Ibambasi
JF-Expert Member
- Jul 25, 2007
- 9,233
- 4,608
Jumatano ya wiki iliyopita nilikuwa namsubiri rafiki yangu mmoja pale kwenye mgahawa inapoanzia barabara ya Lumumba karibu na ofisi ndogo ya CCM.Nilikuwa namsubiri rafiki yangu wakati najipatia Fanta baridi.Pembeni yangu kulikuwa na wazee wawili waliokuwa wanaongea kwa namna fulani ya kukereka kuhusu jambo lililoonekana kuwasumbua sana nafsi zao.Bahati nzuri niliweza kusikia baadhi ya mazungumzo yao,kuwa eti Muungwana ilikuwa amtimue swahiba wake wa karibu sana na aliyekuwa mpika fitina mkuu mwaka 2005 dhidi ya kina Dr. Salim na wengineo,mheshimiwa saaana Lowassa tangu April 2007, na kuwa ni busara za kina Mzee Mwinyi na Kawawa kumzuia Muungwana asimtimue swahiba wake ili kutoleta vurugu chamani na taifani kwa ujumla bali asubiri muda mwafaka.Tafadhali mwenye habari zaidi kuhusu swala hili atufafanulie.