MAFILILI
JF-Expert Member
- Apr 28, 2011
- 2,377
- 1,194
Mkutano mkuu wa CCM ulioisha hivi karibuni, Kizota, Dodoma umebadili mwelekeo wa siasa za Bongo huku CHADEMA wakizidi kuweweseka na kupoteza fursa ya kuvutia watanzania makini. Safu mpya ya uongozi ndani ya Sekretaeti ya CCM imerudisha matumaini kwa kasi kubwa miongoni mwa wananchi hivyo wamefikia muafaka kurejea katika mstari na kurudi CCM baada ya kuvunjika moyo na siasa za maji taka ndani ya CHADEMA. Kudhihirisha hayo nisemayo, wiki iliyopita Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dr. Slaa aliifanya ziara aliyoita ya kuimarisha chama mkoani DSM, matokeo yake amezidi kuporomosha CHADEMA katika mkoa husika.
Dalili chache za chama kuporomoka ni hizi:-
1. Mikutano ya Kigamboni ilikosa viongozi wa wilaya hivyo kuishia kwenda kuongea na wavuvi feri
2. Wilayani Kinondoni pamoja ni kuwa yalipo makao makuu ya Chama yalipo; kikao kilichelewa kuanza hadi wajumbe ilibidi wafuatwe majumbani kwao kwa kutumia bodaboda
3. Wafuasi wa Mdee kutoka jimboni Kawe hawakufurahishwa na kitendo cha Dr. Slaa kuponda utendaji wa mbunge wa Kawe huku katika pazia akiweka mazingira ya mchumba wake, Josephine amrithi Mdee 2015 kugombea jimbo la Kawe kwa tiketi ya CHADEMA.
CHADEMA kaeni chini mtafakari namna ya kujikomboa kisiasa, 2014 inakaribia msije mkapata kipigo mkashindwa kujenga hoja kwa wafadhili wenu kwa ajili ya uchaguzi mkuu 2015