Upinzani Tanzania wamekosa mwelekeo

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
24,478
34,526
Tatizo limeshaonekana kwenye siasa za Tanzania. Wanasiasa ambao wanaunda safu ya upinzani kwa zaidi ya nusu ni wale ambao walikataliwa na chama kilichopo madarakani kutokana na kutokukubalika kwao ama ufisadi wao...

Sehemu ndogo iliyosalia ni wale ambao wameanzia na kukulia kwenye siasa za upinzani. Lakini wanazidiwa kwa mbali sana na wanasiasa waliotupwa ama kukimbia kutoka CCM.

Miaka ya 2005 hadi 2015 siasa za upinzani zilishamiri na kufanikiwa kupata wafuasi na wanaowaunga mkono wapinzani. Sehemu kubwa ilitokana na sera ama mwelekeo wao wa kuangazia masuala ya kitaifa yale yanayoigusa jamii hususani ubunifu wa sera na mwelekeo. Upinzani ulisimama kidete kupiga vita dhidi ya ufisadi hata kufanikisha kufikisha sauti dhidi ya ufisadi vijijini. Walisimama kidete Bungeni kuhusu maadili ya viongozi, utendaji usio na tija hata namna fulani walifanikisha mawaziri kujiuzulu....

Lakini leo ninavyoandika mwelekeo ni tofauti kabisa. Kama wapinzani waliweza kwa aislimia 90% kusimamia vita ya ufisadi miaka ile kabla ya uchaguzi mkuu Oktoba 2015 basi leo wameshuka hadi asilimia 0% katika vita hiyo.

Hakuna chama cha upinzani kinachozungumzia uchumi na dira ya Taifa yenye mwelekeo wa ukuaji wa uchumi

Hakuna chama cha upinzani kinachoangaziua masuala ya Afya, mazingira wala ustawi wa jamii.

Wapinzani wapo bize leo wakichambua kauli za viongozi,

wapinzani wapo bize leo wakipandikiza chuki ndani ya nafsi za watanzania ili waichukie nchi yao

Wapinzani wapo bize leo wakichafua sera ya ulinzi wa nchi hususani kushambulia vyombo vya usalama ili nchi isitawalike

Wapinzani wapo bize leo wakisigina Demokrasia ndani ya vyama vyao.

Wapinzani wapo bize leo kuchochea na kubariki matukio ya uvunjaji wa sheria kama vile kutetea waliogushi vyeti, kutetea wauza unga, kutetea wanaotukana viongozi na taifa na kadhalika

Wakati mataifa yanayotuzunguka wakijipanga kuimarisha uchumi wa nchi zao sisi tunapambana kuharibu Taswira ya nchi ndani na nje ili kusaidia watu wenye njaa kali kushika madaraka ya nchi . watu ambao hawapo tayari kuandaa wanasiasa kizazi cha kesho, watu ambao wanaitumia siasa kujilimbikizia mali na ukwasi....

Ushauri wangu:
Mabadiliko yaanzie ndani ya vyama kabla ya kuyahubiri nje. Hauwezi kusema watu wanywe maji wakati wewe unashindia wine

Nimetoa hoja
 
Zaidi ya wapinzani kutoka ndani ya CCM unategemea watoke wapi tena wakati tangu Nyerere kulikuwa ni Chama kimoja cha CCM na kila mtanzania alikuwa ni mwanachama wa CCM iwe kwa hiari au kwa lazima,hata hao unaosema kuwa ni wazaliwa wa upinzani nao walizaliwa ndani ya CCM walichokifanya ni kuondoka CCM baada ya kujitambua.
 
Acha ukuda mleta mada, siasa mpaka 2020 halafu maccm yanaendelea kufanya siasa jinga kabisa.

Tume huru idaiwe mapema Tanzania ccm itoke vinginevyo!!!
 
Hahaha bila shaka lumumba hayo ni maoni yako binafsi na una haki ya kusema maana unao mdomo.
 
Wapinzani wapo bize leo kuchochea na kubariki matukio ya uvunjaji wa sheria kama vile kutetea waliogushi vyeti, kutetea wauza unga, kutetea wanaotukana viongozi na taifa na kadhalika
Hayo maneno ya kutetea uovu huo waliyasemea wapi wakati hata kumbi za kufanyia makongamano ya siasa wananyimwa?.
 
Acha ukuda mleta mada, siasa mpaka 2020 halafu maccm yanaendelea kufanya siasa jinga kabisa.

Tume huru idaiwe mapema Tanzania ccm itoke vinginevyo!!!
Tume huru hawana guts za kuidai kwani hata ndani ya vyama vyenu mnahitaji uhuru wa kuchagua....

Tukiongelea Demokrasia ni wazi eneo hilo upinzani umeanguka kufikia 0%
 
SUBIRI 2020 NDIYO UTAJUA KUWA UPINZANI UMEKOSA MWELEKEO AU LA
bila puchu (bao la mkono) + jecha +polisccm+tumeccm hamfurukuti.
pesa za rambi rambi imekuwa mtaji wa ccm awamu hii.
 
Umebaki upinzani wakulilia rambi rambi kwenye misiba ya watu na watu wamatukio.
 
Hakuna upinzani huku mnajambajamba. Tulizeni makalio mnawashwa na nini?
 
tapatalk_1486808132233.jpeg
 
Naomba muwe na musimamo mumoja wanainchi tuwa eleweee. leo mtakubali hili kesho mnabadilikaaa. hivi kwa nini??
Je nilini tanzania na sie tutakuwa na upinzani wenye dira??
Tusadiane wanduguuu.
 
Back
Top Bottom