Upinzani bungeni: Serikali iache visingizio hali ngumu ya maisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upinzani bungeni: Serikali iache visingizio hali ngumu ya maisha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Magezi, Jun 18, 2010.

 1. M

  Magezi JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  17th June 2010

  Kambi ya Upinzani Bungeni imeitaka serikali kuacha visingizio kuhusu hali ya maisha inayozidi kuwa mbaya miongoni mwa wananchi wa kawaida kila kukicha, badala yake itafute mbinu ya kupunguza makali ya maisha "kwani hali ni ngumu kwa sasa kuliko wakati wowote".

  Akichangia hotuba ya Bajeti ya Waziri Mkuu na ile ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Msemaji Mkuu wa upinzani katika eneo hilo, Dk. Willibrod Slaa, alisema uchunguzi wa kambi hiyo unaonyesha kwamba bei ya karibu kila kitu imepanda maradufu lakini kipato cha Mtanzania kimebaki pale pale, huku nguvu ya mwananchi kununua bidhaa hizo ikishuka kwa kasi kutokana na kuporomoka kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania.

  "Mathalan wananchi wengi wameacha kunywa chai kwa vile sukari sasa imekuwa bidhaa ya anasa, wastani wa Sh. 1,200 hadi 1,800 wakati mwaka 2005 ilikuwa Sh. 500-600, mikate iliyokuwa kimbilio la walalahoi hasa mijini imekuwa haishikiki tena kwa vile bei inakimbilia Sh. 1,500 – 2,000.

  Nyama inazidi kuwa hadithi ya kusadikika kwani inakimbilia kati ya Sh. 4,500 na Sh. 5,000 kwa kilo katika maeneo mengi," alisema. Alisema mchele ambao ukiacha mahindi unakuwa chakula cha Watanzania wengi unakimbilia sh. 5,000 kwa kilo huku hata kitoweo cha maharage kilichokuwa mkombozi wa familia nyingi nacho hakishikiki kwani kilo katika maeneo mengi ni zaidi ya sh. 1,000.

  "Ndiyo maana kuna msemo ‘all politics is local' (siasa zote zilenge watu wa kawaida). Visingizio vya hali ya uchumi wa dunia hauwahusu wananchi kwani waliiweka/ajiri serikali kwa lengo pekee la kushughulikia masuala hayo," alisema na kuongeza kwamba serikali inaposhindwa kutimiza hayo ndiyo inaitwa; "Serikali iliyoshindwa maslahi ya ndani ya wananchi wake."

  Alisema hali hiyo inafanya taarifa ya serikali kuwa wastani wa kipato cha Mtanzania kwa mwaka 2008 ni sh. 682,737 inapoteza maana kwani watu wenye kipato hicho wasingeshindwa kununua angalau sukari na mchele.

  Alisema wananchi wanataka kula vizuri, kulala vizuri, mishahara inayokidhi haja na siyo takwimu zinazoonyesha kukua kwa uchumi.

  "Wananchi hawali takwimu za vitabuni. Wanahitaji mahitaji yao muhumu kwa maisha ya kila siku," alisema.

  Hata hivyo, Dk. Slaa alisema kambi ya upinzani inapotoa tathmini kuhusu hali ya sasa ya wananchi si kwamba haioni kama kuna mambo mazuri yaliyofanywa na serikali kuanzia zama za chama cha Tanu hadi CCM.

  "Tunachosema ni kuwa kwa raslimali tulizonazo tungeweza kufanya vizuri zaidi…Tungelizielekeza kwenye maeneo muhimu yanayomnufaisha mwananchi," alisema.

  Dk. Salaa ambaye wakati akirusha ‘madongo' mitambo ya televisheni ya taifa ilizima na kuwashwa akiwa kamaliza kuongea, alisema kambi ya upinzani haiwezi kupoteza muda kuzungumzia vitu ambavyo vimefanywa, bali kila wanapochambua mambo wanagundua kwamba vipaumbele vingi vya serikali vina kasoro na kwamba hata pale pesa zinapoonekana kama zimetengwa kwa ajili ya kurekebisha mambo, mara nyingi huwa si kweli ama hazisimamiwi vizuri.

  Alisema serikali isiyoweka vipaumbele kwa wananchi wake ni serikali pia isiyojali wananchi.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Ukisoma kwenye nyekundu hapo juu, hivi TBC1 wana akili kweli?? CCM bado wananfikiri wananchi hawajui ghiliba ambazo wanawafanyia?? Ndo maana yakiambiwa ukweli yanakuja juu kwa sababu yamezoea kwamba watanzania wote ni wajinga na hawajui.......wanajidanganya.
   
 3. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Dk. Salaa ambaye wakati akirusha ‘madongo' mitambo ya televisheni ya taifa ilizima na kuwashwa akiwa kamaliza kuongea,

  Ningepeda kusema ilizimwa badala ya ilizima! Na hicho ndio CCM wanachokiogopa wananchi kuusikia ukweli! Wamefanikiwa kuwaweka gizani kwa nusu kilo za chumvi! wanajua fika kwamba siku mwananchi atakapo funguliwa macho utakuwa mwisho wao!
  Shame on you TBC m/genzi mkubwa kama wewe T.M unaleta siasa za kizandiki namna hii! Shame on you TM
   
 4. M

  Magezi JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Siamini hata mtu kama Tido mhando aliyekwisha fanya kazi BBC bado anakubali kutongozwa na analainika kwa CCM?
   
 5. MANI

  MANI Platinum Member

  #5
  Jun 18, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Inauma TBC inayoendeshwa kwa kodi zetu inakuwa upande wa CCM tu ! Lakini kila lenye mwanzo lina mwisho kwani huko Mkuranga wapo waliorudisha kadi za CCM na ilionyeshwa na kukatwa na ITV sasa sijui kuficha maradhi ndio kuponya, ngoja oktoba ifike waone.
   
 6. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #6
  Jun 19, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,212
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  Kinachohitajika ni Chadema kuwa na redio station yake au angalau inayowaunga mkono, magazeti yake, na hata TV zake. Hizi mass media za serikali kisiasa ni za wote lakini kiukuweli ni za CCM.

  Tuko katika mfumo wa vyama vingi, lakini Katiba tunayotumia iliundwa wakati wa mfumo wa chama kimoja (1977), na mfumo wa utendaji serikalini bado ni ule wa wakati wa chama kimoja.

  As it has been said, you can cheat some of the people some of the time, but you cannot cheat all the people all the time.

  Si Kikwete anawapa wanafunzi wote laptop? Vitu kama hii hotuba ya Dr. Slaa vitawafikia wananchi kwa njia kama hiyo.
   
Loading...