Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 93,481
- 119,320
Kama wengine tulivyotabiri, mambo ya habari za Paul Makonda na vyeti vyake sasa yanaelekea kuishia hewani! Yanaelekea kupita tu kama upepo.
Kutabiri hilo wala hakukuwa na ugumu wowote ule. Huhitaji akili za spesho skuli wala uprofesa wa UDSM kuweza kutabiri mengi yatayojiri nchi hii. Hata akili za ubeba maboksi zinatosha kabisa.
Vyeti vya Makonda si ishu tena. Yaani si ishu kivile. Watu washaanza kusahau kidogo kidogo. Na muda si mrefu toka sasa watu watasahau kabisa. Si suala la 'kama' tena bali ni suala la 'lini'. Na hiyo 'lini' ndo muda si mrefu toka sasa.
Mahasimu wake waliokuwa wamemshikia bango kila kukicha, soda yao imeisha gesi. Pepsi imekuwa kama maji na Coca imekuwa kama maziwa ya Tanga Fresh.
Hata yule askofu...yule prima donna...naye naona wiki hii...au niseme kesho...hana la kumpatia tena kiki.
Nyimbo za Bashite zishaisha utamu. Baada ya kudai kuwa ana vyeti vya Bashite ofisini kwake na baada ya kumwambia atuonyeshe hivyo vyeti, siku moja akaibuka na kikaratasi cha hovyo hovyo alichodai eti ndo matokeo ya Makonda. Na nyumbu kama kawaida yao wakamwamini.
Hata humu JF napo naona sasa watu washachoka na habari za Makonda. Ndo maana hata nyuzi za kumhusu si nyingi kama ilivokuwa.
Lakini binafsi bado naamini kuwa rais atampangia Makonda majukumu mengine na kumtoa katika ukuu wa mkoa wa Dar.
Ila nitoe tu pongezi za kipekee sana kwa mwanamke wa shoka, mwanamke hodari dahari, asiyebabaishwa wala kutetereka, anayesimamia mpaka mwisho kile anachokiamini. Mwanamke ambaye ananikumbusha mwanamke mwingine wa shoka aliyekuwepo humu miaka mingi iliyopita [Mwafrika wa Kike], si mwingine bali ni bibie cocochanel
cocochanel nimekuvulia kofia na nakupigia saluti. Sasa ni rasmi...nakukubali sana. Na ikitokea mimi na wewe tukawepo sehemu moja basi wewe lete bill yako na Ngabu ata take care of it. You rock lady!! You rock big time.