MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 31,757
- 48,407
Upinzani wa Tanzania mjilaumu wenyewe tu, maana chaguzi za serikali za mitaa mligomea na kuona kilichotendeka, CCM walizoa kila kitu bila kupepesa macho, maana kwamba walikua tayari kuwafuta kwenye historia ya nchi, walikua tayari kufanya chochote na lolote bila aibu.
Sasa mmekuwa mkilaumu kwamba tume ya uchaguzi ina upendeleo, kwamba sio huru, kwamba inafuata maagizo ya CCM, licha ya yote mkadiriki kuhusika kwenye uchaguzi chini ya hiyo hiyo tume, mkafanya kampeni iliyokua inahudhuriwa na nyomi kubwa iliyoonyesha kweli mamilioni ya Watanzania walikua wanawapenda, mkafanya CCM wapanic zaidi, ndio hayo matokeo yake, wamekumbakumba kila kitu kiasi kwamba hata wafuasi wa CCM wengi wameonyesha kufedheheshwa na kilichotokea, japo kunao wanajipa ujoto humu kwenye mitandao lakini mioyoni inawauma.
Kwa umoja wa taifa mkubali kusonga mbele hamna kikubwa mnachoweza kukifanya, imeisha hiyo, mlijipeleka kichinjioni huku mkilalamika na ndio hayo matokeo yake. Bunge lote ni kijani kwa kwenda mbele.
Akina Kagame na Museveni popote walipo wanachekelea tu. Afrika tamu sana hili bara.