Upi mkoa bora kuanza maisha?

Kama uko radhi kurisk kuzunguka mkoa mwingine na laki moja si utafute odds 10 halafu weka laki yote.
 
Nakushauri nenda MBEYA wilaya ya RUNGWE au KYELA huko hautojutia mkuu... kuna maeneo makubwa sana ya kilimo. Huwezi kosa chochote kule trust me. Cha kuzingatia ni uwe mpambanaji wa kweli na roho ngumu ya kitafutaji kweli. Hapo utatoboa tu. Nawasilisha.
 
Hujaitaja Dar kwanini? Nenda kwanza Dar es Salaam upite tuition ya mwaka mmoja ndio ufikirie mambo mengine
dar hamna lolote acha kumpoteza mwenzio...watu wengi wanaishi dar wakiwa na matumaini makubwa ya kufanikiwa lakini mwisho wa siku wanazeeka wakiwa hawana kitu.....watu wamezeeka halafu bado wanajiita wasela
 
Msigombane,,,,, mwambieni aende mbeya hasa maeneo ya uyole au mbalizi atatoboa
Hela aliyo nayo haitoshi hata nauli na malazi ya siku mbili maana huyu lazima awe chokoraa kwa kulala zaidi ya mwezi mitaani. Na kwa baridi ya Mbeya sasa hivi ukilala nje siku mbili UNAKUFA
 
Mtoa mada hauna nia ya dhati katika hili, usikalili watu wanakupa mawazo tofauti na ya kwako we unaleta UJUAJI. Kama ulisoma shule ya msingi kumbuka kuna maswali ya kuchagua ambayo jibu lake sahihi huwa si miongoni mwa machaguo uliyopewa na mtoa swali.
 
Back
Top Bottom