Upinzani haipo Katiba Mpya bila kutoleana uvivu

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,822
35,817
Nani asiyejua umuhimu wa katiba mpya? Nani anaweza kuthubutu kujipa jukumu hilo peke yake na kuwasusa wengine kwa sababu zozote zilizokwisha pita?

Misahafu inasema ni furaha kuu mbinguni kwa mwenye dhambi mmoja akitubu.

Hivi hata ya waungwana hatuyasikii?



Nini tofauti ya ya chawa uchwara wanaowanyanyapaa kina Bashiru, Polepole au wengine wajao na yule mwana mwema aliyechukizwa na kurejea kwa mwana mpotevu nyumbani kwa baba yake?

Waelimishwe wanachama na mashabiki kuzielewa agenda za chama dhidi ya chuki binafsi.

Ifahamike agenda za chama ni za kudumu, si marafiki wala maadui.

Tufike mahali tupeane makavu.

Mpo ndugu ambao kwa hakika (siyo siri) mnakera.
 
Demokrasia ina masomo magumu sana ambayo wapinzani lazima wayasome na kuyaelewa, lazima watambue, mtu kukunyima haki yako ulipoihitaji haina maana nae hastahili kupewa haki yake atakapoihitaji.

Haki haina double standard, siku zote imesimama staright kwa wote, mtendee mwenzio unachotaka kutendewa wewe, kinyume na hapo ni ubinafsi, nothing else.

Hizi mentality za visasi zinaonesha vile wanaoipigia kelele demokrasia kila siku wamejaa visasi, hawa wanaoneaha nao wakipewa madaraka kuna uwezekano mkubwa wakaja kufanya kama watawala wa CCM wanvyofanya, ni wabinafsi kama CCM.

Nilidhani wangejifunza kwa Polepole, kumbe I was wrong, Dr. Bashiru amekuja kunithibitishia kwamba hawa watu bado hawajakomaa kidemokrasia, bado wanaamini haki iko upande wao zaidi ya wengine, na hata ikitolewa kwa wengine, basi iwe na exceptions!.

Huu ubinafsi utatuchelewesha sana kuyafikia malengo, na kwa hili wasilaumiwe CCM pekee, kwani hata wapiga debe wa upinzani mitandaoni nao wanastahili kubeba sehemu ya hizo lawama, huu ndio ukweli.
 
Demokrasia ina masomo magumu sana ambayo wapinzani lazima wayasome na kuyaelewa, lazima watambue, mtu kukunyima haki yako ulipoihitaji haina maana nae hastahili kupewa haki yake atakapoihitaji...

Ninakazia:

"Waelimishwe wanachama na mashabiki kuzielewa agenda za chama dhidi ya chuki binafsi."

Agenda za chama ni za kudumu, si maadui wala marafiki.

Ni wazi kuwa wanatuchelewesha sana wanaoendekeza siasa za chuki:

Siasa za chuki: Tanzania tunakwama wapi?
 
Nani asiyejua umuhimu wa katiba mpya? Nani anaweza kuthubutu kujipa jukumu hilo peke yake na kuwasusa wengine kwa sababu zozote zilizokwisha pita...
Ulipomuongelea Bashiru ndio umeharibu ujumbe wako wote. Hana usafi wowote ni mwanasiasa maslahi na kama yeye wamejaa CCM akipewa jukwaa la kuongea kila mtu anashawishiwa sasa fuatilia kwa undani huo uadilifu wake ni vituko vitupu.
 
Ulipomuongelea Bashiru ndio umeharibu ujumbe wako wote. Hana usafi wowote ni mwanasiasa maslahi na kama yeye wamejaa CCM akipewa jukwaa la kuongea kila mtu anashawishiwa sasa fuatilia kwa undani huo uadilifu wake ni vituko vitupu.

Kwa nini CCM mnachomwa sana kumoyo mnapoona jitihada yoyote ya umoja wetu?

Kwamba CCM wewe umekuwa na uchungu na upinzani ghafla?

Kwamba Kila mdhambi hana fursa ya toba? Kuwa hiyo ndiyo hoja yako sasa?

Watu kama wewe tuliwaangazia huku:

Tuwatambue wanaohaha kutusambaratisha kama Taifa

Nadhani hata wewe ulitajwa mle.

Kwani Bashiru si mtu ndugu?
 
Kwa nini CCM mnachomwa snap kumoyo mnapoona jitihada yoyote ya umoja wetu?

Kwamba CCM wewe umekuwa na uchungu na upinzani ghafla...
Ujumbe wake una mashiko lakini mazingira yake ya sasa yanamfanya aeleweke vingine anapojitokeza na kuikosoa serikali ambayo ingeweza kumpotezea mazima na SSH asingefanywa lolote na yoyote yule.

Anadhihirisha kuwa nyuma yake anao watu wengi wenye maoni kama yake na walikuwa wakisikika kwanza ili baadae mkubwa wao aje kusikika. Kwamba ana kinyongo cha hali ya juu hata anapokuwa ndani ya mikutano ya CCM ni ukweli kabisa kwa ushahidi wa maneno aliyosema hadharani.

Ni huyu huyu Bashiru aliyewaita wazee wa CCM wapumbavu wanaofanya mambo ya kipumbavu kipindi kile akiwa katibu mkuu wa CCM, Maisha yanakwenda kasi sana.
 
Ujumbe wake una mashiko lakini mazingira yake ya sasa yanamfanya aeleweke vingine anapojitokeza na kuikosoa serikali ambayo ingeweza kumpotezea mazima na SSH asingefanywa lolote na yoyote yule...

Inafahamika kuwa aliyosema Bashiru ni kweli na ni mwiba mchungu mno kwenu ma CCM.

Kwetu Bashiru ni mfano wa mtoto mpotevu aliyerudi kwa baba yake. Kwetu toba ni haki ya wote.

Kwa wanaomnyanyapaa Bashiru upinzani, ni mfano wa mtoto mwema aliyechukizwa na kurejea kwa mwana mpotevu nyumbani kwa babaye.

Huo ndiyo msingi wa hoja

Kwamba tunajua mnavyoshadadia utengano wetu? Itoshe kukufahamisha bwana Philipo - hatudanganyiki!

Nia yenu mbaya tunaijua.
 
Back
Top Bottom