Upinzani ni agano la Mungu, usaliti toka Kristo

Aug 29, 2017
90
154
Kwa kuangalia kwa jicho tenge unaweza kuhitimisha kwamba mbio za upinzani Tanzania ziko ukingoni. Hitimisho hili linashereheshwa na maneno, matendo na matamanio ya Serikali ya Awamu ya Tano (Ongeza vibwagizo "iliyochini ya mzalendo namba moja Dr. John Pombe Magufuli" na/au "Hapa Kazi Tu").

Katika historia ya ulimwengu wa kileo ni ngumu sana kuepuka marejeo ya Yesu Kristo ama Nabii Issa kwa nafasi yeyote awe kama Mungu mwana, Nabii wa Mungu au Mwanafalsafa wa mwanzo kabisa kuacha maandishi ( Nafasi yake hapa siyo mahala pake, ni mada ya toleo lijalo).

Kwa leo naomba nirejee kwa Yesu na mahusiano yake na serikali ya Kirumi ya wakati ule iliyokuwa ikiongozwa na Kaizari na " Jaji mkuu" Pilato. Yesu alionekana ni mpinzani wa serikali na mkosoaji mkubwa wa mienendo ya watawala hadi kuhukumiwa ajabu kuu la kifo kwa kuteswa "crucification".


Aidha, hata huko mbinguni kwa Mungu ( si imani yangu) inasemekana eti shetani au ibilisi alikuwa ni malaika lakini akageuka mpinzani wa bwana wake na ndo chanzo cha "uhasama" hadi hivi leo.

Usaliti wa baadhi ya watu kwa kukimbia walichokisimamia kwa maslahi ya muda mfupi au uliopo pia hayaanzi na akina Kalanga, Mtulia wala Waitara, Yuda mmoja wa mitume kumi na wawili wa Yesu alimsaliti Mwalimu wake kwa vipande thelathini vya pesa.

Ni imani yangu tu kwamba yanayojiri katika siasa za sasa nchini, yalishajiri hapa ulimwenguni maelfu ya miaka yaliyopita na mshindi anajulikana siku zote.
 
Namsikitikia sana Waitara na wenzake. Watamalizia huu muda uliyobaki na baada ya hapo (2020) wasahau kuhusu ubunge, wajiandae kufanya shughuli nyingine. Nina hakika CCM hawatawateua kamwe.
 
Baha
Namsikitikia sana Waitara na wenzake. Watamalizia huu muda uliyobaki na baada ya hapo (2020) wasahau kuhusu ubunge, wajiandae kufanya shughuli nyingine. Nina hakika CCM hawatawateua kamwe.
Bahati mbaya sana hatujui "mkataba" wao unasemaje, usikute wamepewa ubunge wa maisha.
 
Back
Top Bottom