Michuzi katika bandiko muhimu leo kwenye blog yake, amesema kumekuwepo na upungufu mkubwa wa picha zinazoingia kwenye mtiririko wa blog yake kila siku kutokana na vyama vya siasa kutopeleka picha na habari. Amesema wahusika na propaganda vyamani hawapeleki habari, na hivyo anawaasa wapeleke habari na picha kutangaza sera za vyama vyao for free.
Ninachojiuliza, kwa nini walisitisha kupeleka habari huko isipokuwa CCM?
Kuna blog nyingi tu kama Mjengwa, na wengine wana habari nyingi tu za vyama vya siasa, wahusika hupeleka au timu ya bloggers ndiyo inayohaha kupata habari hizo kupamba blog zao?