Upinzani mjitafakari kwenda jela Kila siku si vizuri

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,233
Naomba Mjitafakari kwani kusota rumande kila siku si vizuri na makosa mengine yanazuilika au unaweza kujizuia Usiyafanye.

Heshima inashuka sana katika Jamii mtu uliyetakiwa kuwatumilia wananchi wako jimboni lakini unatumia mda wako mwingi magerezani.

Mi naomba Mjirekebishe hasa kwenye makosa ambayo yanaepukika na tutumie akina Lema kama ni funzo kwa tabia zetu.

Haiwezekani mtu ufanye vitendo vya kihuni serikali ikakuacha tuu kuna Wabunge wengine wa Upinzani kama Joseph Haule mbona hanaga uhuni huo kuna mambo mengine ni ya Kuepukika tuu.

Hasa Mheshimiwa Tundu Lissu Mara nyingi anapata wasaa wa kufanya mahojiano na Radio stations hasa za Nje kama DW, BBC ajaribu Ku control jazba na kuacha lugha za Kuudhi au Kejeli.


Troll JF Most Lovely Member
 
The only ONE can kill the opposition in Tz, but remember revolutionary ideas never die. And don't forget absolute power corrupts absolutely. The days are numbered and majority will reclaim their country the heads will will be on the spikes for all to see.
 
Maona watanzania wanapenda sana wabunge watata
Ngojea uchaguzi mkuu uje utaamini maneno yangu
 
Binafsi nashangaa comment zilivyo irrelevant wakati nimeshauri you can take it or leave it ila Uzi abuse. Mwenendo wenu unafanya niamini kuwa Mnatumia kweli Mihadarati.
 
jifunze kusimamia kile unachokiamin kuwa ni sahihi acha kuogopa jela maana huko watawala wakiamua uende utaenda tu hasa huku kwetu africa
 
Alichokisema mtoa uzi ni maoni yake ambayo siyo lazima yawe sahihi au yakubalike... ni bora ukafa umesimama kuliko kuishi maisha yako yote umepiga magoti... mwanaharakati hutakiwi kuwa mwoga, nani kafa kwa kulala jela na kunyea debe?
 
Kwani wanakamatwa kwa makosa 'genuine' au ni kwa maagizo toka juu ambaye aliwahi kutamka kuwa atahakikisha hadi ifikapo 2020 hakuna Chama chochote serious kitakakachokuwa bado kinasurvive?

Hata hivyo wanachosahau wanaccm ni kuwa hata Mzee Mandela walipokuwa wanamfungulia mashitaka mfululizo ya 'kughushi' hadi wakamfunga jela miaka 27 walidhani wabamkomoa Mandela.

Hata hivyo baada ya kutoka jela Mwaka 1991 na baadaye kuwa Rais wa kwanza Mweusi huko Afrika Kusini, akawa ni binadamu maarufu zaidi kuliko binadamu yeyote duniani aliyeishi kwenye karne ya 20.

Kwa hiyo kwa namna serikali ya CCM inavyoendelea kuwafunga jela viongozi wa upinzani kwa maagizo toka juu, ndivyo wanavyozidi kuwapaisha wapinzani maradufu!
 
kwa nn haya mambo yameshika kasi sana awamu hii?

mwanzo ilikuaje mbona haikua hvyoo...!!!
tuseme ukweli viongozi wa sasa hekma ni sifuri na busara
Yaani serikali hii ya awamu ya 5 ajenda yao kuu ni kuwafunga midomo viongozi makini wa upinzani kwa kuwafungulia mashitaka 'feki' viongozi hao.....
 
Ungewashauri haya MACCM wenzio!

Police harrasment wanayopata wapinzani sio jambo jema!
 
Haiwezekani mtu ufanye vitendo vya kihuni serikali ikakuacha tuu
Huwa unapata wasaa wa kupitia vifungu vya katiba yetu japo mara mojamoja?
Nakushauri ujenge tabia ya kusioma walau kifungu kimoja kila siku.
 
Back
Top Bottom