Upinzani sasa Tufanye nini?

Josephine

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
786
812
Nimeyapenda mawazo haya:

Vyombo vya dola, polisi, usalama wa taifa, mahakama havitekelezi majukumu yake kama vyombo vya taifa badala yake vinafanya kazi kama matawi ya CCM. Lengo ni kuibeba/kuibakisha CCM madarakani.

Viongozi wa Upinzania ni lazima sasa kupambana na haya:

1. kupigania kuwepo kwa tume ya uchaguzi iliyo huru.

2.Kuhakikisha na kupiga kelele za kutosha kwa vyombo vya dola ili vianze kufanya kazi
kama vyombo vya nchi na sio kama vyombo vya chama.CCM

3.Kususia Changuzi zote kama mapendekezo hapo juu hayatafanyiwa kazi.
 
Josephine haya yalipaswa yawe malengo ya muda mrefu tena ya haraka sana

Vijana waliotiimiza miaka kumi na nane toka mwaka 2010 hawajaingizwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na hii ni kwa kuwa Tume imekaa kimya kwa faida ya wachache na chama tawala.

Ilipaswa kuwe na uraratibu ambao unaeleweka kwa kila mwaka daftari hilo kufanyiwa mabadiliko kuondoa wale waliopoteza maisha na kuwaweka wale wapya ambao wametimiza umri halisi

Hilo halifanyiki na Tumeya Taifa ya Uchaguzi wanaendeela kula posho na mishahara wakati hatuoni kazi wanayoifanya na wamekaa pale kwa sababu wanalinda maslahi ya waliowatuma.

Kikweli hatuna vyombo huru vya usalama ambavyo viko kwa ajili ya maslahi ya wananchi au hata vyama vya upinzani. Viko pale kulinda maslahi ya watawala na kupewa masharti ya nini cha kufanya

Tuanze sasa kudai kuwa na tume huru ya uchaguzi ambayo haitateuliw ana kiongozi aliye madarakani na ambayo itakuwa huru kufanya kazi zake bila kuhakikisha kuwa inafuata kile mwenye filimbi anachoamua. Kuendelea kuwa na hii tume ambayo sio huru na haionyeshi kuwa huru au kufanya kazi kwa matakwa ya wananchi na wapenda demokrasia ni pigo kubwa sana na hatutegemei kwa njia yoyote kupata uchaguzi huru na wa haki
 
Hilo la tatu la kususia siliungi mkono kabisa, ni sawa na kumpa Nguruwe alinde shamba la mihogo.
 
Tangu kuasisiwa kwa siasa ya vyama vingi 1992 sijui nini kinachowashawishi wapinzani kukimbilia kwenye uchaguzi wakati wanajua kabisa wanacheza kwa kutumia sheria ambazo sio fair?

1. Awali ya yote njoo kwenye katiba, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi akishatangaza matokeo ya urais hakuna awezaye kuyapinga hata mahakama
2. Tume ya uchaguzi inateuliwa na rais ambaye kwa sasa ndio mwenyekiti wa ccm na pia sometime ndio anapeperusha bendera ya chama hicho! unatarajia tume hiyohiyo imatangaze kashindwa wakati kikatiba ipo juu ya mahakama??
3. CCM wanatumia rasilimali za umma kama magari, ofisi za wakuu wa mikoa,wilaya na watendaji wa kata kufanya kazi za chama, na hata mawaziri wanafanya kazi za chama wakati ni watumishi wa umma!
4. CCM wamehodhi viwanja kama kirumba, sheikh amri abedi, jamhuri moro/dom na vingine vingi ambavo vilijengwa wakati wa chama kimoja kwa kodi za watanzania wote sasa wapinzani hawaruhusiwi kufanyia kampeni humo
5. Daftari la wapiga kura huwa halifanyiwi marekebisho kwa wakati muafaka, kuingiza wapiga kura wapya au kuondoa waliokosa sifa mfano kufa, kupoteza uraia n.k

Hayo ni machache tu ambayo wapinzani wanayajua fika kuliko mimi na wewe lakini ukifika uchaguzi uwe mkuu au mdogo wanakimbilia tu bila kuyatatua wakishashindwa utasikia yakitajwa uchaguzi ukija wakiona mikusnyiko mingi ya watu wanapata taama ya uchaguzi
Maoni yangu hayo mambo ,matano niliyogusia na mengine kama hayo yasipopatiwa ufumbuzi uchaguzi utakuwa hivi kata 29 wapinzani wanapata 7 tu; Majimbo zaidi ya 300 wapinzani hayafiki sabini, mwendo ndio huo wapinzani lazima wabadilike, pia utitiri huu wa vyama ndio ni demokrasia lakini ukizidi unaua demokrasia kwa kugawa kura!
 
Hakuna sababu ya kususia ila ni kupamabana na hawa madhalimu na udhalimu mpaka haki
ya kweli ya watanzania ipatikane.
 
Vijana ambao wametimiza miaka 18 tokea uchaguzi wa 2010 ni wengi mno sasa hichi chama kichakavu hakitaki hao kwasababu sio mtaji wao
 
nakubaliana nawewe,sasa tuingie kazini.

Iam afraid tuingie kazini lakini we may be too late for 2015, ccm sio warahisi kama tunavowaza wengi, wana mbinu za kila aina chafu na safi na wanaziboresha kwa wakati na nyakati tofauti wapinzani lazima wa think very deep kuing'oa ccm.! lazima mbinu za kisayansi sana, zitumike jiulize kwenye mikutano ya kampeni ya udiwani juzi watu walijaa sana lakini matokea kati ya kata 29 wapinzani wamepata 7 tu why??
 
Kabla ya kuwanyooshea vidole wengine jambo la kwanza kabisa ni Chadema kuandaa wagombea bora kwa kila jimbo na kata, mfano kata ninayoishi mimi mpaka leo sijaona mtu wa kuaminiwa kusimama kwenye udiwani mwaka 2015, sasa wakati ni huu.

Nawafahamu vyema Watanzania na akili zao. mwonekano tu wa mtu ni sehemu ya kuaminiwa au kama umewahi kushiriki shughuri za umma au kamati mbalimbali za maendeleo mtaani au katani. tuwe wakweli jamani kuna wagombea hawachaguliki.

Hakuna kitu kilichonisikitisha kwenye uchaguzi mkuu wa 2010 na mgombea Urais wa Chadema kuwa na posters chache mno na Chadema kuwadanganya watu kwamba eti vifaa vya kampeni vimekwama bandarini, uhuni huu haukubaliki na ujinga usijirudie tena, hakuna kampeni zisizokuwa na vifaa vya kampeni kwa ajili ya hamasa.

Labda ningeomba kuuliza tu kwenye hizi Chaguzi ndogo Chadema ilitowa kiasi cha pesa kwa kata zote kuwezesha kampeni na hamasa? naomba jibu sahihi kwenye hili.
 
kususia si ndio tutakuwa tumewapa advantage?

Hapana,maisha ni hatua kwa hatua.baada ya wananchi kujionea vurugu kwa macho yao ,rahisi sasa kuwashawishi wasiende kwenye uchaguzi mpaka mabadiliko yawepo.

Ni lazima hatua hiyo ifikiwe vinginevyo bado wataendelea kufanya waliofanya,ipo njia nyingine ambayo kama pande zote mbili ikiamua kutumia silaa za mapambano ,basi nchi itaingia kwenye machafuko.
 
Vijana ambao wametimiza miaka 18 tokea uchaguzi wa 2010 ni wengi mno sasa hichi chama kichakavu hakitaki hao kwasababu sio mtaji wao

hakiwezi kikataka lazima kilamishwe kwa nguvu ya umma na hoja mfano wapinzani walitakiwa walishanya utafiti kujua tangu kuboreshwa daftari 2010 hadi sasa wapiga kura wangapi wameongezeka wangapi wamekufa then hizo data zitumike kujenga hoja kuwa daftari liboreshwe, lakini kulalamika bila data is mere nonsense
 
Kabla ya kuwanyooshea vidole wengine jambo la kwanza kabisa ni Chadema kuandaa wagombea bora kwa kila jimbo na kata, mfano kata ninayoishi mimi mpaka leo sijaona mtu wa kuaminiwa kusimama kwenye udiwani mwaka 2015, sasa wakati ni huu.

Nawafahamu vyema Watanzania na akili zao. mwonekano tu wa mtu ni sehemu ya kuaminiwa au kama umewahi kushiriki shughuri za umma au kamati mbalimbali za maendeleo mtaani au katani. tuwe wakweli jamani kuna wagombea hawachaguliki.

Hakuna kitu kilichonisikitisha kwenye uchaguzi mkuu wa 2010 na mgombea Urais wa Chadema kuwa na posters chache mno na Chadema kuwadanganya watu kwamba eti vifaa vya kampeni vimekwama bandarini, uhuni huu haukubaliki na ujinga usijirudie tena, hakuna kampeni zisizokuwa na vifaa vya kampeni kwa ajili ya hamasa.

Labda ningeomba kuuliza tu kwenye hizi Chaguzi ndogo Chadema ilitowa kiasi cha pesa kwa kata zote kuwezesha kampeni na hamasa? naomba jibu sahihi kwenye hili.


napata shida sana na watu kama wewe,

Hivi unajua mtu kujiidentify to kama mwanachadema inamgharimu sana?unaweza ukawajua wagombea waambie sasa wajiweke hadharani?

naomba tunapoongelea kitu tupime pande zote,wagombea wapo ndoyo mnawajua,waambieni wajitokeze waanze kupimwa na wananchi?
Kumbuka wagombea wengi kama si mfanya bihashara ni mfanyakazi,sasa ajitambulishe leo maCCM watamuokoa,tusiwafananishe na wagombea wa CCM,waowanalinda sana.

Naomba tu endelea kuwatia moyo na kuwajengea ujasiri hiyo ndiyo kazi kubwa inayotakiwa.

unapokuja kwenye swala la hela,mungu wangu ivi umeshataka kujua gharama ya operation kwenye mkoa mmoja tu inagharimu shillingi ngapi?ukijua hili utajiuliza je Chadema wanarasilimali gani zinazowaingizia kipato?
halafu ndipo utafute kujua kila kata walipewa nini.
 
Labda tu hii ni clear message kwa wale wote wapenda Urais, wanategemea kura zipi? watu wanajenga chama lakini kuna wapumbavu kila siku wao hadithi yao ni Urais tu. sasa wajitokeze.
 
Kususia uchaguzi hilo sikubaliani nalo hata siku moja, kwani hata zile sauti chache tunazozipata kuwawakilisha wananchi tutakuwa tumekubali kuzifisha na kwa hakika ccm watashangilia kupata mteremko.

Mimi kwa mawazo yangu lazima tupiganie kwa nguvu zote kupatikana kwa tume huru ya uchaguzi na lazima tupiganie kwa nguvu zote vyombo vya dola kufanya kazi kwa uhuru. Pamoja na kutambua ugumu wa kuvitenganisha vyombo vya dola na ccm vivyo hivyo kuna kazi ngumu sana ya kupata tume huru ya uchaguzi lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya ku surrender.

Na jambo jengine la muhimu sana kwa chama kichanga kinachokua kama Chadema lazima tuwe na approach tofauti ya kuwapata wagombea wetu katika nafasi mbalimbali za uchaguzi hasa chaguzi za kitaifa; vijiji/mitaa, udiwani, ubunge na hata urais.

Kwasababu ccm na vyombo vyake vya dola wanatumia hila nyingi sana dhidi ya wananchi na wagombea wetu kwahiyo ni muhimu sana kuwa na mkakati maalum wa kutengeneza na kuwa groom wagombea katika nafasi mbalimbali na kuwa na mkakati mahsusi kulingana na eneo husika na upepo wa kisiasa ulivyo. Tukizitambua hila za ccm na kuzidhibiti kwa kiasi kikubwa tutakuwa tumejihakikishia ushindi, ingawa wakati mwingine ushindi huo utasababisha madhara kwa wafuasi , wanachama na wapenzi wetu.
 
hatujachelewa.Kazi ilishaanza,hapa tunaendeleza mapambano tu.

Je itawafaa nini CDM kama wataamua kususia uchaguzi? Unadhan CDM wakisusia itabatilisha uchaguzi kwa hao watakaoshiriki?

Je huoni kama ni busara kwa hawa wanaonyimwa haki zao za kikatiba (kuchagua viongozi wao) wangeiburuza Tume ya uchaguzi mahakaman kwa msaada wa wanaharakati au kitengo chenu cha sheria na haki za binadamu? Na tuanze sasa
 
Tena nimesoma gazeti la Mtanzania Daima la Jumapili kuhusiana na mtoto wa kigogo kukamatwa China na madawa ya kulevye, tunajua sheria za china yeyote anayekamatwa na issue ya unga anapingwa risasi au kunyongwa je huyu wa kigogo kafanywaje au ndo huyo kigogo atakuwa ameuza kisehemu cha nchi yetu ili mwanae aslile risasi au kitanzi??!!! Naomba hili liwekwe wazi. Na kama aliyesema ana uhakika kwa nini asi,taje huyo kigogo ajulikane!!!

Wananchi tuwekwe wazi kama kuingia msotuni TUKO TAYARI hatuwezi kuvumilia UPUUZI HUU tena.
 
Kuna Kanuni moja ya sayansi jamii inasema hivi
''Usitumie MABAVU kupambana na mtu mwenye nguvu zaidi yako bali tumia AKILI''

*CCM inatumia PESA, VITISHO na DOLA kama sehemu ya mabavu yake ili kuendelea kukaa madarakani. Na itaendelea kufanya hivi siku zote.

*Kwa kuwa upinzani hauna nguvu za kimabavu, inabidi wakazane kutumia akili zao katika mambo haya;

1/KUTAFITI(Chanzo, Sababu, Ushahidi)

2/HOJA(kuhoji, kupinga, kukosoa, kupendekeza, kuunga mkono, kushinikiza)

3/MIJADALA(Midahalo, kongamano, warsha)

4/HARAKATI(Mikutano ya hadhara, Maandamano, Matamko, Kampeni, Migomo, Matangazo, Semina)
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom