Uchaguzi 2020 Upinzani kumsimamisha Membe: Kosa kubwa, usaliti na dhambi isiyosameheka

Mzalendo Uchwara

JF-Expert Member
Jan 26, 2020
3,712
11,687
Benard Membe ameweka wazi kuwa ikiwa vyama vya upinzani vitaungana na kumkubalia agombee ,basi yuko tayari kupeperusha bendera.

Hili litakua kosa kubwa, usaliti wa hali ya juu na dhambi isiyo sameheka kwa sababu zifuatazo.

1. Kama ilivyokuwa kwa Lowasa, Benard Membe atakua amejiunga na upinzani kwa maslahi yake binafsi. Sio kwamba anakubaliana na sera na falsafa za vyama vya upinzani, na wala sio kwamba anavipenda na kuvitakia mema vyama vya upinzani, hapana! Anataka kwenda huko ili tu atimize ndoto yake ya kugombea urais. Angependa zaidi kuitimiza akiwa kwenye chama anachokipenda cha CCM, lakini huko wamemtimua.

2. Kutenda kosa sio kosa bali kurudia kosa ni kosa kubwa, vyama vya upinzani vikiongozwa na CHADEMA vilifanya kosa la namna hii mwaka 2015, litakua jambo la ajabu kama watakua hawajifunza kutokana na maamuzi yale ya hovyo na yanayo kigharimu chama hadi leo hii.

3. Ni usaliti mkubwa kwa wafia chama na wananchi. Jaribu kufikiri mtu kama Tundu Lissu na wengine, wamekipigania chama usiku na mchana kwa jasho na damu, wengine wameuawa, wengine wamepata ulemavu wa kudumu na wengine wamepoteza mali zao, alafu leo hii unapowadia wakati muhimu kama huu, chama kinawaacha hawa wote na kuamua kumpa nafasi 'outsider' ili atimize ndoto zake binafsi! Ni usaliti usio sameheka. Dr. Slaa hawezi kuwasamehe CDM kwa kile walichokifanya 2015, na iwapo watakirudia tena basi kundi kubwa zaidi litajitenga nao na kuunga mkono juhudi, kuwanini ujitese wakati unao wahangaikia hawauoni umuhimu wako?

4. CCM wanaweza kuwa wanapanga hizi drama za Membe na chama chake, kama anavyojitapa yeye mwenyewe kuwa alikua mtumishi kwenye ile idara nyeti, basi tukae tukijua uzandiki na hujuma ni sehemu tu ya umahiri wake. Chama chake pendwa kinaweza kuwa kinamtumia kwa wakati huu ili kuuweka uchaguzi mkuu 'under control', akigombea mtu wao kama Membe hata akishindwa basi wana uhakika wa kumpa maelekezo awatulize wafuasi wake kuwa mambo yanashughulikiwa kwenye vyombo vya kisheria.

Lakini akigombea mtu radical wa upinzani, wanahofu kuwa anaweza kukataa matokeo na kuhamasisha wananchi wayakatae matokea kwa nguvu zote. Mwisho wa siku nchi inaweza kutumbukia kwenye sintofahamu itakayo hatarisha utawala wa CCM (au usalama wa taifa kwa mujibu wa viongozi wa CCM).
 
2. Kutenda kosa sio kosa bali kurudia kosa ni kosa kubwa, vyama vya upinzani vikiongozwa na CHADEMA vilifanya kosa la namna hii mwaka 2015, litakua jambo la ajabu kama watakua hawajifunza kutokana na maamuzi yale ya hovyo na yanayo kigharimu chama hadi leo hii.
Siasa ni watu; CHADEMA haikufanya kosa mwaka 2015 kwa waliyemsimamisha alikuwa na mtaji wa watu na huo mtaji ndio uliompa idadi ya kura zile zilizotangazwa. Ila kwa Membe sidhani kama ana mtaji wa watu kihivyo
 
Mbali na watu, ni muhimu kulinda taswira na itikadi ya chama, unaweza kupoteza mwelekeo kabisa kwa sababu ya 'boost' ya muda mfupi.

Hata angesimama Slaa, kwa upepo wa 2015 ni wazi kuwa angepata kura nyingi vilevile.
 
Ili kunogesha uchaguzi mwaka huu wagombea wawe kama ifuatavyo:-
1. CCM - Mh. J P Magufuli
2. CHADEMA - Mh. Tundu A Lissu
3. ACT - Mh. Benard Membe

Nina hakika mshindi hatavuka 60% na wengine watakuwa na 40%.
 
Membe anachotaka ni uraisi. Kama Lowasa anasubiri moja ya mawili haya litokee ndio ahamie upinzani. Ama CCM wamfukuze au wamkate. Akili yake iko CCM, kama kweli anaelewa upinzani wakati wake ni sasa wa kuvuka mto. Huko nyuma nilijiuliza hivi hata kama Lowasa angeshinda-CDM ingekuwa na lao au angeiendesha CDM vile anaona. Kwangu ni afadhali kukosa kura lakini una jeshi lako unaloliamini na siku nyingine mnaweza kuvuka. CDM hata kama wangeshindwa wakiwa na Slaa naamini sasa wangekuwa imara zaidi.
 
Back
Top Bottom