Upinzani hapa kwetu jifunzeni kitu: Ukishindwa usitafute sababu ya kususa ambayo haipo

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,663
18,036
Wale makamishina wanne wa tume ya uchaguzi ya kenya wametoa sababu kwa nini hawakubaliani na matokeo yaliyotangazwa na mwenyekiti wa tume yao. Raila ametumia hoja ya makamishina hao kama msingi wa kutokuyatambua matokeo yaliyotangazwa. Tuangalie kwa karibu sababu za kususia matokeo hayo:

1. Asilimia za ushindi za wagombea wanne zikijumlishwa zinafika 100.01%. Kimahesabu ilitakiwa zikijumlishwa ziwe 100%.

MAELEZO: Asilimia iliyotangazwa ni approximately (iliyokadiriwa kwa desimali 2). Hii inakubalika kimahesabu, ili mradi haibadilishi nafasi ya mgombea. Ngoja tuoneshe asilimia bila kukadiria:

* Williamu Ruto: 7,176,141/14,213,027 x 100 =50.489885089%. Ikakadiriwa kuwa 50.49%

* Raila Odinga: 6,942,930/14,213,027 x 100 = 48.849059388%. Ikakadiriwa kuwa 48.85%

* George Wajackoyah: 61,969/14,213,027 x 100 = 0.4360014232%. Ikakadiriwa kuwa 0.44%

* David Waihiga: 31,987/14,213,027 x 100 = 0.2250541%. Ikakadiriwa kuwa 0.23%

Ukijumlisha hizo asilimia bila kukadiria kwa desimali 2:
50.489885089%
48.849059388%
+ 0.4360014232%
0.2250541000%
JUMLA: 100%

Ukijumlisha kwa kukadiria desimali 2: 50.49% + 48.85% + 0.44% + 0.23% = 100.01%

Kwa mtu aliyeaminiwa kuwa kamishina wa tume huru ya uchaguzi, kutumia sababu ya kujumlisha asilimia kwa kutumia zilizokadiriwa na kufumbia macho asilimia halisi ili kujenga hoja NI AIBU YA MWAKA. Pia Raila kukubali hoja hiyo na kuifanya kama sababu ya kugomea matokeo na kwenda mahakamani ni AIBU YA MWAKA PIA. Ukitilia maanani kuwa wote Raila na Ruto wamekadiriwa kwa kiasi sawa! Ruto amekadiriwa kwa juu ikawa 50.49% na Raila amekadiriwa kwa juu ikawa 48.85%.


Hiyo sababu haiwezi kuwa sababu ya kubadilika kwa mshindi, achilia mbali kuwa makamishina hawakupaswa kujumlisha hivyo.

Lakini pia kwa makusudi kabisa hilo ongezeko la 0.01% wakadai ni ongezeko la kura zaidi ya laki moja. Wakati hata kama hilo ongezeko ni ongezeko halisi (wakati si ongezeko halisi) basi lingekuwa ni ongezeko la kura 1,421 tu. Hata kama hizo ukiamua kuzitoa kwa Ruto na kumpa Raila bado isingebadili mshindi wa uchaguzi huu.

Sasa hiyo hoja ndiyo hoja kubwa sana kwa mtazamo wa wale makamishina wanne waliosusa na wakaifanya hoja namba MOJA.

2. Makamishina wanadai hawakushirikishwa! Wanadai walioneshwa tu matokeo ambayo yameshaandikwa tayari, mwenyekiti hakutupa nafasi ya kuyahaskiki! Ikumbukwe kuwa kuna timu ya wataalamu wa tume waliokuwa wanahakiki matokeo pamoja na mawakala wa wagembea wote. Hivi inaingia akilini kazi kubwa ya kuhakiki matokeo ya kwa siku 6 iliyofanywa na watu wengi sasa iweze kuhakikiwa tena na makamishina 7 kwa masaa machache kabla ya matokeo kutangazwa!! Hicho ni kitu kisichowezekana na kililenga kutaka kukwamisha zoezi zima! Kwa hiyo namuunga mkono mwenyekiti kutumia mamlaka yake ya kikatiba kutangaza matokeo, asiyeridhika aende mahakamani!!

Ushauri wangu kwa Raila: Matokeo ya vituo vyote wanayo, na jumla ya kura aliyopata anaifahamu, aseme bayana amepata ngapi? Mawakala wake walishiriki uhakiki, ni vituo vipi ambavyo kura zake zimepunguzwa? Vinginevyo ANAJIAIBISHA!!




.
 
Wakikusikiliza watakuwa wametusaidia sana, mkuu. Sisi hapa tuko na presha kubwa sana sana ya maandalizi ya uapisho wa president-elect Ruto.
 
Back
Top Bottom