Upinzani kabla hatujamkaribisha Membe katika viunga vyetu tunaweza kumpa mtihani huu was yeye kwenda mhakamani kuishitaki CCM

Thailand

JF-Expert Member
Nov 15, 2019
262
778
Upinzani msipokuwa macho mnaweza Kila mwaka wa uchaguzi mkawa Ni wa kutumiwa tu na watu was CCM wasipopata wanachokiitaji wanatuacha Kama ilivyotokea kwa Lowasa na Fredrick Sumaye.

Tunaweza kumpima Membe kwa mtihani mdogo tu kabla hatuja msaini rasmi kwenye chama mojawapo Cha upinzani.
Katiba ya CCM inaruhusu Kila mwanachama kugombea nafasi yoyote ya Uongozi Kama Ni kipindi sahihi Cha kufanya hivyo bila kubagua kwa visingizio vyovyote mtu yeyote atakae weka Nia ya kugombea nafasi hiyo.

Sasa kwa Nini uongozi was CCM kuchapisha form moja hali inajua kwa kufanya Hilo Ni kwenda kinyume na takwa la kikatiba. Kwanini wasinge ruhusu Kila Mwenye Nia ya kuchukua form achukue aende ashindwe kwenye kura ya maoni ndani ya chama!

Kwa hiyo Membe ili upate kibali huku upinzanini lazima utuoneshe kwanza namna unavyowasulubu hao Wana CCM wenzako waliokunyima nafasi ya kugombea Urais huku ukiwa umejiandaa kwa muda mrefu na huku unakidhi vigezo vya katiba yenu.

Upinzani tutafeli Sana endapo tutaendelea kuamini Hawa viumbe was kijani kufika chamani na kukabidhiwa nafasi kubwa ya kugombea Urais huku tukiwaacha wafia chama wetu wakitushangaa kwa makosa tunayoyafanya.

Yaani Membe hasipowaburuza mahakamani CCM kwa kosa Hilo walilofanya akakimbilia upinzani hiyo nafasi atakayopewa Ni Bora abaki akisapoti upinzani ila twende na Tundu Lissu au John Heche vijana shupavu wasioogopeshwa na kelele za fisiemu.
 
Hahah hawezi hata kwa dawa,CCM made him.

Vyeo,Exposure,Mali alizonazo,nafasi za watoto wake/ndg zake kwny maofisi manono anajua bila CCM asingevipata so huyo ni mshirika wao wa kufa na kuzikana.

Wapinzani waende na Lissu.
 
Upinzani msipokuwa macho mnaweza Kila mwaka wa uchaguzi mkawa Ni wa kutumiwa tu na watu was CCM wasipopata wanachokiitaji wanatuacha Kama ilivyotokea kwa Lowasa na Fredrick sumaye.
Tunaweza kumpima Membe kwa mtihani mdogo tu kabla hatuja msaini rasmi kwenye chama mojawapo Cha upinzani.
Katiba ya CCM inaruhusu Kila mwanachama kugombea nafasi yoyote ya Uongozi Kama Ni kipindi sahihi Cha kufanya hivyo bila kubagua kwa visingizio vyovyote mtu yeyote atakae weka Nia ya kugombea nafasi hiyo.
Sasa kwa Nini uongozi was CCM kuchapisha form moja hali inajua kwa kufanya Hilo Ni kwenda kinyume na takwa la kikatiba. Kwa Nini wasinge ruhusu Kila Mwenye Nia ya kuchukua form achukue aende ashindwe kwenye kura ya maoni ndani ya chama!
Kwa hiyo Membe ili upate kibali huku upinzanini lazima utuoneshe kwanza namna unavyowasulubu hao Wana CCM wenzako waliokunyima nafasi ya kugombea Urais huku ukiwa umejiandaa kwa muda mrefu na huku unakidhi vigezo vya katiba yenu.
Upinzani tutafeli Sana endapo tutaendelea kuamini Hawa viumbe was kijani kufika chamani na kukabidhiwa nafasi kubwa ya kugombea Urais huku tukiwaacha wafia chama wetu wakitushangaa kwa makosa tunayoyafanya.
Yaani Membe hasipowaburuza mahakamani CCM kwa kosa Hilo walilofanya akakimbilia upinzani hiyo nafasi atakayopewa Ni Bora abaki akisapoti upinzani ila twende na Tundu Lissu au John Heche vijana shupavu wasioogopeshwa na kelele za fisiemu.
Ana kesi dhidi ya Musiba ambayo mapaka itakapoamuliwa inaweza ikampa ushindi kwa sababu maneno ya Musiba ndiyo chanzo cha hata yeye kufukuzwa huko. Membe tayaru ana kesi huko Mahakamani.
 
Tumewaambia kabisa na wapinzani waliokula hela za Membe wamrudishie haraka sana. Kilichotokea kwa Lowassa kimetufundisha kutokurudia kosa. Uzuri maoni yetu yako wazi kwa Membe, na hivyo vyama kuona msimamo wetu.
 
Ana kesi dhidi ya Musiba ambayo mapaka itakapoamuliwa inaweza ikampa ushindi kwa sababu maneno ya Musiba ndiyo chanzo cha hata yeye kufukuzwa huko. Membe tayaru ana kesi huko Mahakamani.

Rudisha hela ya Membe tafadhali, usimdamganye kuwa unaweza kumpigia debe kwenye upinzani wa kweli. Vinginevyo kama umeshaanza ujenzi, mpeleke TADEA.
 
Mkuu nadhani hufatilii zaidi kuhusu membe na CCM, aende mahakamani kwa lipi? Membe alishafukuzwa CCM zamani sana hata kabla ya mchakato wa kuchukua fomu

Sasa anaenda mahakamani kama nani?

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Hao wapinzani wenyewe tunawaamini kwa vipimo gani hadi huyo Membe tumuwekee mtihani wa kumpima?
 
Back
Top Bottom