Upinzani sasa ushirikiane na Serikali iliyopo madarakani

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,321
4,671
Umefika wakati wa vyama vya upinzani kushirikiana na serikali iliyopo madarakani ili tupate Tanzania tunayoitaka.

kwa Serikali ya sasa yale Magumu yote yanasawazishwa ndio maana hata upinzani hawana cha kusemea tena kama ni masuala ya Rushwa,Madawa ya kulevya,uwajibakaji kazini yote yanafanyika kwa Asilimia kubwa sana.

Ninaimani hata suala la Ajira ni Muda tu na Muda ukifika Ajira zitatoka na kila mtu atacheka,

Ili kuijenga Tanzania mpya ni vyema Vyama vya upinzani kushirikiana na Serikali bega kwa bega ili kusukuma gurudumu la maendeleo mbele zaidi na pale penye shida wakae meza ya mazungumzo na kutatua changamoto hizo na hata wakiona mambo hayaendi sawia watoe ushauri wa kujenga kwa manufaa ya Nchi yetu.

Asanteni
 
wazungu wanasema too much democracy is undemocracy inafika mahali inabd ubadili aina ya utawala ila malengo yakifiwe.

hiyo democracy ndo imesababisha mpaka leo tupo hapa huku wenzetu wakizid kuchanja mbuga
 
Hii ni ajabu ilioje...unaonaje kama badala ya kuutaka upinzani ushirikiane na serikali, ungeitaka serikali ndiyo ishirikiane na upinzani? Kwa kuanzia, nadhani ingefaa kama upinzani ungekuwa huru kutimiza wajibu wake kulingana na matakwa ya Katiba. Aliyefungwa mdomo atawezaje kutoa ushirikiano hata kama angependa? Upinzani utashirikiana vipi na serikali isiyoheshimu Katiba? Hii ni kama kumtaka raia mwema ashirikiane na mhalifu kwa kuwa tu mhalifu ana nguvu kumzidi. Waliompa Hitler ushirikiano hadi leo, miaka zaidi ya 80 baadaye, bado wanawindwa wakamatwe na kushtakiwa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kuna tatizo la kutoza kodi kwa hata wasioweza kupata hiyo kodi, Je la kusanyo kutumiwa vibaya kama kununua ndege isiyo hitaji kwa 80% wakulima wa Tanzania? Je kilimo kutokuwa kipaumbele huku kikiajili 80% ya Wa Tanzania? Elimu bure kutokuwa bure! Demokrasia iko wapi? Katiba kuwa mbovu na bado ikavunjwa? Nk
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Sijui upeo wako wa kuelewa ni wa kiwango gani. Wataweza je kushirikiana ktk mazingira yaliyoko? Huwa unaiangalia bunge wakati yule mumama sijui dakitari wa sindano sijui wa nini anapokuwa kwenye kiti cha enzi?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Sioni kipengele cha katiba kilichovunjwa na kama katiba ikivunjwa unahaki ya kutafuta haki sehemu yoyote ile iwe kwenye mahakama za ndani au za nje ila sijaona wapinzani wakifungua kesi yoyote ile kuhusu katiba kuvunjwa.

Kuhusu mikutano ya kisiasa sina shaka juu ya hilo tunatengeneza nchi kwanza mfano pale Usa hivi baada ya uchaguzi umesikia vyama vya upinzani vikiendelea na mikutano zaidi ya raia kuandamana?
 
Sijui upeo wako wa kuelewa ni wa kiwango gani. Wataweza je kushirikiana ktk mazingira yaliyoko? Huwa unaiangalia bunge wakati yule mumama sijui dakitari wa sindano sijui wa nini anapokuwa kwenye kiti cha enzi?
Huenda Katiba inavunjwa kwa kuwa ni mbovu
 
wazungu wanasema too much democracy is undemocracy inafika mahali inabd ubadili aina ya utawala ila malengo yakifiwe.
Mpaka sasa tuna miaka zaidi ya hamsini toka tupate uhuru, je ni lini aina ya utawala imebadilishwa hapa Tanzania?

hiyo democracy ndo imesababisha mpaka leo tupo hapa huku wenzetu wakizid kuchanja mbuga
Watu wale wale, mfumo ule ule, chama kile kile...kitu gani kimebadilika?
Sioni kipengele cha katiba kilichovunjwa na kama katiba ikivunjwa unahaki ya kutafuta haki sehemu yoyote ile iwe kwenye mahakama za ndani au za nje ila sijaona wapinzani wakifungua kesi yoyote ile kuhusu katiba kuvunjwa.
Pole...unayo macho lakini huoni, unayo masikio lakini husikii...hilo ndilo tatizo linalowakabili Watanzania wengi kama wewe.
Kuhusu mikutano ya kisiasa sina shaka juu ya hilo tunatengeneza nchi kwanza mfano pale Usa hivi baada ya uchaguzi umesikia vyama vya upinzani vikiendelea na mikutano zaidi ya raia kuandamana?
Unaishi kwenye dunia ya peke yako, siyo hii tunayoishi sisi. Huko USA tayari Rais kafungwa luku kwa ulevi wa madaraka na kutoheshimu Katiba. Kwa hiyo vyama vya siasa si wananchi...this is idiocy at its best.
 
Umefika wakati wa vyama vya upinzani kushirikiana na serikali iliyopo madarakani ili tupate Tanzania tunayoitaka.

kwa Serikali ya sasa yale Magumu yote yanasawazishwa ndio maana hata upinzani hawana cha kusemea tena kama ni masuala ya Rushwa,Madawa ya kulevya,uwajibakaji kazini yote yanafanyika kwa Asilimia kubwa sana.

Ninaimani hata suala la Ajira ni Muda tu na Muda ukifika Ajira zitatoka na kila mtu atacheka,

Ili kuijenga Tanzania mpya ni vyema Vyama vya upinzani kushirikiana na Serikali bega kwa bega ili kusukuma gurudumu la maendeleo mbele zaidi na pale penye shida wakae meza ya mazungumzo na kutatua changamoto hizo na hata wakiona mambo hayaendi sawia watoe ushauri wa kujenga kwa manufaa ya Nchi yetu.

Asanteni
Unashirikianaje na mtu anayekuchukia
 
Ufahamu wako uko sawa kweli? Unazijua mahakama zetu? Kamuulize Lema pale kisongo nini kimejiri
 
Sioni kipengele cha katiba kilichovunjwa na kama katiba ikivunjwa unahaki ya kutafuta haki sehemu yoyote ile iwe kwenye mahakama za ndani au za nje ila sijaona wapinzani wakifungua kesi yoyote ile kuhusu katiba kuvunjwa.

Kuhusu mikutano ya kisiasa sina shaka juu ya hilo tunatengeneza nchi kwanza mfano pale Usa hivi baada ya uchaguzi umesikia vyama vya upinzani vikiendelea na mikutano zaidi ya raia kuandamana?
Huko kwa wakubwa wao baada ya kuingia kupiga Kura na Trump kutangazwa harakati za democrats ziliishia pale. Wao wanataka harakati kuanzia January to December
 
Umefika wakati wa vyama vya upinzani kushirikiana na serikali iliyopo madarakani ili tupate Tanzania tunayoitaka.

kwa Serikali ya sasa yale Magumu yote yanasawazishwa ndio maana hata upinzani hawana cha kusemea tena kama ni masuala ya Rushwa,Madawa ya kulevya,uwajibakaji kazini yote yanafanyika kwa Asilimia kubwa sana.

Ninaimani hata suala la Ajira ni Muda tu na Muda ukifika Ajira zitatoka na kila mtu atacheka,

Ili kuijenga Tanzania mpya ni vyema Vyama vya upinzani kushirikiana na Serikali bega kwa bega ili kusukuma gurudumu la maendeleo mbele zaidi na pale penye shida wakae meza ya mazungumzo na kutatua changamoto hizo na hata wakiona mambo hayaendi sawia watoe ushauri wa kujenga kwa manufaa ya Nchi yetu.

Asanteni
Hata hayo maovu ya Serikali ya awamu ya tano.unayasemea.wapi??Wakiongea kwenye Bunge wananyamazishwa na NS alipikwa na Serikali,wakisema.kwenye TV,Redio au Magazeti yanafungiwa.Mikutano ya siasa imefungiwa wenye haki ni CCM tu.Unataka wasimamie wapi??
 
wazungu wanasema too much democracy is undemocracy inafika mahali inabd ubadili aina ya utawala ila malengo yakifiwe.

hiyo democracy ndo imesababisha mpaka leo tupo hapa huku wenzetu wakizid kuchanja mbuga
Matokeo ya mtihani wa taifa kidato cha nne madhara yake ni ya siku nyingi imewadhulu Lumumba
 
Hata hayo maovu ya Serikali ya awamu ya tano.unayasemea.wapi??Wakiongea kwenye Bunge wananyamazishwa na NS alipikwa na Serikali,wakisema.kwenye TV,Redio au Magazeti yanafungiwa.Mikutano ya siasa imefungiwa wenye haki ni CCM tu.Unataka wasimamie wapi??
Nani kaongea pointi kwenye Bunge akakalishwa chini?na vp yule Mbunge wa Mbeya aliyeonyesha middle finger kweli utamwacha mtu kama yule makosa mengine wapinzan wanafanya ila wakiadhibiwa wanaona kama wameonewa
 
Ufahamu wako uko sawa kweli? Unazijua mahakama zetu? Kamuulize Lema pale kisongo nini kimejiri
ninachoamimi haki inachelewa tuu ila kama kweli hana hatia atatoka tuu na kuendelea na kazi zake.
 
Umefika wakati wa vyama vya upinzani kushirikiana na serikali iliyopo madarakani ili tupate Tanzania tunayoitaka.

kwa Serikali ya sasa yale Magumu yote yanasawazishwa ndio maana hata upinzani hawana cha kusemea tena kama ni masuala ya Rushwa,Madawa ya kulevya,uwajibakaji kazini yote yanafanyika kwa Asilimia kubwa sana.

Ninaimani hata suala la Ajira ni Muda tu na Muda ukifika Ajira zitatoka na kila mtu atacheka,

Ili kuijenga Tanzania mpya ni vyema Vyama vya upinzani kushirikiana na Serikali bega kwa bega ili kusukuma gurudumu la maendeleo mbele zaidi na pale penye shida wakae meza ya mazungumzo na kutatua changamoto hizo na hata wakiona mambo hayaendi sawia watoe ushauri wa kujenga kwa manufaa ya Nchi yetu.

Asanteni
wapinzani kuipinga serekali ili itekeleze wajibu wake kwa ufanisi zaidi ni ushirikiano tosha pia.
 
Back
Top Bottom