Upinzani Tanzania kusumbuliwa haya mambo yananiudhi na kunikera sana

Haki na maendeleo

Senior Member
Jun 15, 2021
123
262
Habari wakuu, mimi ni Mtanzania! Lakini haya mambo yananikera sana yanayofanywa na viongozi wetu wanaojiita wazalendo,

1: Kumuona mtanzania mwenzangu anakamatwa bila sababu ya msingi kisa tu ni upinzani, huwa nakosa amani, mm nimeokoka na nimuombaji sana, lakini ninapoona haki ya mtu inaporwa huwa naumia sana kwenye moyo wangu, ni upumbavu wa hali ya juu, CCM kila siku wanafanya mikutano ya hadhara na ya ndani lakini upinzani wakitaka kufanya wanaita ni kuivuruga amani. Hiyo mbele za Mungu ni kufuru na Mungu hadhihakiwi!! Amani gani hiyo wanavuruga?

Watanzania serikali isitufanye kuwa ni wajinga!! Na kwa kuwa sisi hasa waombaji huwa tunamwachia Mungu na Mungu alishawaonyesha kuwa yeye ni Mungu bado watu hawajiulizi tu?

Wewe fikiria , unaweka wabunge wako unaowataka, unapora haki ya wananchi, watu wanakufananisha wewe na Mungu, huwezi kukemea, watu wanabambikiziwa kesi za kijinga na wewe ni raisi hata kukemea hamna, unanunua wapinzani huku unapiga marufuku siasa wakati huo chama chako siasa, yaani wewe mtu mmoja ndo mwamuzi wa kila kitu alafu bila aibu unainua bibilia takatifu na katiba ambayo hukuifuata miaka mitano mbele za Mungu kuapa kuwa akusaidie!! Ni mambo ya ajabu, Mungu hadhihakiwi rejea kwa Herode, nakuhakikishia huwezi baki salama, Mungu hashirikishwi kwenye mambo ya kijinga, Kila alitajaye jina La Bwana na auache uovu (Mwendazake).

Bado tu viongozi wetu hawajifunzi!!, sisi wananchi tunataka katiba, wale akina mbowe hawako peke yao sisi wananchi na wanamaombi tupo nyuma yao, kinachofanyika kwao ni uonevu wa hali ya juu!!,

Mimi kama mwananchi na mwanamaombi, mbowe asipoachiwa na viongozi wa chadema!! Maombi yale tulioyoomba mwaka jana na yakafanya kazi!

Tutaanza na sasa hivh kuomba tena, na kipindi hiki tunaanza na wabunge wote haramu ambao hawakuchaguliwa na wananchi na wanakula hela zetu bila hata kulipa kodi.

Tunamtaka Mbowe#####
 
Back
Top Bottom