mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,666
Kwa kutambua au kutokujua; kelele, kebehi, lawama, shutuma na aina hiyo ya mtizamo wa Vyama vya Upinzani, bila shaka unaijenga na kuimarisha Serikali mpya ya CCM ikiongozwa na Dr Magufuli (hapa kazi tu#). Kwani:
1) Lawama nyingi ni za utendaji ambao haukuwa wa kuridhisha wa Serikali iliyopita.
2) Serikali ya Magufuli katika kurekebisha hali hiyo, inashutumiwa kutenda kinyume cha sheria.
3) Kwa mstakabala huo, Serikali inapata shavu kutoka kwa wananchi waliokua wamekwisha kukata tamaa.
4) Kwamba agenda ya UPINZANI ya mabadiliko inabaki kwenye vinywa vyao na makaratasi, huku na kwa wakati, Rais Magufuli akileta mabadiliko ya kweli kwa vitendo.
USHAURI:
Iwapo nia ya UPINZANI ni kuiumbua Serikali iliyopo sasa madarakani, ili kujiwekea matumaini ya kushika dola, basi ni busara kusubiri marejesho ya bajeti yake Magufuli mwakani ili kuwa na agenda nzito dhidi yake na Serikali, kama/iwapo atakuwa ameshindwa kufikia malengo aliyojiwekea (tafsiri ya bajeti ya Serikali yake). Kwa sasa si wakati mwafaka wa kuibeza Serikali ya sasa kwa vigezo vya utendaji wa serikali iliyopita.
CHAMBUA CHUNGUZA AMUA CHUKUA HATUA