Upinzani Unapopinzana (Unapohujumiana)

Nonda

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
13,370
4,297
Kwanza, ninawasalimu wakuu

Kwa muda mrefu nimekuwa nikitupia jicho jf. Nimejionea mengi. Nimejifunza mengi.

Wakati uchaguzi unakaribia nimeona jf ilipata wanachama wengi. lakini vilevile nimeona mada zinazowasilishwa zinalenga ushabiki zaidi wa kivyama. Tetesi pia zimeongezeka. Udini umeanza kupigiwa tarumbeta. Tunakwenda wapi?

Jambo moja lililonihuzunisha sana mimi kama M-tan-zan-ia ni kuona vyama vinavyojiita vya upinzani vinapigana vijembe, vinahujumiana, vinadharauliana. Hali hii inaonesha kuwa ukomavu wa kisiasa na ushawishi wa kisiasa bado ni mdogo katika vyama hivi. Hali hii inainufaisha CCM na inawaacha njia panda Watanzania ambao wanategemea vyama vya upinzani viwe vipaza sauti vyao, lakini pia watanzania wanategemea kuwa vyama hivi viwe mbadala siku CCM watakaposalimu amri.

Tuna vyama vikuu vya upinzani viwili CHADEMA na CUF, aidha vipo NCCR, TLP, UDP.

Baada ya uchaguzi kumalizika ni wazi CHADEMA na CUF ndivyo vyama vikuu vinavyoonekana kuwa ni changamoto kwa CCM.Lakini inaonekana kuanzia viongozi wa vyama hivi, wanachama wao na wapenzi wao wameingia katika malumbano ambayo kwa kifupi tunaweza kuyafupisha na kuyaita "VITA VYA PANZI".

Sote tunaelewa kuwa kuendelea na vita hii ni kuwa tunawatowa mhanga Watanzania wanaotaka mageuzi ya kweli na "KUNGURU" anachekelea hili. Ni kuwa CCM wataendelea kutawala kwa miongo kadha.

Tusitegemee kuwa hata kama CHADEMA na CUF watashirikiana kuwa hakutakuwa na tofauti lakini viongozi wa vyama hivi wanaweza kuwa na "common tone" na hapo ndiyo itaonekana kuwa wapo hapo kuwakilisha watanzania na siyo matakwa yao kichama au binafsi.
Tanzania ni kubwa kuliko chama chochote na kuidondosha CCM kuunda serikali Tanzania kunataka kazi. Kazi kweli kweli.

Kwanza bila ya Katiba Mpya itakayoshirikisha wigo mkubwa, umma wa watanzania katika kuiandika basi upinzani usahau kuingia madarakani kwa amani.Watanzania tusisahau jina kamili la CCM. MAPINDUZI ndio msisitizo. Katiba mpya najuwa ni agenda ambayo CHADEMA na CUF wanakubaliana.

CHADEMA na CUF wana sera ya Serikali Tatu.

Kuna sababu gani ya msingi inayowafanya wasikae pamoja kushirikiana katika kusukuma mbele agenda hizi? Katiba mpya ndani ya miaka miwili, tume huru za uchaguzi, Serikali tatu kwa Tanzania.

UMOJA ni NGUVU na Utengano ni udhaifu.

Kama ni milioni 200 au 100 za kuongoza upinzani, mnashindwa kuona mbali. mkiingia madarakani kuna mabilioni.

Kama tatizo ni kuwa CUF wamefanya muafaka na CCM basi CHADEMA hasa viongozi walipaswa kukaa na wenzao wa CUF kuwadadisi, kujifunza na kubadilishana nao mawazo kuona vipi wamefikia kushirikiana na CCM katika kuunda Serikali kule Zanzibar. Nani hajuwi kuwa Zanzibar kwa miongo kadhaa imekuwa na hali tete? Nani hajuwi kuwa CCM wanaposhindwa katika uchaguzi kupitia kisanduku cha kura huwa wana-back up plan?

Hekima, uwazi, kuaminiana na kuheshimiana kwa viongozi wa vyama vya upinzani inaonekana viko katika kiwango cha chini. Mnaweza kupingana bila ya kupigana. Pinganisheni hoja, changianeni mawazo kuona vipi mtawaletea watanzania afueni ya maisha...sizungumzii "maisha bora au maendeleo". Hayo yatawezekana tu pale Serikali Zetu Tatu zitakaposimikwa/ zitakapoundwa kupitia katiba mpya, tume huru za uchaguzi, nakuwepo mfumo mzuri wa mgawanyo wa madaraka wa mihimili ya dola.

Otherwise, Itakuwa ni kuganga njaa tu.

CHADEMA na CUF hamna haja ya kutoleana aibu zenu, kejeli au name calling kwenye viriri au vyombo vya habari. Watanzania hawatunufaika kwa hili isipokuwa wapenda mipasho na kuongeza furaha ya "KUNGURU". Kaeni chini, mjadiliane..mtakapotoka kwenye vikao vyenu muje na kauli za matumaini kwa Watanzania siyo kuendeleza kuwakatisha watu tamaa ya maisha. Kwa hilo CCM hawataki wala hawahitaji msaidizi. Si tumeona ndege ya uchumi inapaa na maisha bora kwa kila Mdanganyika? Wenyewe wanajuwa Watanzania ni kama kichwa cha mwendawazimu.Wanatubadilishia wimbo (kauli mbiu(, sisi tunaendelea kutimkwa!!! Tunacheza mdundiko!! Wao wanachana life!!!

Let us bring change!

Nawasilisha wakuu.
 

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,524
13,099
Mkuu nimekusoma.Nadhani kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa hapa JF utagundua hisia za wananchi.Kwa kifupi ni kwamba CUF ni mamluki wa CCM.Chadema hawawezi kushirikiana na mamluki ambao wao mafanikio ni kuongoza tu Zanzibar.CUF ni sehemu ya utawala wa Tanzania.Kuishirikisha CUF siri yoyote ni kuiuza kwa watawala na CCM.Kama ungefanikiwa kufuatilia mdahalo wa Mbowe na Hamad ungegundua kwamba CUF ni kwapa la CCM.Kwa mpenda demokrasia na mwanamageuzi yoyote hawezi kukubali CUF kushirikiana na Chadema.
 

Madela Wa- Madilu

JF-Expert Member
Mar 24, 2007
3,063
725
Nonda.

CUF wameolewa na CCM.
Ugomvi mkuu hapa ni kwa nini wanalala kitanda kimoja na CCM halafu wankuja kutaka uchumba CHADEMA?
Kule mtaani tabia hii tunaiita umalaya, hapa JF sijui tunaiita nini??
Hii si Vita ya panzi CHADEMA ndo chama Rasmi cha Upinzania Bungeni lakini si chama pekee cha upinzani.
Wapinzania kuwapinga wapinzania ni kitu cha kawaida katika Mabunge yote duniani.
Kila chama kina jua kwa nini kimo katika kambi ya upinzania.
Kama wote mnapinga katika namna moja kwa 99% nilazima mtaunda chama kimoja tu.
hakuna hujuma wala nini ndo mwendo mdundo katika kambi ya upinzani.
 

lebabu11

JF-Expert Member
Mar 27, 2010
2,460
1,701
CCM, CUF, CHADEMA,NCCR,TLP na vyama vingine vyote vya siasa vilivyopo Tanzania ni vyama huru tangu vilipoanzishwa vikiwa na lengo la kuongoza nchi vyenyewe bila ulazima wa kuungana. Hata hivyo vina hiari ya kuungana au kushirikiana.
Kama CCM walivyoshinda kuunda serikali, CHADEMA wana idadi inayotosha kuunda serikali kivuli kulingana na kanuni na hivyo hawawezi kulazimishwa kushirikisha chama kingine.
 

Mundali

JF-Expert Member
Sep 16, 2010
749
164
Siasa za Zenji ni muendelezo wa siasa za nchi kadhaa za afrika zinazoiga demokrasia. Hii mifumo ya kidemokrasia wapendwa tumeiga tu toka ughaibuni. Tawala zetu za kiasili ni za machifu na ndio maana mfumo huo umeendelea mpaka leo. Nadhani mnaweza mkanipata vibaya hapa lakini ukweli unabaki kwamba tuna utawala wa kichifu katika jina la demokrasia. Utawala wa machifu ni wa kurithi ambapo mtawala aliye madarakani ndiye mwenye mamlaka ya kupendekeza mrithi wake. Kwa upande mwingine, serikali zenye mfumo wa kichifu kama hizi zetu chama kilichopo madarakani ndicho chenye haki ya kuweka watawala kwa kiini macho cha uchaguzi. Hali hii huwezeshwa na utungaji wa sheria kandamizi, kuhodhi vyombo vinavysimamia chaguzi hizo, kudhibiti watendaji wakuu wa vyombo hivyo. Rejea Zimbabwe, Kenya, Afrika ya kati, Uganda, Rwanda, Tanzania. Ili kulinda maslahi ya machifu ushindi hulazimishwa kwa gharama yoyote na hata kwa kuwanunua wapinzani wa machifu na kuwapa vyeo serikalini (mfano zanzibar, kenya, zimbabwe). Dhana ya upinzani huwekwa na watawala ili kuhalisha utawala wao, ni iwapo chama mbadala kinakuwa na nguvu kubwa machifu hufanya juhudi za kununua viongozi wake.
 

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
225
CCM, CUF, CHADEMA,NCCR,TLP na vyama vingine vyote vya siasa vilivyopo Tanzania ni vyama huru tangu vilipoanzishwa vikiwa na lengo la kuongoza nchi vyenyewe bila ulazima wa kuungana. Hata hivyo vina hiari ya kuungana au kushirikiana.
Kama CCM walivyoshinda kuunda serikali, CHADEMA wana idadi inayotosha kuunda serikali kivuli kulingana na kanuni na hivyo hawawezi kulazimishwa kushirikisha chama kingine.

Hakuna haja ya kulazimishana kushirikiana. Naamini CUF hawakulazimishwa kuridhiana na baadaye kushirikiana na CCM huko Zenj, walifanya hivyo kwa ridhaa yao wenyewe. Hivyo hivyo Chadema hawawezi kulazimishwa kushirikiana na chama chochote katika Kambi ya upinzani! FULL STOP!!!

And that should be loud and clear to every one.
 

Mahesabu

JF-Expert Member
Jan 27, 2008
5,504
1,740
NONDA.......bado hatujakuelewa...tafuta kinywa utumbukize maneno haya haya..... kwenye magazeti yatakuwa front page...!
PROF SHIVJI......AZAVERY ET AL.....!
 

Nonda

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
13,370
4,297
Nonda.

CUF wameolewa na CCM.
Ugomvi mkuu hapa ni kwa nini wanalala kitanda kimoja na CCM halafu wanakuja kutaka uchumba CHADEMA?
Kule mtaani tabia hii tunaiita umalaya, hapa JF sijui tunaiita nini??
Hii si Vita ya panzi CHADEMA ndo chama Rasmi cha Upinzania Bungeni lakini si chama pekee cha upinzani.
Wapinzania kuwapinga wapinzani ni kitu cha kawaida katika Mabunge yote duniani.
Kila chama kina jua kwa nini kimo katika kambi ya upinzania.
Kama wote mnapinga katika namna moja kwa 99% nilazima mtaunda chama kimoja tu.
hakuna hujuma wala nini ndo mwendo mdundo katika kambi ya upinzani.

Mkuu.
Kusema kuwa CUF wameolewa na CCM ni upotoshaji wa historia yote tokea vyama vingi viliporuhusiwa tena Tanzania au ni kuepuka kufikiri kwa makini!
Pia kusema CUF wanakuja kutaka uchumba na CHADEMA pia ni kufurahisha na kufurahisha wanaJF na wale wanaopenda kuona kuwa upinzani unajenga picha ya vurugu na migogoro tu.
Tuchukulie mfano wa Kenya. Unaweza kusema kuwa Chama cha Raila au muungano wa vyama alioungoza wameolewa na Chama Cha Kibaki ?au wako katika uchumba na Kibaki?

Chimbuko la CUF na CCM kuunda serikali ya GNU Zanzibar ni muafaka (maridhiano). Huu sijuwi ni mwafaka wa ngapi? La kufurahisha ni kuwa makubaliano yao yamepitia hatua nyingi. Yalianza na vikao baina ya CCM na CUF na yakapelekwa katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Huko yakapata baraka za wawakilishi wa wananchi na wananchi wa Zanzibar wakapiga kura kuridhia baada ya Uchaguzi (Uchafuzi!!??) iundwe hiyo serikali ya Umoja wa Kitaifa "GNU". Wazanzibari wamechoshwa na migogoro, mipasuko, kero zisizokwisha.

Ukitaka kujikumbusha ni vyema kupitia Mgogoro wa Zanzibar, ulianzia baada ya uchaguzi (uchafuzi) wa 1995. Leo tunazungumza ni 2010.

Ndiyo katika mada niliyoiwasilisha nimeonesha kuna mambo ya msingi; Katiba Mpya, Tume huru ya uchaguzi, serikali tatu. Haya pekee kama kweli wanania na niwakweli yanatosha kuwafanya juu chini kuona wanashirikiana katika kuyafanikisha. Sisemi kuwa ni jambo rahisi lakini Uongozi maana yake nini?
CUF wana wanadiplomasia wazuri ambao wameweza kuzishawishi nchi wahisani kuibana Serikali ya Mkapa na Kikwete kuleta suluhu Zanzibar.

CHADEMA wana malalamiko kama waliyokuwa nayo CUF tokea 1995. CHADEMA inaonekana wanawanasheria wazuri. watakapoamua kushirikiana katika kuzipa msukumo unaostahili agenda hizo tatu. Wakiunganisha nguvu na kidiplomasia, za kiuanasheria na wabunge walionao katika BUNGE basi 2015 tutazungumzia mabadiliko makubwa ya maana katika Tanzania!

CUF , CHADEMA na vyama vyengine vya Upinzani ni lazima viache siasa za maji taka. Na watakapojenga hoja zenye nguvu na kutumia lugha ya kuheshimiana na kistarabu hata CCM watatega sikio. Binadamu ana uwezo wa kubadilika.

Natumai nimechangia mawazo ili tuone wapi tunakwenda na vipi tutafika huko. Mageuzi au mabadiliko si lele mama!
 

Nonda

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
13,370
4,297
Hakuna haja ya kulazimishana kushirikiana. Naamini CUF hawakulazimishwa kuridhiana na baadaye kushirikiana na CCM huko Zenj, walifanya hivyo kwa ridhaa yao wenyewe. Hivyo hivyo Chadema hawawezi kulazimishwa kushirikiana na chama chochote katika Kambi ya upinzani! FULL STOP!!!

And that should be loud and clear to every one.

Mkuu,
Ukelele uliopiga nimeusikia na nimeuelewa.

Ni kweli CUF hawakulazimishwa na mtu kushirikiana na CCM kuunda Serikali ya Umoja wa kitaifa. Na ni upotoshaji wa hali ya juu kuwaaminisha wananchi kuwa CUF wanashirikiana na CCM kama Vyama katika maana halisi ya "chanda na pete". CUF wamefikiria Kitaifa zaidi na hawakujikita kichama katika maamuzi haya. Unaposhindana na kichwa ngumu kama CCM ni lazima ubadilishe tactics na strategies.

Hali ya kimazingira iliyoikumba Zanzibar kwa muda mrefu ndio imelazimisha CUF na CCM kuunda serikali ( sio vyama, au chama) shirikishi. Vyenginevyo zanzibar ingekuwa bado hii leo imo katika hali tete, mgogoro, mpasuko mwengine. Walichofanya CCM na CUF ( kwa hisani kubwa ya CUF na ukomavu wake wa kisiasa) ni kuepusha umwagaji wa damu unaotakana na ubadilishaji wa matokea ya Uchaguzi.Pia kutokana na yale CCM waliyokuwa wameyapanga (back up plan) walikuwa -caught by a surprise na compromise ya CUF. Kwa hili nafikiri timu ya CUF inastahili pongezi. Unafikri CCM wamependa kukaa meza moja na CUF? na nakuhakikishia CCM wakipata mwanya watayaharibu maridhiano kule Zanzibar. mkuu unataka kujifanya huwajuwi CCM? Wanaona Tanzania ni milki yao peke yao na mpinzani ni adui.

Fikiria ule umati uliokusanyika pale Bwawani siku ya kutangaza matokeo ya uraisi wa zanzibar. Tungepeleka body bags ngapi? Kwa zanzibar watu 20 ni wengi sana lakini hata maiti moja ingekuwa ni too much. Si tulimsikia Mkapa Jangwani akisema ni lazima serikali ya Zanzibar iongozwe na CCM?
CUF wameweka mbele maslahi ya Taifa kama vile CHADEMA walivyoamua kuwanasihi wananchi na wanachama wao wasiingie mitaani kupinga uchakachuwaji uliofanyika katika uchaguzi uliokwisha.

Nina imani kubwa kuwa kuna uwezekano kwa Zanzibar kupata tume huru ya uchaguzi kabla ya kuwa na tume huru ya uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano wa Tan-Zan-ia.

Upinzani wakiungana au kushirikiana ni kwa faida ya taifa , wakiendelea na malumbano watachezea mkong'oto, kisago mmoja mmoja kutoka kwa CCM na serikali yake. Anaeumia zaidi ni mwananchi wa kawaida.

Kwa hiyo, bado ninaamini kuwa kuna faida kwa upinzani kuunganisha nguvu zao, kushirikiana katika common ground, kudai katiba mpya, tume huru ya uchaguzi within 2-3 years. Tukiingia katika Uchaguzi wa 2015 bila ya hayo, tutarajie nini? Uvunjfu wa amani, maafa kwa Taifa? Au CHADEMA wanamiujiza gani ya kuifanya CCM isalimu amri?
Bado huoni umuhimu wa upinzani kuwa na sauti moja?
 

Nonda

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
13,370
4,297
NONDA.......bado hatujakuelewa...tafuta kinywa utumbukize maneno haya haya..... kwenye magazeti yatakuwa front page...!
PROF SHIVJI......AZAVERY ET AL.....!

Mkuu kama hufanyi utani basi ni PM ili unipe muongozo. Nipo tayari kujifunza.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom