Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,007
- 9,873
Wafuasi wa upinzani wamekuwa wakipinga hatua ya rais ya kugombea kwa mara ya tatu. Upinzani huko Ivory Coast umekataa mpango wa serikali wa kufanya mabadiliko katika tume ya uchaguzi kabla ya uchaguzi utakaofanyika wiki ijayo na kusisitiza kwamba utasusia uchaguzi huo.
Rais Alassane Ouattara anatafuta kuchaguliwa katika muhula wa tatu hatua iliyozua utata. Kugombea kwake kumesababisha maandamano kote nchini humo.
Umoja wa Mataifa umeonesha wasiwasi wake kuhusu ghasia zinazoendelea ambazo zimesababisha vifo vya watu karibu saba huku zaidi ya 40 wakijeruhiwa, kwa mujibu wa serikali.
"Wagombea wa upinzani wanasisitiza kuwa wataendelea kuasi dhidi ya utekelezaji wa sheria na kusema wanataka taasisi za kimataifa kuingilia kati," Maurice Kakou Guikahue, msemaji wa upinzani, alizungumza na wanahabari Alhamisi.
Wagombea wawili wa upinzani – aliyekuwa rais, Henri Konan Bédié, na aliyekuwa waziri mkuu, Pascal Affi N'Guessan – walitangaza kususia uchaguzi mapema mwezi huu.