Upinzani Ndani Ya Mtandao

Ibambasi

JF-Expert Member
Jul 25, 2007
9,277
4,682
Jumatano ya wiki iliyopita nilikuwa namsubiri rafiki yangu mmoja pale kwenye mgahawa inapoanzia barabara ya Lumumba karibu na ofisi ndogo ya CCM.Nilikuwa namsubiri rafiki yangu wakati najipatia Fanta baridi.Pembeni yangu kulikuwa na wazee wawili waliokuwa wanaongea kwa namna fulani ya kukereka kuhusu jambo lililoonekana kuwasumbua sana nafsi zao.Bahati nzuri niliweza kusikia baadhi ya mazungumzo yao,kuwa eti Muungwana ilikuwa amtimue swahiba wake wa karibu sana na aliyekuwa mpika fitina mkuu mwaka 2005 dhidi ya kina Dr. Salim na wengineo,mheshimiwa saaana Lowassa tangu April 2007, na kuwa ni busara za kina Mzee Mwinyi na Kawawa kumzuia Muungwana asimtimue swahiba wake ili kutoleta vurugu chamani na taifani kwa ujumla bali asubiri muda mwafaka.Tafadhali mwenye habari zaidi kuhusu swala hili atufafanulie.
 
mmmmmmhhhh,labda,wenye habari tupeni vioja,nadhani huu ndio muda muafaka wa kumtimua sasa.
 

Nani alisema kwenye Siasa kuna Guarantee..??

Hakuna. Lakini, amtimue kwa lipi? Kashindwa kumtimua Karamagi aje amtumue EL!! Kwanza kwa lipi hasa? Unajua sasa hivi magazeti yanaandika sana kuhusu uoza wa serikali ya awamu ya tatu ili kuwasahaulisha watu mabovu ya serikali ya awamu ya nne!

Serikali ya awamu ya nne ni washkaji na hakika nawaambia, mkiisikia JK kamtimua waziri yeyote basi ujue huyo waziri kamtukana JK personally.......Kila aliyeko kwenye madaraka sasa hivi yupo pale kwa kulipwa fadhila!

Halafu, mbona JK anaonekana "msafi na mchapakazi" ila watendaji wake eti ndio wanamwangusha? Kama ni kweli, sasa kwanini asiwatimulie mbali.....Wote lao moja tu!
 
RA anajua kucheza na Magazeti, issue inayokazaniwa kuandikwa ni ya Mkapa kiasi kwamba watu wanajishau kuhusu uozo wa awamu ya 4 ambao unaliteketeza taifa.
 
kuna wana CCM wengi tu ambao wamechoka tena sana, shida ni jinsi tu ya kuonyesha tofauti zao wanajua wanaweza kuishia pabaya kama watazungumza yanayowasibu. Kila 1 ananun'gunika chini chini.
 
RA anajua kucheza na Magazeti, issue inayokazaniwa kuandikwa ni ya Mkapa kiasi kwamba watu wanajishau kuhusu uozo wa awamu ya 4 ambao unaliteketeza taifa.

Na ndiye Rais wa nchi kwa sasa! Nadhani anaweza kuwa na "guts" za kugombea urais baada ya kipindi cha pili cha JK...ana angalia upepo unakwendaje tu... na asingekuwa na "asili ya Asia" hakika angeshagombea urais....Asante kwa Miss Tanzania wa mwaka huu kwa kutoa kiashirio cha asili hiyo kukubalika katika maeneo fulani fulani
 
Sababu za Kumtimua zipo ila nia JK hana, anachofanya sasa ni kulipa fadhila kwa wachafuzi wa majina ya watu katika mchakato wa kumpata mgombea 2005 (a.k.a mtandao). ila anaweza wabadilikia 2010 japo atashinda kwa ufinyu au kwa nguvu za dola (a.k.a kuiba kura na kutisha wananchi0
 
[QUOTE=bill;87727]RA anajua kucheza na Magazeti, issue inayokazaniwa kuandikwa ni ya Mkapa kiasi kwamba watu wanajishau kuhusu uozo wa awamu ya 4 ambao unaliteketeza taifa.[/QUOTE]


Angalia gazeti la RAI lilivyomshupalia Prof. Maghembe juu ya ufisadi wizara ya mali asili na upandaji wa bei ya mbao. Ishu yenyewe inachukuliwa kama ni personal. Kisa: ameyagusa makampuni ya uwindaji ya kwao.
 
tunatamani vurugu na ndiyo maana ya hamu na mavichwa ya habari mengi magazetini!!!!!!!

Ni kwa kiasi gani nchi hii imepata tatizo la kuibadili serikali?????
 
JK han ubavu wa kumtimua EL kwani EL ndio kamweka pale alipo.
JK hajui mtandao walikuwa wanakula nini kwa kipindi chote cha miaka kumi ya uhai wake, alikuwa hajui wanapata wapi pesa za kupiga simu, alikuwa hajui ni kwa nini wote walikuwa ni VODACOM

Kuwa kwao kwenye mtandao wa vodacom haikuwa ni bahati mbaya ila ni ili kuweza kuwekewa pesa za bure kutoka kwa RA.

kwa wale waliofuatilia uteuzi wa kule dodoma ni kwa nini wajumbe walipewa simu ambazo mtandao wake ulikuwa ni vodacom? fikiri then jadili.
 
Nadhani waungwana mnakosa kazi za kufanya...vipi mtu ukachukue maneno ya mitaani na kuja nayo JF kama si umbea.Hii ni shughuli ya kuumiza vichwa na malipo yake ni sifuri.Tupeni mambo ya uhakika tujadili lakini kuokoteza mazungumzo ya watu wanaokunywwa kahawa yao ...sioni umuhimu wake.
Kama nia ni kukandamiza..serikali basi leteni mada za kweli tujadili.lakini kukandamiza bila kuwa na nguvu ya hoja ni udhaifu.
 
Nadhani waungwana mnakosa kazi za kufanya...vipi mtu ukachukue maneno ya mitaani na kuja nayo JF kama si umbea.Hii ni shughuli ya kuumiza vichwa na malipo yake ni sifuri.Tupeni mambo ya uhakika tujadili lakini kuokoteza mazungumzo ya watu wanaokunywwa kahawa yao ...sioni umuhimu wake.
Kama nia ni kukandamiza..serikali basi leteni mada za kweli tujadili.lakini kukandamiza bila kuwa na nguvu ya hoja ni udhaifu.

Thats JF mkuu " We dare to talk openly"
 
Kuna hoja ya maana zaidi ya kujadili mustakabali wa nchi yetu na haswa upinzani ndani ya mtandao?

Mtandao kwa sasa ndio unaendesha nchi japo kwa kutumia remote control, hivyo hatuna budi kuujadili kwani the moment tunaacha kujadili hapo ndio patakuwa mwisho wa taifa hili kama bado watakuwepo lakini , tutaacha kuwajadili siku nguvu ya umma ikiwaondoa wote hapo walipo.
 
Mahakama ya Kadhi sasa hivi ni suala lingine linalotumika kutuyeyusha na kadhia ya ufisadi. Sasa hivi lakini wamechagua kete mbaya sana kudivert attention ya walalahoi kwani implications zake ni kubwa kuliko kadhia yenyewe ya ufisadi.
 
Back
Top Bottom