Upigwaji mnada ng'ombe 6,000 vs uchomwaji moto vifaranga 6,000

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,022
40,691
Naomba kufahamu tofauti za kisheria zinazopelekea ng'ombe 6,000 walioingizwa kinyume cha sheria toka Uganda kupigwa mnada na vifaranga 6,000 vilivyoingizwa kinyume cha sheria kutoka Kenya kuchomwa moto. Naomba ufafanuzi wa kisheria tafadhali.
 
VIFARANGA NI WADOGO WANACHOMEKA KIRAHISI MKUU.HAO NG'OMBE TUTAHITAJI MOTO MKUBWA MNO KUWACHOMA NA TUTACHAFUA ANGA KWA MOSHI...(In mkulu's voice)
 
VIFARANGA NI WADOGO WANACHOMEKA KIRAHISI MKUU.HAO NG'OMBE TUTAHITAJI MOTO MKUBWA MNO KUWACHOMA NA TUTACHAFUA ANGA KWA MOSHI...(In mkulu's voice)
Kwahiyo hakuna mbinu nyingine ya kuwateketeza ng'ombe hao ili kuepuka kuingiza magonjwa toka nje ikiwa ndio hoja iliyotumika kuteketeza vifaranga? Kwahiyo tunaogopa magonjwa ya aina flani tu na magonjwa mengine tuna ubia nayo?
 
Ng'ombe wangeingizwa kipindi kile cha ugonjwa was bonde la ufa bila Shaka wangechomwa.....vifaranga vimeingizwa kipindi hiki cha ugonjwa wa mafua ya ndege ambao majirani zetu wameshaulipoti kuingia nchini mwao.....
 
Kenya kuna mafua ya ndege? Tupeane updates
 
Uganda umelipotiwa......na nchi ikisha patwa na huo ugonjwa kinachofuata ni kuteketeza ndege wote.....mbona imeshatokea nchi kazaa za ulaya.
 
Hata mimi nashangaa kwanini ng'ombe wanapigwa mnada alafu vifaranga wachomwe moto!!

Au wenda yule dadaalikua mpinzani au kuna kigogo alikua anamfukuzia?
 
Back
Top Bottom