Upinzani kwa sasa naufanisha na timu ya Taifa Senegal 2002

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
2,360
2,000
Wakijiita Simba wa Teranga wakiwa chini ya kocha maarufu Bruno Metsu mfaransa huyu apumzike kwa amani wakiwa pia na wachezaji maarufu kama Diof,Tony silva,Diop,Ferdinand coly,Fadiga,Camara nk walifanikiwa kufika robo fainali kombe la dunia na kufungwa na Uturuki goli 1 kwa bila ikawa mwisho wao na kurudi nyumbani huku wakituachia waafrika wapenda soka majonzi makubwa.

Baada ya hapo Senegal ilipotea kwenye ramani ya Soka kabisa mpaka tena mwaka huu ambapo wamefanikiwa kufuzu kushiriki Kombe la dunia kule kwa Putin Russia wakiwa na kijana wao mahiri Mane nini kilichangia Senegal kupotea kwenye Ramani ya soka WALIJISAHAU na kutowekeza kwa vijana wakidhani kuwa kina Diof watakuwepo tu vizazi na vizazi.

Kuja kushtuka wamechelewa na kukuta jahazi limezama kabisa ila hawakukata tamaa waliamka na kusimama na kuendelea na Safari tena na leo hii wanacheza kombe la dunia.

Same same kwa Upinzani baada ya ushindi mnono walijisahau kuwekeza kwenye soka la vijana na kuishia kufanya Usajili kwa wachezaji ambao hawawez kwendana na Kasi ya Vijana hatukatai mpira wanapiga vizuri ila tatizo pumzi inakata mapema kama ni wachezaji ni kuwaingiza kipindi cha pili au kwa kwanza tu na mwishowe kuwapa mapumziko.

Ila bado wakijipanga wanamuda na haitakua mshangao tukiwaona wakicheza tena fainali za mwaka 2022

[HASHTAG]#NAM[/HASHTAG]
 

Daraja2

JF-Expert Member
Jul 10, 2017
213
250
Vp kuhusu "super eagles" ya Nigeria mwaka 1998 ilivyokomea robo kwa kupigwa 4G mkuu!?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom