Upepo wa Tundu Lissu 2020, Utakuwa mkali sana!

uran

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
7,081
10,181
Nimetafakari sana juu ya huyu nguli wa Siasa nchini Tanzania. Sipati picha siku anatua Tz na atangaze nia ya kugombea Urais, Kuna viongozi wakubwa ndani ya CCM watakufa kwa pressure.
Naona kama Watanzania wana hisia kali sana juu ya Tundu Lissu, yupo kwenye Mioyo ya watu wengi.

Amepata kibali, na anakubalika...

CCM watatumia mbinu kubwa sana hili lisitokee moja wapo ikiwa ni kuwavuruga Wanachadema, hata wajaribu kuwahusisha CDM na kushambuliwa kwa Lissu.

Tundu Lissu-ni Tishio kubwa kwa CCM wajiandae kutingishika, wasipojishika vizuri lazima waanguke-(take my word)
 
Nakumbuka kwenye kampeni za uchaguzi Mkuu uliopita Lowasa akiwa juu kisiasa wote tuliamini atashinda, katika mkutano mmoja wapo alisema kama chadema hawatashinda uchaguzi Mkuu ule kupitia yeye basi itabidi wasubiri kwa miaka mingine hamsini! Ngoja tuone itakuwaje
 
Mashabiki wa CHADEMA ni kama huwa hamna akili! Nyie mnadhani URAIS ni kama UENYEKITI wa CHADEMA!
Tundu Lissu hana bado hadhi ya URAIS na hana upepo wowote kwenye nafasi hiyo!
Huo ndo ukweli mchungu ambao hamwezi kuukubali!
Kama Lowasa hakushinda kupitia chadema Lisu ataweza kweli? Kwamba Lisu ana nguvu na anakubalika kiasi hicho? Kwamba Lisu atapigiwa deki barabara kwa omo kama Lowasa? Ngoja tuone!
 
Kuna ukweli mchungu.
Kitendo cha Tundu kujichimbia majuu kitakuwa na madhara kama ya Lowassa kuchelewa kujiunga Chadema baada ya kukatwa Ccm hadi wafuasi wake wengi wakakuta nafasi za Ubunge Chadema zishateuliwa na kujaa.
Tundu Lissu hatafikisha nusu ya mtikiso wa Lyatonga kwa Mkapa
 
Tundu Lissu hawezi kumfikia hata Lowassa achilia mbali Augustino Mrema na Dkt. Slaa.

Mrema na Dkt. Slaa walipata umaarufu katika kipindi ambacho wananchi wengi waliamini kuwa nchi inanuka rushwa na ufisadi ambao ulikuwa unagusa maisha ya chini kabisa ya wananchi. Hakuna wakati ambao watawala wanaogopa kama watu wa kipato cha chini kabisa wanapoamua kupambana na utawala.

Utawala wa sasa umejenga imani kwa watu wa kipato cha chini na masikini ambao wanaamini matatizo yao yanafanyiwa kazi au yatafanyiwa kazi. Kujenga Imani kwa wananchi wengi ni nguzo na silaha mathubuti kwa wanasiasa.

Tundu Lissu atapata uungwaji mkono kutoka kwa baadhi ya wananchi wenye kipato cha kati na juu na manazi wa CHADEMA kwa sababu utawala huu umehakikisha kipato chao kisichofuata sheria na utaratibu kimedhibitiwa.

Nadhani kelele za ''elitist'' na wanazi wa CHADEMA kwenye mitandao ya kijamii zinakufanya udhani Lissu anakubalika kwa kiwango kikubwa nchini! NOPE!

Ogopa sana watawala wanaoitwa ''populist leaders'' katika wakati ambao wananchi wengi masikini wamejenga imani nao.

Mrema na Dkt. Slaa walikuwa ''populist leaders'' kama ilivyo kwa Rais Magufuli kwa sasa.

Katika Uchaguzi ambao present incumbent haitakuwa na shida ni katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Watu wenye akili pana na maono kwa sasa hawaongelei Uchaguzi wa 2020 kwa sababu mshindi anajulikana labda litokee jambo ambalo liko nje ya uwezo wa kibinadamu. Ndio maana unasikia wanaongelea suala la kubadilisha katiba au la kwa sababu wanajua mwaka 2020 atashinda Uchaguzi Mkuu!
 
Mashabiki wa CHADEMA ni kama huwa hamna akili! Nyie mnadhani URAIS ni kama UENYEKITI wa CHADEMA!
Tundu Lissu hana bado hadhi ya URAIS na hana upepo wowote kwenye nafasi hiyo!
Huo ndo ukweli mchungu ambao hamwezi kuukubali!

Kama Magufuli na JK wameweza kuwa marais wa Tanzania nani atashindwa? Mtu yoyote mwenye akili timamu anaweza kuwa rais wa Tanzania, kubali kataa lakini habari ndio hiyo.
 
Anaweza
Anaweza
Anaweza..
Kama hawaamini waruhusu siasa ziendelee Kama kawaida,waache tuwe na tumeb huru ya uchaguzi ,wakurugenzi wa halmashauri ambao ni wasimamizi wa ndani ya halmashauri wasiteuliwe na Rais waone
Jioni haifiki watajuta balaa
 
Hujui unaloongea au unajaribu kupotosha. 2015 Wananchi wengi walijiandikisha kwa hasira wakiamini Lowassa atakuwa mgombea wa ccm. Wakati huo kitambulisho kilipewa jina ya kichinjio ili kumkata Lowassa. Miezi miwili cdm wakafanya kosa la kipuuzi la kumchukua Lowassa, kwenye uchaguzi mkuu mtu huyo mchafu akapata kura 6m+. Sasa kama mtu aliweza kupata kura 6m+ huku miezi miwili kabla ya uchaguzi hao waliompigia walikuwa wanamchukia, tena alifanya kampeni akiwa mgonjwa, hapo kuna wapiga Kura wa kusema watampa kura Magufuli?

Kwa uwezo wa ushawishi wa Tundu Lissu na uwezo mdogo kwa ushawishi wa Magufuli, ni bora Magufuli aendelee kutumia madaraka yake kunajisi box la kura kama hataki kupata msongo wa mawazo. Hiyo mbinu ya viongozi wastaafu kumcha huu ya rais bora Magufuli aendelee kuishikilia maana ndio salama ya ccm.
 
Kwangu jiwe hana mvuto wowote ninapomsikiliza natamani hata kufaaaa kiukwel lisu ni kiumbe wa ajabu kuwahi kutokea dunian mm ninamkubali sana!
 
39 Reactions
Reply
Back
Top Bottom