Upigaji wa honi za Magari wakati wa kuingia Majumbani

Mkuu umechanja?
Jamani tunapangiana hata namna ya kufunguliwa geti majumbani mwetu?
Tozo tumekubali sasa hadi honi nisipige getini kwangu?
 
Wengine kwenye magari yao kuna kua na kiasi kikubwa cha pesa ,haswa wafanyabiashara wa kariakoo,hautakiwi kuremba get,ni mwendo wa honi chap ufunguliwe
 
Habari Wakuu!

Kuna hii tabia ya Watu wanaoishi katika Nyumba zenye mageti, pindi wanapokuwa wanarudi majumbani mwao kuanza kupiga honi (wakati mwingine mfululizo) ili wafunguliwe mageti, hasa hizi nyumba ambazo mageti yake hufunguliwa na Mmojawapo wa mwanafamilia na sio Mlinzi.

Hivi kuna ulazima huo kama humo ndani unapotaka kuingia ni kwako na karibia watu wote wa humo ndani una namba zao za simu? Kuna tatizo lolote ukimpgia simu mmojawao ukiwa nje umesimama au umekaribia kabisa getini kuwa akufungulie?

Ki usalama pia hii nadhani haijakaa vizuri, watu wanaweza kujua umerudi au bado kwa kusikilizia honi zako tu, mana mlio wa honi unaenda mbali kidogo.

Pia ni usumbufu hata kwa majirani hasa nyakati za usiku, kwa maoni yangu upigaji wa simu ni bora zaidi Kuliko ufunguliwe geti kwa kupiga honi.

Naomba kuwakilisha.
uko sahihi sana, kwenye jambo la ulinzi umesema kweli kabisa.
Na ili elimu hii iweze kupita na kupokelewa vizuri ni lazima matukio kadhaa yatokee watu wapigwe vitasa akili zikae sawa. kwa wale wazee wa fursa, wakati ni huu huu wa kuonyesha uzalendo
 
na huwa wanahasira hao wajinga hasa mwanafamilia anapochelewa kufungua geti.

Afu msiwe mnakuwa na hasira za kijinga kwa watu wanaobaki nyumbani,na wao ni wa muhimu
 
Habari Wakuu!

Kuna hii tabia ya Watu wanaoishi katika Nyumba zenye mageti, pindi wanapokuwa wanarudi majumbani mwao kuanza kupiga honi (wakati mwingine mfululizo) ili wafunguliwe mageti, hasa hizi nyumba ambazo mageti yake hufunguliwa na Mmojawapo wa mwanafamilia na sio Mlinzi.

Hivi kuna ulazima huo kama humo ndani unapotaka kuingia ni kwako na karibia watu wote wa humo ndani una namba zao za simu? Kuna tatizo lolote ukimpgia simu mmojawao ukiwa nje umesimama au umekaribia kabisa getini kuwa akufungulie?

Ki usalama pia hii nadhani haijakaa vizuri, watu wanaweza kujua umerudi au bado kwa kusikilizia honi zako tu, mana mlio wa honi unaenda mbali kidogo.

Pia ni usumbufu hata kwa majirani hasa nyakati za usiku, kwa maoni yangu upigaji wa simu ni bora zaidi Kuliko ufunguliwe geti kwa kupiga honi.

Naomba kuwakilisha.
Kweli kabisaa wengine wanazidisha mnoo,hii ni kero kubwaa😏
 
Back
Top Bottom