Upinzani unatoka kwenye Agenda bila kujielewa

GJHariohay

JF-Expert Member
Oct 24, 2013
1,038
2,000
Habari zenu mabibi na mabwana.

Nimefuatilia kwa utulivu mjadala wa ununuaji wa wabunge na viongozi wetu unaoendelea majukwaani. Mjadala huu umeonesha wazi kuwa wapenda mabadiliko wamefikia hata kukata tamaa.
*Hapana msikate tamaa!*

Naomba niahirishe maumivu yenu kwa muda wakati dawa kamili inaendelea kutengenezwa.

MOSI.
Msipige ramli ni nani anaondoka. Wala msihukumiane kabla ya wakati. Kushukiana bila uthibitisho kunaweza kutugawa na mwisho kutunyima kupambana kwa pamoja.

PILI
Msiwalilie wanaoondoka. Jililieni ninyi na wapiga kura wenu. Biblia inasema *"walikuwa kwetu lakini hawakuwa wetu"*Bebeni mzigo na uchungu wa wapiga kura wenu na pangeni namna ya kulinda imani yao kwenu.

TATU.
HESHIMUNI WABUNGE.
Wabunge ni viongozi wa kisiasa wenye hadhi ya juu na majukumu makubwa katika jamii. Mnapowasemasema na kuwatamka kwa maovu ambayo hamna uthibitisho kwayo mnawaumiza mioyo yao. Subirini ithibitike ndipo muwatuhumu.

NNE
Kabla sijaja jukwaani kufundisha somo la kujichuja kwa chama, naomba kuwahakikishia kuwa ununuzi huu wa viongozi wetu ni tafsiri ya wazi ya kukua kwa chama. Hakuna kocha anayenunua mchezaji kutoka timu mbovu isiyo na viwango.

TANO
Baada ya CCM kufilisika sana, sasa haina jingine la kufanya isipokuwa kuficha taswira yake. Hapa wanahangaika kunyamazisha wakosoaji na kununua watu wakuisemea vizuri. Sina uhakika kuwa hili ni jukumu linalotekelezwa na CCM kama chama au serikali yake.

Chama makini kikiingia madarakani kinatumia dola kutekeleza ilani yake kwa lengo la kufikia malengo ya taifa.

SITA
Wanaoondoka waende salama. Watuache wachache watakaoifikisha Tanzania *Kaanani.* Hatuwezi kwenda wote hadi pale.

Kuna watakaobaki njiani wakila nyama na kuhangaika na mizoga inayooza punde. Kuna watakaougua njiani kwa maradhi ya pepo za kusi. Kuna watakaokufa kwa mishale ya mfalme na wana wa mfalme.
Lakini iwe iwavyo *"we as a people will reach the promised Land"*
Tutafika msiogope.

Mnaoteswa na maisha yenu kuwekwa rehani msiogope, saa yaja majina yenu yatang'aa mbele ya taifa.

Iweni na siku njema na tafukari njema.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom