MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,172
- 23,974
Siasa za Tanzania ni za aina yake ambazo zinaweza kukupa matumaini ambayo hayapo kama huzijui vizuri. Siasa za Tanzania ni kama upepo unaopita ambao hauna madhara yoyote kwa wanaozijua vizuri siasa za Tanzania!
Baada ya Uchaguzi Mkuu 2020, hoja zilizojaa kwenye mitandao ya kijamii kwa wiki tatu zilikuwa ni Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) na Rais Magufuli!
Wasiozijua vizuri siasa za Tanzania wakaambiwa wakusanye vielelezo na vidhibiti ili wahalifu nchini wakashitakiwe kwenye mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC). Wasiozijua vizuri siasa nchini wakakusanya na kukabidhi ''vielelezo'' na ''vidhibiti'' kwa waliowaagiza!
Watanzania tukaaambiwa ''tukae mkao wa kula'' kwa sababu ''vielelezo'' na ''vidhibiti'' vimewasilishwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC). Maelezo haya yaliwafanya wasiozijua vizuri siasa za Tanzania kuanza kushangilia huku wengine wakitumaini wako mbioni kushuhudia Uchaguzi Mkuu mwingine kwa sababu watawala wa sasa wakiongozwa na Rais Magufuli wanapelekwa gerezani, Uholanzi!
Wanaozijua siasa za Tanzania vizuri wakasema, hizi ni porojo za kisiasa za kipoza uongo (political placebo) ambazo baada ya muda ukweli utazisambaratisha!
Kwa sasa huwezi kusikia tena suala la Rais Magufuli kupelekwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) likijadiliwa na wale waliolianzisha kwenye mitandao ya kijamii! Wanajua UPEPO UMEPITA!
Hata yule aliyekuwa anajiita ''Mwanasheria'' wa Tundu Lissu, Robert Amsterdam huwezi kumsikia tena akipiga kelele kuhusu Rais Magufuli na ICC! UPEPO UMEPITA! Nasikia amehamia kwenye siasa za Uganda!
Upepo uliopo kwa sasa ni upepo wa Halima Mdee na wenzake! Hata huu upepo baada ya muda utapita bila kuleta madhara yoyote kwa wale wanaozijua vizuri siasa nchini! Hata Halima Mdee wakati akiongea na vyombo vya habari alisema huu ni upepo tu ''usio na madhara'' ambao utapita!
Walewale waliokuwa mstari wa mbele kwenye upepo wa Rais Magufuli na ICC kwa sasa tena wamekuwa mstari wa mbele kwenye upepo wa Halima Mdee na wenzake!
Baada ya huu upepo wa Halima Mdee na wenzake kupita, wabunge wa viti maalum wa CHADEMA wataenda bungeni na CHADEMA wataendelea kupokea ruzuku zitokanazo na Uchaguzi Mkuu ambao viongozi wa CHADEMA wanatuambia ''hawautambui''!
ACT-Wazalendo pia watajiunga na serikali ya mapinduzi Zanzibar AKA SUK kuunda serikali na maisha yataendelea!
Hii ndio Tanzania ambayo kama huzijui vizuri siasa zake unaweza kujipa matumaini ambayo kiuhalisia hayapo bali unachohangaika nacho ni siasa za kipoza uongo (political placebo)!