Upinzani ulikufa na Dkt. Slaa na Zitto Kabwe

Jumong S

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
7,312
10,492
Ndiyo kwanza msosi ulikuwa umeandaliwa. Mara nikasikia vipaza sauti, " Rais anawasiliiiii" niliacha ugali wangu na Sato nikakimbia Kama swala. Watu walikuwa wengi from town na vijijini. Watu walisafiri takribani 50Km kuja kumsikiliza Dr Slaa! Alianza ZZK kumwaga mawe, naye akamkaribisha Mbowe ambaye alimkaribisha Rais Tarajali. Alipopokea Mic alianza kwa kufuta machozi....."Si..ja..wahi ku..ona watu wanaonipenda Kama nyinyi"

Aliongea mazito huku tukishangilia. Nilipata tabu kumuona but mti niliopanda ulinisaidia. Those were the ages when Upinzani ulikuwa hot, upinzani halisi. Mtu akiongea Sera zinakugusa moyoni! Unatamani asimalize but giza lilitukatili. Nautamani wakati ule! Walipoanza kuvurugana now naenjoy movies tu na mpira!

Nikimsikiliza Lissu na Membe naona kama ni waigizaji wa Ze Comedy wanaburudisha jukwaa! Very few contents, mihasira na back agendas! Lissu wa Leo Tabora unaona kabisa analazimisha!

Tanzania bado sana kuwatoa CCM! Labda Kuna kizazi chaja kinachojielewa otherwise come 28th Oct tumpigie kura Mzee Rungwe tukajilie Ubwawa na kuku wa kienyeji na kapilipili kwa mbaliiii.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom