Upepo wa Tundu Lissu 2020, Utakuwa mkali sana!

Mashabiki wa CHADEMA ni kama huwa hamna akili! Nyie mnadhani URAIS ni kama UENYEKITI wa CHADEMA!
Tundu Lissu hana bado hadhi ya URAIS na hana upepo wowote kwenye nafasi hiyo!
Huo ndo ukweli mchungu ambao hamwezi kuukubali!
Mkuu Kama Magufuli ameweza kutuongoza kwa miaka mitano ni mtanzania gani meingine anaweza akashindwa?
 
Kama Lowasa hakushinda kupitia chadema Lisu ataweza kweli? Kwamba Lisu ana nguvu na anakubalika kiasi hicho? Kwamba Lisu atapigiwa deki barabara kwa omo kama Lowasa? Ngoja tuone!
Mkuu wewe upo mbali sana,Ila Magufuli anajua kura alizopata,wewe unadhani kule kujigamba kuwa yeye ndo rais ilikuwa kwa bahati mbaya?
 
Tundu Lissu hawezi kumfikia hata Lowassa achilia mbali Augustino Mrema na Dkt. Slaa.

Mrema na Dkt. Slaa walipata umaarufu katika kipindi ambacho wananchi wengi waliamini kuwa nchi inanuka rushwa na ufisadi ambao ulikuwa unagusa maisha ya chini kabisa ya wananchi. Hakuna wakati ambao watawala wanaogopa kama watu wa kipato cha chini kabisa wanapoamua kupambana na utawala.

Utawala wa sasa umejenga imani kwa watu wa kipato cha chini na masikini ambao wanaamini matatizo yao yanafanyiwa kazi au yatafanyiwa kazi. Kujenga Imani kwa wananchi wengi ni nguzo na silaha mathubuti kwa wanasiasa.

Tundu Lissu atapata uungwaji mkono kutoka kwa baadhi ya wananchi wenye kipato cha kati na juu na manazi wa CHADEMA kwa sababu utawala huu umehakikisha kipato chao kisichofuata sheria na utaratibu kimedhibitiwa.

Nadhani kelele za ''elitist'' na wanazi wa CHADEMA kwenye mitandao ya kijamii zinakufanya udhani Lissu anakubalika kwa kiwango kikubwa nchini! NOPE!

Ogopa sana watawala wanaoitwa ''populist leaders'' katika wakati ambao wananchi wengi masikini wamejenga imani nao.

Mrema na Dkt. Slaa walikuwa ''populist leaders'' kama ilivyo kwa Rais Magufuli kwa sasa.

Katika Uchaguzi ambao present incumbent haitakuwa na shida ni katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Watu wenye akili pana na maono kwa sasa hawaongelei Uchaguzi wa 2020 kwa sababu mshindi anajulikana labda litokee jambo ambalo liko nje ya uwezo wa kibinadamu. Ndio maana unasikia wanaongelea suala la kubadilisha katiba au la kwa sababu wanajua mwaka 2020 atashinda Uchaguzi Mkuu!
Mkuu umenitoa machozi kwakweli...yaani Taifa ili liendelee kua chini ya umwagaji ,ukiukaji wa katiba,visasi,umaskini kabisa. Hivi hao watu wa chini wanaishi Mars au Venus..MAANA kadri unavyosema basi utadhani labda hao watu wa chini SWAPO apa nchini. Hivi umeona ugumu gani kutaja ata ayo manufaa.
 
Bado mimi siamini kwenye chaguzi hizi zinazofanyika bila tume huru ya uchaguzi, naamini kabisa upinzani juu ya kasoro ndogo ndogo walizonazo lakini huwa wanashinda. Sehem kubwa ya ushindi wa Ccm unategemea vyombo vya ulinzi pamoja na mkurugenzi wa tume ya uchaguzi. That is the fact. Kuhalalisha ushindi wa ccm kwenye chaguzi hizi ni kuhalalisha dhuluma kwa kiwango cha standard gauge.
 
Nimetafakari sana juu ya huyu nguli wa Siasa nchini Tanzania. Sipati picha siku anatua Tz na atangaze nia ya kugombea Urais, Kuna viongozi wakubwa ndani ya CCM watakufa kwa pressure.
Naona kama Watanzania wana hisia kali sana juu ya Tundu Lissu, yupo kwenye Mioyo ya watu wengi.

Amepata kibali, na anakubalika...

CCM watatumia mbinu kubwa sana hili lisitokee moja wapo ikiwa ni kuwavuruga Wanachadema, hata wajaribu kuwahusisha CDM na kushambuliwa kwa Lissu.

Tundu Lissu-ni Tishio kubwa kwa CCM wajiandae kutingishika, wasipojishika vizuri lazima waanguke-(take my word)
Membe imekuwaje tena, Lissu hawezi teuliwa kupeperusha bendera ya chadema urais 2020, watampa Membe
 
Nimetafakari sana juu ya huyu nguli wa Siasa nchini Tanzania. Sipati picha siku anatua Tz na atangaze nia ya kugombea Urais, Kuna viongozi wakubwa ndani ya CCM watakufa kwa pressure.
Naona kama Watanzania wana hisia kali sana juu ya Tundu Lissu, yupo kwenye Mioyo ya watu wengi.

Amepata kibali, na anakubalika...

CCM watatumia mbinu kubwa sana hili lisitokee moja wapo ikiwa ni kuwavuruga Wanachadema, hata wajaribu kuwahusisha CDM na kushambuliwa kwa Lissu.

Tundu Lissu-ni Tishio kubwa kwa CCM wajiandae kutingishika, wasipojishika vizuri lazima waanguke-(take my word)
Naona Membe ameyeyuka sasa ni Tundu Lisu, sawa.
JPM Mwisho wa Reli, Bendera Chuma, Kamba chuma na Chuma ni Chuma.
 
Lissu ni zaidi ya Lowassa...hana makandokando huitaji omo kumsafisha...alafu ni RC
 
Back
Top Bottom