Upinzani njaa Tanzania

WENYELE

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,291
2,000
Jamani samahani hivi CUF na Prof Lipumba walipotelea wapiii??? Nilishasema tangu mwanzo kuwa hili ndiyo anguko la CUF Tanzania bara, NCCR Maguezi nayo iko wapi naona kimya sana au kwasababu ina mbunge mmoja Mh James Mbatia, Mungu amponye nimesikia anaumwa, nakuombea upone haraka.

Ile chama ya Zito nayo nasikia wanachama waihama tu sijuwi kunaaanii Mama Ana Ngwila wapi mama!!!!! UDP ya cheo, TADEO, PPT maendeleo na ile ya Hashimu Rungwe wao wanaonekana wakati wa uchaguzi.

Baada ya UKUTA wa CHADEMA nasikia sahiz ni kupotea kwa Ben Saanane, Mungu akulinde uliko kama uko hai, ikiisha hoja ya Ben Saanane sijuwi mtakuja na nini!!!!

Huuu ndiyo upinzani wa Tanzania utakao ing'oa CCM, hamna hoja ya kudumu yenye tija kubwa kwa watanzania, sahiz hamuongelei katiba mpya wala tume huru ya uchaguzi ila 2020 mje mtuambie mmeaibiwa kura sijuwi nani atawaelewa. Sipondi upinzani ila nataka upinzani wenye tija, unaoweza kuaminiwa na watanzania na kuleta ushindani na CCM na siyo bora upinzani. zile zama za matusi zilishapita njooni na hoja, mtamkumbuka sana Mkwere. Usipende kusikia unayopenda tu sikia na ukweli huu mchungu ili upone
 
Tukundane

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
10,734
2,000
Ruhusuni mikutano muone hoja zenu mnazozijenga juu ya barufu pamoja na giriba zenu kwa wananchi zitakavyo yeyushwa kama theruji ya mlima kilimanjaro na hoja nzito kutoka kwa wapinzani,kama mtu mmoja tu,kamanda Lissu aliwaendesha mputamputa mpaka mukakata bunge live ili musiendelee kuadhilika,mikutano ikiruhusiwa UKAWA wakaanza kutema madini yao sindiyo mtatamani aridhi ipasuke mjifukie,
 
Lupyeee

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
2,685

Magazeti, redio, Tv, blogs, jamii forum mikutano ya ndani ipo, unaweza ukayeyusha hizo hoja unazoziita za barafu.

Dunia ya leo si lazima ushindishe watoto wa wenzio juani kuwahutupia upuuzi, alafu jioni unajilipa miposho kibao.
 
milangomitatu

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
1,484
2,000
Magazeti, redio, Tv, blogs, jamii forum mikutano ya ndani ipo, unaweza ukayeyusha hizo hoja unazoziita za barafu.

Dunia ya leo si lazima ushindishe watoto wa wenzio juani kuwahutupia upuuzi, alafu jioni unajilipa miposho kibao.
Taja magazeti gani? ?TV stations zipi???radio station ipi? ??inaweza kurusha habari za wapinzani kwa sasa? ?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom