Upigaji wa kura bungeni ya kutokuwa na imani na serikali unawezekana kwa kiasi gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upigaji wa kura bungeni ya kutokuwa na imani na serikali unawezekana kwa kiasi gani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gosbertgoodluck, Jan 24, 2011.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Jan 24, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Wazee,

  Nimemsikia Mhe. Kafulila kwenye matangazo ya Dira ya Dunia ya Idhaa ya Kiswahili BBC leo akieleza mpango wake wa kupeleka hoja bungeni ili wabunge wapige kura ya kutokuwa na imani na serikali. Naomba wataalam wa sheria hususani kwenye masuala ya bunge watuelimishe kidogo kuhusu mpango huu. Kwa kuangalia bunge letu la sasa, hivi kweli mpango huu wa Mhe. Kafulila unaweza ukainyima usingizi serikali?

  Tafadhali karibu kwa mawazo.
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  DOWANS KABURI LA DHAHABU KWA CCM NA MAFISADI WAKE WOTE:

  Kwa maoni yangu: Dowansi ni KABURI LA DHAHABU kwa CCM na Mafisadi wote nchini lililoletwa na Mwenyezi Mungu kutuokaa jumla Watanzania baada kusikia kilio chetu cha dhati dhidi ya dhuluma nyingi chini kwa miaka mingi.

  Jamani kweli Mungu yupo, hasinzii wala hapuuzi hata sauti zetu sie akina Matonya wa ulimwengu huu!!!

  Watanzania, Mungu yupo na anatupenda sanaaa hivyo tuache kumkasirisha kila mara kwa kukubali mtu kutugawanya kwa misingi ya imani zetu!!!
   
 3. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2011
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,804
  Likes Received: 6,314
  Trophy Points: 280
  Wabunge wa CCM juzi juzi hapa walipelekwa seminar na wakaambiwa wawe kitu kimoja na wafute tofauti zao ndani ya bunge lijalo ili kudhibiti upinzani.

  Kuna haja ya taasisi husika kutoa elimu ya uraia kwa wabunge wa CCM kwamba hata kama itatokea uchaguzi ndani ya bunge (speaker, kutokuwa na imani na PM etc), kura ni SIRI na Serikali will never know who voted against them. Tusidhani wanavijiji peke yao tu ndo wanahitaji elimu hii.
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  WABUNGE WAKOME KUPIGA KELELE KAMA WALEVI KLABUNI PINDI
  WANAPOTOLEA MAONI MISWADA MBALIMBALI BUNGENI:


  Taratibu za kupitisha miswada bungeni kwa KUPIGA KELELE ZA DIO AU LAA kama walevi kamwe haipendezi kwa waheshimiwa wabunge wetu katika bunge zetu Dodoma na Zanzibar.

  Tubadilishe haraka hii KANUNI YA BUNGE na upitishwaji miswada ifanyike kwa KURA ZA SIRI na ijulikane wazi kwamba hoja gani ilipitishwa kwa kura ngapi hasa kuliko kuwafanya waheshimiwa wabunge wetu kila mara kutia aibu kwa kupigia kelele mswada utafikiri wwako kilabuni.

  Mara utawasikia ... NDIOOOOO IPITEEEE ... mimi kama spika natangaza kwamba hoja hii imepita kwa kauli moja. Jamani 'kauli moja ndio sawa na kura ngapi maana DEMOKRASIA ni mpaka tuhesabu kura na matokeo yafahamike???

  Katika bunge la Februari kwanza tukomeshe HUU UTAMADUNI WA ENZI ZA CHAMA KIMOJA kujipitishia tu mambo na hata mjumbe aliyekua anachapa usingizi kuibuka na kuunga tu tera kwenye kupiga kelele za ndioooo naunga mkono hoja asilimia mia kwa mia kama alivyosema mjumbe aliyetangulia.

  hata mjumbe mwenyewe hamtambui wala kilichosemwa hana habari nayo maana alikua usingizini. Jamani haka kautamaduni kabadilishwe haraka na UBORA WA SHERIA NA MISWADA mbali mbali watu tutaanza kuziona tu siku si nyingi.
   
 5. P

  Popompo JF-Expert Member

  #5
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33

  mkuu natamani kukugongea thenkx ila sioni ni wapi.umeongea vizuri sana
   
 6. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #6
  Jan 24, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Just thank you is enough, na hii ni moja ya ugonjwa wa wabunge wetu wengi kujali chama kuliko hoja halisi.
   
Loading...