Upinzani Tanzania tafuteni mwanamikakati, acheni kulia lia haitosaidia.

Pendo Julliet

JF-Expert Member
Sep 15, 2017
243
324
Mwaka 2017 unaelekea ukingoni, mengi yamejitokeza yakuskitisha na kutia hasira hayo yote yamefanywa na watawala.

Watawala wamepoka haki sana wametumia madaraka yao vibaya sana, kwetu sisi wapenda haki tumejaribu kutumia mitandao kama hivi kupaza sauti zetu.
Ndiyo tunapaza sauti zetu kukemea, kulaani na kupinga watawala hawa wanaofurahi kuona raia wakiteseka kwa umaskini unaozidi kila uchao.

Hakika imekuwa siyo rahisi sana kwa mtu kutoka hadharani na kupinga udhalimu wa hawa watu wasio na utu.
Kweli kusimama hadharani na kuwakemea hawa walevi wa madaraka inahitaji ujitoe wewe mwenyewe na usiogope mateso na hata kifo ukimaliza kuzungumza.

Tumeona hata wanasiasa wa upinzani wameogopa sana kuchukua hatua kali dhidi ya watawala, wamerudi nyuma na sasa wamebaki kulalamika na kulia lia tu kama mfungwa aliyebambikiwa kesi na mapolisi tena hukumu yake kunyongwa.

Wengi wanalalamika kwa kutumia hizi social network, nenda huko utaona hasira za wengi kuanzia raia wa kawaida hata viongozi.
Hakuna free speech tena, tulizoea kuona viongozi wa dini wakikemea watawala na wanaskilizwa lakini sasa kwa kiburi cha watawala wanatisha hadi viongozi wa kidini!

Watawala hawa wanapata wapi ujasiri huu wa kuwanyamazisha hadi viongozi wa kidini?

Inakuaje yule kardinali wa wakatoliki Pengo akisifia kwa kuwapamba wao wanafurahia na hatuoni wakimtisha kwa kuingilia siasa?

Tusiendelee kuona haya yakiendelea kutokea, yani tusilalamike tu huku mitandaoni ifike mahali tutoke hadharani kupinga watawala mapolisi hawatoeza kuua wote.

Upinzani ni kama umekubali kunyamazishwa hii ndiyo inaskitisha zaidi.
Viongozi wa upinzani walitishwa kwenye ile kampeni ya maandamano ya UKUTA wameogopa kwelikweli hawataki tena hata kuthubutu.

HAKI HAIOMBWI HUTAFUTWA, hata mwanaharakati aliwahi kuzungumza hilo namnukuu.

"Freedom is never voluntarily given by the oppressor, it must be demanded by the oppressed" - Martin L. King jr.

Hali imefikia hapa sijafika kutafuta mchawi hapa, simlaumu yeyote hapa nataka kushauri.

Ni muda wa chama cha upinzani Tanzania kama CHADEMA kutafuta wanamikakati kama wanavyofanya wengine abroad.
Huyu siyo lazima awe mwanachama chama kinatangaza nafasi za ajira na mtu anaomba na anapitia interview kama kazi nyingine tu.

Analipwa vizuri kwa kazi hiyo na lazima aende kwa mkataba wa ajira yake unavyomtaka afanye anafanya kazi hii kwa principles na ethics za chama bila kuingiliwa na extrimist wa chama.
Huyu anakuwa free wale wenye chama hawatakiwi kumuingilia sababu yeye anakuwa analindwa na mkataba na hatakiwi kuwa na conflict of interest ya kupigania uongozi wa juu kwenye chama.

Huyu ni strategist wa chama, kwenye mkwamo kama huu wa sasa Tanzania ambapo watawala wanafanya watakavyo huyu mwanamikakati ndiyo anafanya kazi kubwa ya kuongoza mikakati ya ushindi.

Huezi kuwa na watawala wanaongoza nchi watakavyo, bila kufata sheria na katiba ya nchi halafu watu wote wanaogopa kupinga, achilia mbali kuandamana hali hii ikiendela taifa letu pendwa la Tanzania linaelekea kwenye umauti.

The fight should never stop especially in hard times.

Wapigania haki wa kweli hawaogopi mateso au risasi za moto za mapolisi au kufa kwa kudai haki kwao ni heri zaidi ya kuishi kama mtumwa ndani ya nchi yako mwenyewe.

Nawatakia kila la heri.
Heri ya mwaka mpya ujao wa 2018.

[HASHTAG]#HAKI[/HASHTAG].
 
Wanamikakati ndio kina Kakobe.
20171229_141313.png
 
...HAKI HAIOMBWI HUTAFUTWA, hata mwanaharakati aliwahi kuzungumza hilo namnukuu.

"Freedom is never voluntarily given by the oppressor, it must be demanded by the oppressed" - Martin L. King jr...
Acheni kumnukuu MLK na kumhusisha na vitu vya kilofa lofa.
 
King anataka wanaoonewa wapinge kwa kuchukua hatua kama kufanya migomo na maandamano bila hivyo wataendelea kupata mateso na maumivu tu.
Yani kama Tanzania inakiwa watu waandamane tu kila jiji kubwa.
 
We hapo ulipo umeshanya nini la la maana la kuonekana na la kushikika!
Ujira wangu naopata natuma nyumbani Tanzania kusaidia ndugu, jamaa na marafiki.
Nasaidia wenye uhitaji maalumu pia.
Nawaelimisha pia kukataa umaskini wanaopitia walikate limdudu linalosababisha shida chama cha kijani wanaelewa sasa
 
Mwaka 2017 unaelekea ukingoni, mengi yamejitokeza yakuskitisha na kutia hasira hayo yote yamefanywa na watawala.

Watawala wamepoka haki sana wametumia madaraka yao vibaya sana, kwetu sisi wapenda haki tumejaribu kutumia mitandao kama hivi kupaza sauti zetu.
Ndiyo tunapaza sauti zetu kukemea, kulaani na kupinga watawala hawa wanaofurahi kuona raia wakiteseka kwa umaskini unaozidi kila uchao.

Hakika imekuwa siyo rahisi sana kwa mtu kutoka hadharani na kupinga udhalimu wa hawa watu wasio na utu.
Kweli kusimama hadharani na kuwakemea hawa walevi wa madaraka inahitaji ujitoe wewe mwenyewe na usiogope mateso na hata kifo ukimaliza kuzungumza.

Tumeona hata wanasiasa wa upinzani wameogopa sana kuchukua hatua kali dhidi ya watawala, wamerudi nyuma na sasa wamebaki kulalamika na kulia lia tu kama mfungwa aliyebambikiwa kesi na mapolisi tena hukumu yake kunyongwa.

Wengi wanalalamika kwa kutumia hizi social network, nenda huko utaona hasira za wengi kuanzia raia wa kawaida hata viongozi.
Hakuna free speech tena, tulizoea kuona viongozi wa dini wakikemea watawala na wanaskilizwa lakini sasa kwa kiburi cha watawala wanatisha hadi viongozi wa kidini!

Watawala hawa wanapata wapi ujasiri huu wa kuwanyamazisha hadi viongozi wa kidini?

Inakuaje yule kardinali wa wakatoliki Pengo akisifia kwa kuwapamba wao wanafurahia na hatuoni wakimtisha kwa kuingilia siasa?

Tusiendelee kuona haya yakiendelea kutokea, yani tusilalamike tu huku mitandaoni ifike mahali tutoke hadharani kupinga watawala mapolisi hawatoeza kuua wote.

Upinzani ni kama umekubali kunyamazishwa hii ndiyo inaskitisha zaidi.
Viongozi wa upinzani walitishwa kwenye ile kampeni ya maandamano ya UKUTA wameogopa kwelikweli hawataki tena hata kuthubutu.

HAKI HAIOMBWI HUTAFUTWA, hata mwanaharakati aliwahi kuzungumza hilo namnukuu.

"Freedom is never voluntarily given by the oppressor, it must be demanded by the oppressed" - Martin L. King jr.

Hali imefikia hapa sijafika kutafuta mchawi hapa, simlaumu yeyote hapa nataka kushauri.

Ni muda wa chama cha upinzani Tanzania kama CHADEMA kutafuta wanamikakati kama wanavyofanya wengine abroad.
Huyu siyo lazima awe mwanachama chama kinatangaza nafasi za ajira na mtu anaomba na anapitia interview kama kazi nyingine tu.

Analipwa vizuri kwa kazi hiyo na lazima aende kwa mkataba wa ajira yake unavyomtaka afanye anafanya kazi hii kwa principles na ethics za chama bila kuingiliwa na extrimist wa chama.
Huyu anakuwa free wale wenye chama hawatakiwi kumuingilia sababu yeye anakuwa analindwa na mkataba na hatakiwi kuwa na conflict of interest ya kupigania uongozi wa juu kwenye chama.

Huyu ni strategist wa chama, kwenye mkwamo kama huu wa sasa Tanzania ambapo watawala wanafanya watakavyo huyu mwanamikakati ndiyo anafanya kazi kubwa ya kuongoza mikakati ya ushindi.

Huezi kuwa na watawala wanaongoza nchi watakavyo, bila kufata sheria na katiba ya nchi halafu watu wote wanaogopa kupinga, achilia mbali kuandamana hali hii ikiendela taifa letu pendwa la Tanzania linaelekea kwenye umauti.

The fight should never stop especially in hard times.

Wapigania haki wa kweli hawaogopi mateso au risasi za moto za mapolisi au kufa kwa kudai haki kwao ni heri zaidi ya kuishi kama mtumwa ndani ya nchi yako mwenyewe.

Nawatakia kila la heri.
Heri ya mwaka mpya ujao wa 2018.

[HASHTAG]#HAKI[/HASHTAG].
umejitahidi kuandika we ni kati ya wadada wanaojitambua
 
Kwani Mbowe unayemsema amechangiaje umaskini wa watanzania?

Dada umeandika mambo mazuri sana pale juu. Tunakuomba uje ww kwa muda hapa nchini uliendeshe wazo lako tuone ufanisi wake. Kuna wenzako wengi tu wanasema wapinzani wabadili mbinu, ukiwaambia wataje hizo mbinu wanapotelea hapo katikati. Ww wangalau umetaja mbinu, sasa ili tusikosee mbinu yako hebu njoo utuelekeze kwa vitendo. Tunakungoja.

Mimi mbinu yangu iko wazi nayo ni ya machafuko ila itakuwa na madhara kwa taifa letu. Hata kama tukishindwa kwenye hii lakini tutaheshimiana.
 
Mwaka 2017 unaelekea ukingoni, mengi yamejitokeza yakuskitisha na kutia hasira hayo yote yamefanywa na watawala.

Watawala wamepoka haki sana wametumia madaraka yao vibaya sana, kwetu sisi wapenda haki tumejaribu kutumia mitandao kama hivi kupaza sauti zetu.
Ndiyo tunapaza sauti zetu kukemea, kulaani na kupinga watawala hawa wanaofurahi kuona raia wakiteseka kwa umaskini unaozidi kila uchao.

Hakika imekuwa siyo rahisi sana kwa mtu kutoka hadharani na kupinga udhalimu wa hawa watu wasio na utu.
Kweli kusimama hadharani na kuwakemea hawa walevi wa madaraka inahitaji ujitoe wewe mwenyewe na usiogope mateso na hata kifo ukimaliza kuzungumza.

Tumeona hata wanasiasa wa upinzani wameogopa sana kuchukua hatua kali dhidi ya watawala, wamerudi nyuma na sasa wamebaki kulalamika na kulia lia tu kama mfungwa aliyebambikiwa kesi na mapolisi tena hukumu yake kunyongwa.

Wengi wanalalamika kwa kutumia hizi social network, nenda huko utaona hasira za wengi kuanzia raia wa kawaida hata viongozi.
Hakuna free speech tena, tulizoea kuona viongozi wa dini wakikemea watawala na wanaskilizwa lakini sasa kwa kiburi cha watawala wanatisha hadi viongozi wa kidini!

Watawala hawa wanapata wapi ujasiri huu wa kuwanyamazisha hadi viongozi wa kidini?

Inakuaje yule kardinali wa wakatoliki Pengo akisifia kwa kuwapamba wao wanafurahia na hatuoni wakimtisha kwa kuingilia siasa?

Tusiendelee kuona haya yakiendelea kutokea, yani tusilalamike tu huku mitandaoni ifike mahali tutoke hadharani kupinga watawala mapolisi hawatoeza kuua wote.

Upinzani ni kama umekubali kunyamazishwa hii ndiyo inaskitisha zaidi.
Viongozi wa upinzani walitishwa kwenye ile kampeni ya maandamano ya UKUTA wameogopa kwelikweli hawataki tena hata kuthubutu.

HAKI HAIOMBWI HUTAFUTWA, hata mwanaharakati aliwahi kuzungumza hilo namnukuu.

"Freedom is never voluntarily given by the oppressor, it must be demanded by the oppressed" - Martin L. King jr.

Hali imefikia hapa sijafika kutafuta mchawi hapa, simlaumu yeyote hapa nataka kushauri.

Ni muda wa chama cha upinzani Tanzania kama CHADEMA kutafuta wanamikakati kama wanavyofanya wengine abroad.
Huyu siyo lazima awe mwanachama chama kinatangaza nafasi za ajira na mtu anaomba na anapitia interview kama kazi nyingine tu.

Analipwa vizuri kwa kazi hiyo na lazima aende kwa mkataba wa ajira yake unavyomtaka afanye anafanya kazi hii kwa principles na ethics za chama bila kuingiliwa na extrimist wa chama.
Huyu anakuwa free wale wenye chama hawatakiwi kumuingilia sababu yeye anakuwa analindwa na mkataba na hatakiwi kuwa na conflict of interest ya kupigania uongozi wa juu kwenye chama.

Huyu ni strategist wa chama, kwenye mkwamo kama huu wa sasa Tanzania ambapo watawala wanafanya watakavyo huyu mwanamikakati ndiyo anafanya kazi kubwa ya kuongoza mikakati ya ushindi.

Huezi kuwa na watawala wanaongoza nchi watakavyo, bila kufata sheria na katiba ya nchi halafu watu wote wanaogopa kupinga, achilia mbali kuandamana hali hii ikiendela taifa letu pendwa la Tanzania linaelekea kwenye umauti.

The fight should never stop especially in hard times.

Wapigania haki wa kweli hawaogopi mateso au risasi za moto za mapolisi au kufa kwa kudai haki kwao ni heri zaidi ya kuishi kama mtumwa ndani ya nchi yako mwenyewe.

Nawatakia kila la heri.
Heri ya mwaka mpya ujao wa 2018.

[HASHTAG]#HAKI[/HASHTAG].
mwanzo nilitaka kukupinga Ila mwishoni nimekuelewa una point.

kweli kuna watu so wazuri jukwaani Ila in wana mikakati wazuri.
 
Back
Top Bottom