Upinzani Kenya wadai Serikali inatumia Shirika la Ujasusi NIS kuwasajili wageni kama wapiga kura

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
1c54b6c1ed5029448526c6c4266aaa53.jpg
Kiongozi wa Muungano wa Upinzani nchini Kenya (CORD) Raila Odinga anaishtumu Serikali kwa kutumia idara ya ujasusi nchini humo NIS kuwasajili raia wa nchi jirani kama wapiga kura kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Agosti

Odinga amesema kuwa shirika hilo limeweka mikakati ya raia wanaoishi katika mpaka na Kenya ambao ni raia wa Uganda na Ethiopia kuja nchini kujiandikisha

Aidha, amedai kuwa Serikali inapanga kutumia mbinu iliyotumia mwaka 2007 na 2013 ili kuiba kura, suala ambalo amesema upinzani hautakubali

"Lazima idara hii ijitokeze na kuacha inachokifanya, hatutakubali kinachoendelea", alisema Odinga

"Inabidi Tume ya uchaguzi iachiwe kazi ya kuwasajili wapiga kura" aliongeza Odinga

Hivi karibuni Odinga na kinara mwenzake wa upinzani Kalonzo Musyoka, walidai kuwa namba za vitambulisho vyao vimetumiwa kuwasajili wapiga kura wengine, madai yaliyoshughulikiwa na Tume ya uchaguzi

Tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC wiki iliyopita, ilianza zoezi la mwezi mmoja kuwasajili wapiga kura wapya

IEBC imesema zoezi hilo ambalo linatarajiwa kumalizika Februari 14, linawalenga wapiga kura wapya milioni 6 ambao hawakupiga kura mwaka 2013

Wapiga kura milioni 24 wanatarajiwa kushiriki katika zoezi la kupiga kura tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu baada ya zoezi hili kukamilika

Rais Uhuru Kenyatta anatetea wadhifa wake huo Muungano wa upinzani bado hujatangaza mgombea wake.
 
Back
Top Bottom