Upi ni uamuzi sahihi wa kufanywa na abiria pindi gari (hususan daladala) inapoanza kurudi nyuma baada ya kushindwa kupanda mlima? Yaliwahi kukukuta?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu Watanzania;

Upi ni uamuzi sahihi wa kufanywa na abiria pindi gari (hususan daladala) inapoanza kurudi nyuma baada ya kushindwa kupanda mlima?

download (2).jpg

Je, ulishawahi kujikuta katika hali hii na ulifanya nini?

Nimeamua kuomba ushauri hapa kwa maana kwamba siku ya tarehe 13 October 2020, ambapo mvua kubwa sana ilinyesha sana, nilipokuwa ninatoka Kitunda huku Dar sasa ninarudi Kivule nikiwa katika bodaboda maeneo ya sehemu moja wanaitwa kwa Mwailafu nilishihudia gari ya abiria almaarufu kama daladala ikirudi "reverse" baada ya kushindwa kupamba mlima mdogo kutokana na udongo wake kuwa unatereza kwa kiingereza wanasema "treacherous"

Katika harakati za kutaka kuokoa maisha yao kuna abiria wawili ambao ni wakaka wao wakaruka nje lakini abiria wengine wote wakabaki ndani ya daladala ile huku wakipiga mayowe wasijue nini la kufanya.

Mungu si Athumani, dereva wa ile gari alikuwa jasiri na shupavu alifanikiwa kuigonesha ile gari pembezoni mwa ukingo wa barabara hivyo kuzuia gari ile isiingie katika daraja kubwa ambalo bado linaendelea na ujenzi.

NB: Picha hapo juu haina uhusiano wowote na hicho kisa nilichosimulia.

Kuna baadhi ya watu wanadai kuruka wakati daladala/gari ime-fail brake mlimani sio uamuzi sahihi ila kuna baadhi wanadai kuwa ndio jambo jema la kufanya wakati wa janga la namna ile

Upi ni uamuzi sahihi wa kufanywa na abiria? Je, ulishawahi kujikuta katika hali hii na ulifanya nini?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Tatizo ni abiria kupanic ,suala la kuruka siyo rafiki sana ila inategemea na mwendo kama liko slow its fine but kama liko speed sana ni changamoto ,kuna jamaa aliruka but kilichotokea ni kwamba yeye pekeyake ndiye alifariki
Duh!!
 
Tatizo ni abiria kupanic ,suala la kuruka siyo rafiki sana ila inategemea na mwendo kama liko slow its fine but kama liko speed sana ni changamoto ,kuna jamaa aliruka but kilichotokea ni kwamba yeye pekeyake ndiye alifariki
Hapo ni kutulia tu... .kuna vitu vingine vimepangwa toka siku unazaliwa. Mungu ndiye jaji hapo
 
Upi ni uamuzi sahihi ili abiria aokoe maisha yake, wewe kama mtaalam wa masuala ya usalama barabarani acha kutoa majibu ambayo yapo too general...
Hiyo ni ajali, kwenye ajali hakuna jibu la moja kwa moja, zaidi inategemea mazingira ya ajali.
Kama dereva angeweza angalau kulizuia, Yaani lisimame na kutokurudi nyuma, pengine ingekuwa salama kwa abiria wote kutoka.
Tukio hili, walioruka walipona, nina mfano ambapo kulitokea ajali aliyeruka ni mmoja tu na ilitokea ndio namfahamu, na yeye pekee ndie aliyepoteza maisha kwa kiangukiwa na basi.
 
Back
Top Bottom