Upinzani Tanzania hauna ubunifu wa kutosha...!


K

Kamundu

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2006
Messages
2,449
Points
2,000
K

Kamundu

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2006
2,449 2,000
Napenda sana wapinzania Tanzania kwani wanaongeza uwazi na ufanisi wa serikali sana. Upinzani vilevile wanajitahiji sana kuelimisha watanzania kwenye wakati mgumu sana. Lakini upinzani Tanzania wana kasoro moja kubwa wanafikiria matatizo ya Tanzania yanatokana na siasa pekee ukweli ni kwamba Tanzania ina tatizo kubwa ya mbinu nzuri za kufanya kazi nitatoa mfano mmoja leo kalini nitatoa mingine muda unavyoenda

Elimu:
Je wapinzani ni lini wametoa sera za kubadilisha mfumo wa elimu zaidi ya kusema mishahara ya walimu iongezwe. Je ni kwanini wapinzani wasingekuja na sera mfano wanavyuo kabla ya kupewa vyeti vyao wakafundishe miezi sita ua mwaka. Tunajua kabisa mikopo iliyotolewa kwa wanavyuo haitarudi sasa ni kwanini kusiwe na sera za kibunifu kama za kuwatumia wana vyuo. Mfano mwingine Je ni kwanini shule ambazo zinafelisha wanafunzi karibu wote bado ziko wazi wakati watanzania wanalipa ada za shule! upinzani uko wapi kwenye hili?. Tanzania ni kubwa sana haitaweza kuwa na walimu wa sekondari kila mahali je kuna sera gani ambazo upinzani wanazo za kuelimisha watoto wa sekondari Tanzania sio pesa tu bali ubunifu kama boarding schools, kukuza shule ambazo zipo na zina nafasi. sijawahi kuona sera hapa ya upinzania. Tatizo sio pesa tu bali mbinu bora za maendeleo

Mfumo wa serikali:
Nimesoma sana kwamba upinzani wanataka serikali iwe ndogo na mawaziri wawe wachache. Lakini udogo wa mawaziri pekee hautasaidia kupunguza gharama. Kama upinzani unataka kupunguza gharama kikweli ni kupunguza matumizi ya serikali kwa kupunguza shughuli ambazo serikali inafanya. Serikali inamatumizi makubwa si kwasababu mawaziri ni wengi bali ni kwasababu serikali haina mpaka kwenye katiba ambao unaeleza kinagaubaga shughuli za serikali . Serikali ya Tanzania inalipa walimu wote na kujenga shule, madaktari na kujenga hospitali, polisi, jeshi, wafanyakazi wengi wa serikali, wabunge wote, biashara ya mashamba, biashara ya ndege, treni, ujenzi wa barabara, maji, umeme hauwezi kuwa na shughuli zote hizi na kuwa na ufanisi kwa nchi kama Tanzania.

Upinzani badala ya kulalamikia ufanisi wanatakiwa kushauri jinsi gani mfumo wa serikali ubadilike mfano Katiba ya USA inasema serikali inatakiwa kushughulikia vitu tu ambavyo watu hawawezi kufanya wenyewe ulinzi, kuchapisha pesa, kutunga sheria,na vitu muhimu kama maji, viwango vya elimu, afya, na security ya chakula. Sasa Tanzania kwasababu hakuna sheria kila serikali ikija na miradi inaongeza gharama za serikali na kupunguza fungu kwenye shughuli muhimu. Pesa yakulipa madeni ya ATC ndiyo hiyo ingeweza kulipa pesa za walimu. Je Watanzania wanataka mfumo gani wa siasa kama wa China, USA, Brazil au tuna mfumo wetu wenyewe ambao hatujui unapokwenda!! upinzani unatakiwa kufafanua mambo kama haya kwa watu badala ya kufuata mfumo wa sasa ambao haueleweki tunaenda wapi. Bila kubadilisha mfumo hakuna serikali ambayo inaweza kufanya vizuri kwenye mfumo huu kwani rushwa pekee sio Tatizo.

Kodi:
Je Watanzania tunalipishwa asilimia zaidi ya 50% kwenye magari je ni lini tumepewa faida ya kodi hizi? je kodi ingepunguzwa mpaka 10% ingesaida zaidi kwenye kodi za magari kuongezeka, mafuta, spare, matairi, mafundi n.k upinzania hauna sera ya kueleweka kwenye kodi na hawafanyi research na imebakiwa wananchi kulalamikia kodi pekee huku upinzania ukinyamaza tu. Tanzania inamagari yasio zidi milioni 2 kwenye nchi kubwa ambayo ni zaidi ya state of Texas.

Sasa kuna mpinzani kafanya research na kutuambia vizuri future ya usafiri Tanzania na kodi ya 50% ni kweli inasaidia uchumi au!!!? Upinzani unatakiwa kufukiria tofauti lakini mpaka sasa nnimeona ni maswala ya rushwa, mikataba na majimbo pekee ndiyo vinaongelewa!!
 
K

Kamundu

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2006
Messages
2,449
Points
2,000
K

Kamundu

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2006
2,449 2,000
Ni wakati wa kuongelea maendeleo ya kweli
 

Forum statistics

Threads 1,294,412
Members 497,915
Posts 31,175,122
Top