Upepo kwa CHADEMA utabadilika endapo watafanya yafutayo:-

Zee la kitaa

JF-Expert Member
Oct 25, 2017
403
211
CDM ni chama kikuu cha upinzania Tanzania, kimefika hapo kwa ajenda za msingi za kutetea maslahi ya taifa hili na kupigania rasilimali za taifa hili. Hoja kubwa iliyo kipandisha chadema hadi kuwa chama kikuu cha upinzani ni kupambana na rushwa ambayo ilikuwa imetamaraki katika maeneo mbalimbali. Katika kipindi cha awamu ya tano ya uongozi mambo mengi ambayo yalikuwa yanapingwa na wapinzania; Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri wa Muungano ameweka nguvu na jitihada zakutosha kupambana nayo, hivyo wapinzani kuanza kumwambia anatekeleza ilani yao, mara ni rais wakwake hana chama, na maneno mengi. Upepo ukabadilika na kuanza kumwita mara dikiteta mchwara na maneno mengine. Hivi ajenda kuu za chadema sikuhizi zimekufa ama zilitokana na uzembe wa serikali kusimamia na kupambana na maovu ambayo wananchi walikuwa wakiyapata. Ili CDM irudi katika enzi zake nashauri yafuatayo:-
  • Tengenezeni chama kiwe kama taasisi imara ambayo itakuwa na wasemaji wake na si kila mtu anaropoka kwa niaba ya chama.
  • Imarisheni chama kwa kufungua matawi mengi maeneo karibia na watu, yani mashina katika vijiji.
  • Muwe na transparency katika ruzuku na zitumike kuimarisha chama na maendeleo ya chama
  • Tumieni wasomi wenu kutengeneza sera ambazo zitakidhi matakwa ya wananchi
  • Fanyeni chama chenu kiwe kimbilio kwa watanzania pale haki zao zinapominywa
  • Imarisheni maelewano kati yenu; acheni kusingizina na kurushiana vijembe bali mjenge mahusiano mema.
  • Mikakati yenu ijipambanue kupingana na rushwa, ufisadi, uzembe na kusimamia maliasili za taifa hili
Huu ni ushauri na si ugonvi. Sipendagi matusi ni maoni yangu tu. Naomba kuwasilisha:-
 
Wasimtegemee Mange kama katibu muenezi habari
Wawe na sera imara na endelevu
Wasifanye chama kama SACCOS
Mbowe a.k.a Mugabe aache chama kichague wengin
Acheni kutengeneza matukio ya kuuwa na kusingizia wengine(serikali)
 
Back
Top Bottom