatamu, watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa, wachambuzi wa siasa na wasomi wa kada mbalimbali wamepaza sauti zao kuwa kumekuwa na ukiukwaji wa demokrasia na kuminywa kwa haki za vyama vya siasa kufanya "SIASA" ili kuendelea kujiimarisha zaidi.

Ni ukweli usiopingika kuwa kumekuwa na tofauti sana kati ya utawala huu na utawala uliopita juu ya mtazamo na kuthamini uwepo wa siasa zinazoikosoa na kuipa changamoto serikali. Kwa haraka haraka ni kama serikali hii haioni kama upinzani wanamchango wowote katika kuihudumia jamii wanayoiongoza. Kifupi serikali inaonekana inajiamini inaweza kufanya vizuri zaidi hata kama vyama vya upinzani vingefutwa tangu juzi na kwa bahati mbaya Upinzani nao nikama wamekosa "plan B" kwani kila leo wao nikulalamika tu na hakuna hatua "madhubuti" zenye mashiko wanazochukua ili kuendelea kujiimarisha na kuaminiwa zaidi.

Mwenendo wa serikali hii unaweza kuwajenga upinzani zaidi kuliko hata inavyoonekana machoni pa wengi kwamba upinzani huenda ukajeruhiwa. Kwa mfano, kwa sasa wamekatazwa kufanya mikutano ya hadhara na maandamano na Bungeni sheria zinaonekana kuwabana wao sana kuliko umuhimu wa michango yao.

Kitu wanachotakiwa kufanya ni kucheza kila ngoma nzuri inayochezwa na serikali kwani serikali hii inaonekana kupenda kusifiwa zaidi. Wasisubiri kuja kukosoa na kupaza sauti pale serikali wanapoboronga tu! Wasipende kukosoa kila kitu kinachofanywa na serikali, wapongeze vile ambavyo hata jamii inaona serikali iko sawa kwa mfano ishu ya madawati wangeitumia kama "KICK" kwa sasa na wakajisahaulisha kwa muda sarakasi za Bungeni! na pale serikali inapoenda kombo wafumbe macho kidogo kwa kuchungulia "reactions"kutoka kwenye jamii wanapoona mwitikio wa miguno ndipo waje hadharani kukosoa kwa nguvu zote lakini kwa akili.

Lakini wakijikita kuikosoa serikali tu kila siku bila hata kuungana kwa yale yanayoiunganisha jamii, upinzani huenda wakapata jeraha ambalo kulitibu linaweza kuwagharimu. Ni vema wakiwekeza kwenye mbinu za kujua kula na kipofu kwa sasa kuliko kitu kingine chochote kwani teuzi hizi hakika serikali wanampango mkakati ambao kambi ya upinzani hawana namna ya kuuzuia kwa sasa.
Ni hayo tu kwa leo.
 
Andiko lako limekosa mantiki, kwa kuwa umechanganya mambo. Haijulikani unataka kufikisha ujumbe gani. Kaa chini lipitie upya halafu ndio uje hapa.
 
Back
Top Bottom