tatum
JF-Expert Member
- Jan 16, 2018
- 5,786
- 4,490
Wiki kama mbili hivi kumekuwa na malumbano na mijadala mingi sana katika vyombo vya habari vya hapa Tanzania kuanzia kwenye tv,redio na mitandao ya kijamii kuhusu ziara ya Mhe Tundu Lissu huko Ulaya na Marekani akiwa anajaribu kueleza yale anayopna yeye kuwa ni mapungufu ya Serikali ya awamu ya tano katika utawala wake.
Baada ya mijadala na mahojiano yake huko majuu na kushikiliwa bango na watz wenye msimamo kama Tundu Lissu naona upepo huo sasa umetulia na watu wameanza kufanya kazi zao kama kawaida na kujadili mambo ya msingi sasa ya kuendeleza nchi na watu wake.
Tulijua tu kuwa upepo huu utatulia tu baada ya muda mfupi na ndiyo mara nyingi mambo ya kisiasa yalivyo.
Tusubiri atakapo ibuka tena kwenye kurudi kwake Tanzania kama kweli atarudi na kuitangazia dunia kuwa sasa anarudi Tanzania kama alivyojinasibu huko Marekani kuwa atarudi kwa kishindo kikuu hapa nchini.
Naona kwa maneno yake aliyokuwa anaiaminisha dunia kuwa nchi yetu ikoje huko majuu kiukweli ni ngumu sana kurudi hivi karibuni labda baada ya miaka 20 kuisha au asirudi kabisa.