Upi Mustakabali wa ACT-Wazalendo Kwenye Siasa za Upinzani Tanzania?

Una ufahamu mdogo wa mambo ya siasa. Hayo makundi uliyotaja leo hii vyama vya siasa vilivyopo ukiachia ccm, vikijaribu kuonyesha ukaribu tu na makundi hayo, utasikia yanajihusisha na siasa. Yaani ni makosa hayo makundi kuonyesha mahusiano yoyote na chama cha siasa cha upinzani, na yanaweza kukutana na hujuma za wazi dhidi ya ccm kupitia taasisi za kimamlaka, na mifano ipo wazi.

Tuje kwa Nyerere ambaye ni mfano wako. Nyerere alikuwa na mahusiano na hiyo Govenor Turnbull sio kwa sababu Huyo gavana alitaka, bali Tanganyika haikuwa koloni la Uingereza, ila ilikabidhiwa kwa Uingereza na Umoja wa mataifa, mpaka tutakapokuwa tayari kujitawala yenyewe. Nyerere ndio aliyekuwa na chuki ya wazi dhidi ya mfumo wa vyama vingi ili aburuze watu kwa mtazamo wake. Na kwa taarifa yako Nyerere ndio muasisi wa viongozi kukaa madarakani wapendavyo, na hakuna mwenyekiti yoyote wa chama cha siasa aliyejimilikisha chama cha siasa muda mrefu kama yeye. Alikuwa mwenyekiti wa TANU na Ccm zaidi ya 20yrs,na kama sio sera zake kuingiza nchi hii kwenye umasikini mkubwa, asingetoka madarakani kwenye ccm na urais.
Ndugu yangu unasumbuliwa na tatizo la kujiona unajua kila kitu. Ukifanikiwa ku deal na hilo tatizo perpendicularly utakuwa umefanikiwa pakuwa sana maishani.
Punguza u much know
 
Ndugu yangu unasumbuliwa na tatizo la kujiona unajua kila kitu. Ukifanikiwa ku deal na hilo tatizo perpendicularly utakuwa umefanikiwa pakuwa sana maishani.
Punguza u much know

Nakubaliana na ushauri wako, sasa nataka kujua, unamsaidia niliyemquote au umechukizwa na nilichomjibu huyo boss? Fuatilia anachojibu na ninachomjibu, kisha huo ushauri wako ili unitendee haki uelekeze kwake pia.
 
Tuachane na huyo Mkarura sijui nani.

Nakukumbusha tu, kuna wakati hata wewe uliwahi kusema Mh Mbowe anatakiwa kupumzika ili kupisha damu mpya ya uongozi, je bado unaamini Mbowe anapaswa kupumzika au hadi afikishe miaka 20 kama Nyerere ?
 
Wala sibahitishi kwenye hilo na msimamo wangu uko wazi peupe kwenye hilo. Acha huyo Mbowe tu, mimi sio muumini wa kiongozi yoyote wa kuchaguliwa kukaa madarakani zaidi ya miaka 10. Pitia post zangu toka Mbowe akae madarakani zaidi ya miaka 10, kama kuna popote nilipowahi kuunga mkono huo uhuni wake.
 
Tupo pamoja kwenye hilo. Tunachofeli wabongo kwa kiasi kikubwa ni kukosa utii wa sheria tulizotunga.
 
ifahamike Zito anajiona ni superior kuliko Mbowe,
Na hili ndio linamtesa mpaka leo..... kujenga chama nchi nzima sio jambo dogo. Aliwahi mkejeli kivp mkoa anaotoka ina mbunge mmoja tu wakati yeye Zitto "Alisaidia" wabunge zaidi ya 5 upinzani kuukamata Kigoma.

Matarajio ya zitto ilikua 2020 CHADEMA wangekosa viti vyote ila wao kule zanzibar wangetangazwa hivyo wangekuwa KUB...na possibly Lissu angekatwa so Membe angekua powerhouse ya upinzani ili kuongeza viti maalum.

Kama ulivyosema JPM hakutegemea politics kuimaliza CHADEMA hivyo mwisho wa siku tukakosa wote. Sadly enough Maalim naye akatangulia Mbele za haki so kuelekea 2025 zitto ana mtihani haswa otherwise I wisha angebaki CHADEMA I'm sure by now angekua Mwenyekiti.

Ajifunze kwa Mnyika.... Unyenyekevu una faida zake.
 
Kabisa mkuu,Zito aliamini ana ushawishi na uwezo wa kujenga Chama kikubwa kuliko cdm. Nadhani hakujua kuna matamanio na uhalisia. Kwa sasa ndio anajifunza kwa vitendo mambo haya. Hapo alipo yuko kwenye wakati mgumu na hajui ashike lipi, maana akirejea cdm atakuwa amempa Mbowe heshima ambayo hayuko tayari, akienda ccm anajua watu watamdharau japo atapata cheo. As how it stands sioni akiinyanyua ACT huku Bara, na hao Wapemba ndio watakaokuwa na sauti kwenye chama, na yeye atabaki ceremonial leader.
 
Na hili ndio linamtesa mpaka leo..... kujenga chama nchi nzima sio jambo dogo. Aliwahi mkejeli kivp mkoa anaotoka ina mbunge mmoja tu wakati yeye Zitto "Alisaidia" wabunge zaidi ya 5 upinzani kuukamata Kigoma.

Matarajio ya zitto ilikua 2020 CHADEMA wangekosa viti vyote ila wao kule zanzibar wangetangazwa hivyo wangekuwa KUB...na possibly Lissu angekatwa so Membe angekua powerhouse ya upinzani ili kuongeza viti maalum.

Kama ulivyosema JPM hakutegemea politics kuimaliza CHADEMA hivyo mwisho wa siku tukakosa wote. Sadly enough Maalim naye akatangulia Mbele za haki so kuelekea 2025 zitto ana mtihani haswa otherwise I wisha angebaki CHADEMA I'm sure by now angekua Mwenyekiti.

Ajifunze kwa Mnyika.... Unyenyekevu una faida zake.
Zitto kinachomtesa ni tamaa
 
ACT ni Zito Kabwe, na chama hiki ni matunda ya msuguano wa Zito dhidi ya chama chake cdm, kutokana na kutumiwa na ccm. Chama hiki kilikuwa na mkono wa kundi la JK, akiwemo Membe, Mwigulu, January, Nape nk, lengo la kuanzishwa chama hiki ilikuwa kiwe back up ya kuilinda ccm dhidi ya cdm. Fedha na mikakati yote ya chama hiki alipewa Zito na hilo kundi la JK. Rejea uchaguzi wa 2015 ACT iliweza kusimamisha wagombea karibu nchi nzima, huku kukiwa kichanga kabisa bila support kubwa ya watu.

Uchaguzi wa 2015 ndio ulimaliza kabisa mipango ya ACT baada ya Magufuli kuwa rais. Magufuli alipoingia madarakani alitupilia mbali mipango, mienendo na kundi lote la JK, ikiwemo support kwa ACT. Hili lilikuwa pigo kubwa sana kwa ACT kwani ilitegemea zaidi support ya ccm kufanya siasa za upinzani, kwa lengo la kuhakikisha ccm haizidiwi na cdm. Lakini Magufuli aliweza kutumia madaraka vibaya kuihujumu cdm kuliko kutumia mbinu za kisiasa kupambana na cdm, hivyo hakuwa na uhitaji wa hiyo ACT hasa ukizingatia Magufuli hakutaka mambo ya JK kabisa na kundi lake.

Hali hii ilimfanya Zito awe mkosoaji mkubwa wa Magufuli, kwani ni kama aliharibu matarajio yote ya kuikuza ACT, ifahamike Zito anajiona ni superior kuliko Mbowe, hivyo alitarajia kumkomoa Mbowe iwapo ACT ingefanikiwa kuwa mbadala wa CDM kwenye siasa za upinzani, hasa huku Bara. Ni bahati tu uchaguzi wa 2020 ACT ilifaidika na mgogoro wa CUF baada ya Maalim Seif kuondoka na wafuasi wake na kutua ACT. Lakini bahati hiyo inaifanya ACT kuwa na nguvu huko Zanzibar hasa Pemba, bali sio kwa ushawishi wa Zito.

Kwa sasa Zito ana kazi ya kuijenga ACT huku Bara, hivyo hana namna zaidi ya kutumia ushawishi wa JK kwa mama Samia, ili warudishwe kwenye upinzani unaotakiwa na ccm. Hivyo Zito anawajibika kwenda kwa tahadhari ili kumrahisishia JK kumshawishi mama Samia awabebe ACT, tatizo ni moja kwenye mazingira haya, mama Samia urais na uenyekiti wake wa ccm ni wa kurithi, na hasa ukizingatia ni Mzanzibari anajikuta hana nguvu ya maamuzi hayo. Hata ushiriki wa Zito kwenye hizi chaguzi za marudio, ni kujaribu kusaka huruma ya rais Samia kwa chama chake, lakini matokeo ya uchaguzi aliyoyapata kwenye chaguzi alizojichanganya kushiriki huku Bara, zimeishia kumfubaza kisiasa. Kwa sasa Zito yuko njia panda, na iwapo uchaguzi ujao kama hakutakuwa na mabadiliko ya kisiasa yatakayofadisha chama chake, namuona Zito kwa aibu akirudi Cdm, au aamue kukata mzizi wa fitina kwa kujiunga na ccm mshirika wake wa muda mrefu kwa kificho, ili akajaribu bahati yake. Sioni Zito akiendelea kuvumilia kuishi bila hata ya kuwa waziri, kwani anajiamini kutokana na elimu yake na huku umri wake ukienda.

Cc: Zito, Act Wazalendo, bams, Paskali Mayalla, Salary slip, sky eclat, Kiranga, joka kuu, mag3, nguruvi3
Miaka inaanza mpaka inakatika, unaandika milundo ya maandishi takataka kabisa
 
Back
Top Bottom