EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,308
Nimeyapenda mawazo haya:
Vyombo vya dola, polisi, usalama wa taifa, mahakama havitekelezi majukumu yake kama vyombo vya taifa badala yake vinafanya kazi kama matawi ya CCM. Lengo ni kuibeba/kuibakisha CCM madarakani.
Viongozi wa Upinzania ni lazima sasa kupambana na haya:
1. kupigania kuwepo kwa tume ya uchaguzi iliyo huru.
2.Kuhakikisha na kupiga kelele za kutosha kwa vyombo vya dola ili vianze kufanya kazi
kama vyombo vya nchi na sio kama vyombo vya chama.CCM
3.Kususia Changuzi zote kama mapendekezo hapo juu hayatafanyiwa kazi.
Baada ya kufanya vibaya kwenye changuzi za udiwani ndiyo mmeshtuka.
Hivi Ikulu pia ni chombo cha dola? Siku hizi CCM huwa wanafanyia vikao vyao pale. Mbona Chadema hamjawhi kusema lolote kuhusiana na hili?
Tovuti ya Ikulu nayo siyo chombo cha dola? Mbona imetapakaa picha za chaguzi za CCM lakini Chadema hamsemi chochote?
Mpaka Ikulu inatumiwa kama chombo cha CCM lakini nyie Chadema mko kimya tuu. Labda na nyie mkiingia Ikulu mtakuwa mnafanya hivyo.
napata shida sana na watu kama wewe,
Hivi unajua mtu kujiidentify to kama mwanachadema inamgharimu sana?unaweza ukawajua wagombea waambie sasa wajiweke hadharani?
naomba tunapoongelea kitu tupime pande zote,wagombea wapo ndoyo mnawajua,waambieni wajitokeze waanze kupimwa na wananchi?
Kumbuka wagombea wengi kama si mfanya bihashara ni mfanyakazi,sasa ajitambulishe leo maCCM watamuokoa,tusiwafananishe na wagombea wa CCM,waowanalinda sana.
Naomba tu endelea kuwatia moyo na kuwajengea ujasiri hiyo ndiyo kazi kubwa inayotakiwa.
unapokuja kwenye swala la hela,mungu wangu ivi umeshataka kujua gharama ya operation kwenye mkoa mmoja tu inagharimu shillingi ngapi?ukijua hili utajiuliza je Chadema wanarasilimali gani zinazowaingizia kipato?
halafu ndipo utafute kujua kila kata walipewa nini.
Ukishaona hivyo, jua watu hawako tayari kwa mabadiliko. Mtu ambaye yuko tayari kwa mabadiliko atakuwa tayari kwa lolote lile.
Suala la gharama ni la kujitakia tuu. Ziko njia bora na cheaper zaidi za kufikisha ujembe kwa wananchi badala ya hii mikutano ya hadhara ambayo so far mmekuwa mkifanya tokea miaka 1990s bila mafanikio.