Upeo wa Uwezo wetu kufikiri? - Kwanini suluhisho la tatizo la maji vijijini ni kuchimba visima?

:heh::heh:
Falsafa za wavivu wa pwani wanaoshinda kwenye bao!!, ukizifuata utakwama! Eti mwenda pole hajikwai (badala ya mwenda pole anakawia kufika)
:heh::heh:
Karibu kila kijiji kinaweza kuwa na reservoir tank. Siyo kama nahusisha sana wamarekani, ila jinsi ya kujua kama upo mji gani wakati unaendesha vijijini ni through water reservoirs ambazo nyingine zimejengwa miaka 200 iliyopita!

images


Ila hiyo kitu inahitaji nishati, either umeme au mafuta.. hata solar.
Mtanisamehe wakuu, uwezo tunao na sababu tunazo!.... fedha hatuna.
 
Umesahau hii, mkuu. JOSHUA NASARE kuanza na kuchimba visima. mfuuuuuuuu. Kaz kweli kweli. au wachimbe malambo nini. acha siasa hapa ni jiografia ndiyo inapelekea visima kuwa suluhisho. Huwezi kusambaza mabomba kama chanzo cha maji hakiko karibu na eneo husika. au ulitaka wachimbo malambo? hayo yapo na ni kwa ajili ya mifugo.

Maana ya kutumia mabomba ni nini chanzo cha maji kiwe mbali au karibu? Kwa mantiki yako inawezekana tu kutumia mabomba chanzo cha maji kikiwa karibu? Strange logic this!
 
Nimeuliza mahali pengine kuwa kwanini basi hawa wanaowapelekea wenzao chemli za jua na visima wao wenyewe hawaanzii pa kutambaa. Umewahi kuona yeyote kati yao akianza kujenga nyumba ya makuti pindi akipata fedha kidogo?

Serikali hufanya kitu kinachofanana na hiyo "logic": kutumia udongo (yes udongo japo wao huita changarawe) kujenga barabara ambapo mvua ikinyesha mara moja tu udongo wote unasombwa na maji (kwa kisingizio cha kutokuwa na fedha za kutosheleza kujenga kwa kiwango cha lami!). Kwa maana hiyo kila mwaka zoezi hilo hilo moja linarudiwa. Mtu ungetarajia njia sahihi ingekuwa kujenga barabara inavyotakiwa kwa awamu kulingana na fedha zilizopo - mtu asiniambie kuwa kufanya hivyo kungesababisha sehemu ambayo haijajengwa isipitike kwa sababu uweke udongo au usiweke tofauti ni ndogo!
 
Nadhani itafika siku wataalamu wetu watakapopewa RUHUSA ya kutumia utaalam wao kutusogeza mbele. Mifano michache ipo pale utaalamu ulipotumika baada ya siasa kuamua utumike, mafanikio makubwa yapo.
- maji shinyanga na mwanasiasa lowasa,
- barabara za mawe mwanza
- ni chache ninazojua.
Tuna ushahidi pia pale siasa inapoangamiza utaalamu
- umeme
- elimu
 
Mara nyingi sana nimesikia wanasiasa wakitoa ahadi za kuchimba visima kama njia ya kutatua tatizo la maji - iwe mjini au vijijini. Hebu angalia vichwa hivi vya habari kisha usome swali langu tena:

Wamarekani kuchimba visima 20 Dakawa

Watumia Sh400 mil kuchimba visima

Dewji achimba visima kwa milioni 500 Singida


Abood aingiza mitambo ya kuchimba visima

Mbunge aanza kuchimba visima 60 jimboni

Ujenzi visima vya maji Morogoro, wakazi pembezoni mwa mji kunufaika.


Sasa kuna vitu najiuliza:

a. Kwanini mara nyingi suluhisho la haraka linalochukuliwa kukabiliana na tatizo la maji ni kuchimba visima na hivyo kuwasababisha wananchi kuyafuata maji kutoka majumbani mwao badala ya kufikiria mfumo wa kuwaletea maji hayo (yanayopatikana kwenye visima hivyo) kwa wananchi?

b. Je, kuna uwezekano wa kubuni njia ya kuunganisha visima kadhaa kutengeneza mfumo wa maji wa mahali (local water supply system) badala ya kuwa na visima kimoja kimoja? Kwa mfano, visima 50 (au hata kimoja tu) vinajaza maji kwenye tanki la jumuiya na kutoka kwenye tanki (lililoko uphill) mabomba yanarudishwa wa wananchi? Kinachohitajika ni kutengeneza pump ya upepo kusukuma maji mlimani.

c. Ni kweli kuchimba visima vingi yaweza kuwa ni suluhisho la sasa "hivi" la maji lakini ni visima vingapi ambavyo vimebakia kutumika baada ya miaka na viko katika hali gani na je ndilo suluhisho bora zaidi? Kuna namna nyingine yoyote ya kuweza kutumia maji yaliyoko ardhini kutengeneza mfumo wa maji safi katika jamii mbalimbali?

Ninajua kuna wataalamu wa mambo mbalimbali hapa ambao wanaweza kutusaidia kujibu swali hili: Je inawezekana kutumia maji ya visimani kuweza kuyafikisha kwenye nyumba ya kila mwanakijiji badala ya kila mwanakijiji kulifuata bomba au kisima kilipo?

Ngoja na mimi nichangie kidogo.
Kwanza kuna aina nyingi ya visima, kuna visima vifupi ambavyo tumevizoea Tanzania. Hivi maji yake ni yale yanayotegeme groung water level. Hivi ufanisi wake huwa ni wa msimu na muda mfupi. Kuna visima ambavyo ni virefu 100 - 300 meters, hasa boreholes. hivi hutegemea mito ya chini ambayo huwa chini ya miamba. Kama feasibility study yake inafanyika vizuri, hivi hutoa maji mengi na huweza kulisha miji. Sasa ni swala la kuwatumia wataalamu na sio wanasiasa kuamua mipango ya maji katika vijiji na manispaa NK. Kama kijiji hakina mto karibu, hii ya visima ni option nyingine.
Asante, Nawakilisha.
 
:heh::heh:
:heh::heh:
Karibu kila kijiji kinaweza kuwa na reservoir tank. Siyo kama nahusisha sana wamarekani, ila jinsi ya kujua kama upo mji gani wakati unaendesha vijijini ni through water reservoirs ambazo nyingine zimejengwa miaka 200 iliyopita!

images


Ila hiyo kitu inahitaji nishati, either umeme au mafuta.. hata solar.
Mtanisamehe wakuu, uwezo tunao na sababu tunazo!.... fedha hatuna.

Fedha ni nyingi sana, tunazo na tena tunazo nasema!
Ambacho hatuna ni utashi na dhamira kwa uongozi!
Kwa kurudi kwenye hoja, wengi tumejaribu kuonyesha ugumu wa mpango huo kwa kulinganisha na kile ambacho kimekuwa kinafanywa na wenzetu sehemu mbalimbali, ni kweli ni uchambuzi mzuri.
Ila kwa jinsi nilivyomuelewa Mwanakijiji mie ni kwamba je ni kwa kiasi gani kama taifa tumelichukulia hili kama MAONO MAKUBWA (big picture) na kujaribu kuiendea kama taifa huru kwa kutumia njia zetu wenyewe na utaalamu wetu, vipi tumevishirikisha vyuo vyetu vya technology kama MTC, ATC na DIT?
Vimefanya utafiti? Vimesemaje?
 
..TATIZO TUMEWAACHIA WANASIASA WAINGILIE HATA MAMBO YA KITAAALAMU.
Wao ndo wanaamua ni kitugani kipewe kipaumbele na kifanywe vipi.

Hapo kwenye BOLD hapo!
Hilo ni gonjwa baya sana la nchi hii, na ndilo linalosababisha tuonekane watu hatuna upeo (tumefikia mwisho wa kufikiri).
Ukiachilia kadhia ya maji, hilo gonjwa kwenye BOLD ndio chanzo cha matatizo ya umeme tuliyonayo sasa! Mwanasiasa wa Tanzania ni mtaalamu wa kila kitu!

 
Nani amesema ili mabomba yaweze kusambwazwa ni lazima chanzo cha maji kiwe kwenye eneo husika? umewahi kusikia vitu vinaitwa pampu?

Mwanakijiji hemu rudi kwenye vichwa vya habari ulivyoweka uangalie ni nani anayechimba hivyo visima? Ni Serikali au watu binafsi? naomba uwaombe radhi hao waungwana sababu walichokifanya sio kazi yao wamejitolea tu ili kupunguza tatizo la ukosefu maji kwenye maeneo husika.

Swala la usambazaji Maji safi na salama kwa kila mwananchi kwa mfumo bora zaidi ya hii unayopendekeza liko kwenye Ilani za Chama za Uchaguzi 1995,2000, 2005 na 2010 na sasa inaandiliwa nyingine kwa uchaguzi wa 2015 ambako utafanyika uboreshaji zaidi, au wewe unataka nini?
 
mimi huwa sipendi sana kufikir haya kwani najikuta na frustrate tu. ni bora nikawa nachangia kwenye other social aspects
 
MMJ, utaalamu wa kusafirisha maji, upo tangu miaka elfu huko nyuma, walitumia wamisri zamani sana hakuna mwanasayansi au mhandisi hata aliefeli asiejua hilo. Utaalamu wa siku hizi ni mkubwa sana na unajulikana na wataalamu wengi tu.

ila kurudi kwenye point kuwa uwezo wa kufikiri ni mdogo, ni kweli pale ambapo tunafikiri kuwa kuacha kutumia utaalamu ndio utaalamu wenyewe.
 
[
a. Kwanini mara nyingi suluhisho la haraka linalochukuliwa kukabiliana na tatizo la maji ni kuchimba visima na hivyo kuwasababisha wananchi kuyafuata maji kutoka majumbani mwao badala ya kufikiria mfumo wa kuwaletea maji hayo (yanayopatikana kwenye visima hivyo) kwa wananchi?]
Mkuu hapa kinachofanyika ni zimamoto. Unakuta hakuna upembuzi yakinifu uliofanya. Ungefaywa miradi mingi ya maji isingewezekana. Nani atalipia gharama za uendeshaji mradi baada ya uzinduzi? Maji yaliyopo chini yataendelea kuwapo katika ubora wake wa sasa kwa muda gani? Jambo la muhimu ambalo siku zote husahaulika huku uswahilini ni ukweli kwamba rasilimali ya maji salama inapungua siku hadi siku duniani kote. Je ongezeko la idadi ya watu hapo kijijini linaakisi vipi ukweli huu?
 
Linalowezekana leo lisingoje kesho!

Chelewa chelewa utamkuta mtoto si wako. Ngojangoja huumiza matumbo.

Nadhani suala la kuchimba visima kila mahali (saizi moja inatosha wote) si sahihi. Linaweza likawa suluhisho la muda mfupi lakini kwa muda mrefu nina mashaka. Hata kama kuna mifano michache huko Dodoma ya visima vilivyochimbwa tangu 1930 hivyo ni vichache sana. Kwa ujumla miundo mbinu ya visima huharibika haraka zaidi.

Mpango ambao unafaa sehemu nyingi za nchi yetu ni uchimbaji wa mabwawa. Kwanza, mabwawa yakisimamiwa vizuri yanaweza kuleta manufaa zaidi kuliko visima. Kufuga samaki, kumwagilia, kunywesha mifugo ni baadhi ya mambo ambayo visima haviwezi kukidhi. Ukweli ni kuwa hatuna mpango wowote wa kuwaondolea wanavijiji matatizo ya maji. Hatua zinazochukuliwa sasa ni za kisiasa tu wala hazina utaalam wowote.
Nilitokwa na machozi nilipoenda Mwadui ambako Mcanada mmoja mwaka 1947 alichimba mabwawa matatu ambayo yanatumika hadi leo. Hakuna tena hata bwawa moja lililoongezeka katika wilaya ya Kishapu tangu tupate uhuru. Nikajiuliza, hivi katika miaka hamsini ya uhuru, tungejiwekea kuchimba bwawa moja kila wilaya kila baada ya miaka mitano, saa hizi kila wilaya ingekuwa na mabwawa kumi. Hii ingekuwa hatua kubwa sana katika kutatua matatizo ya maji kwani bwawa moja lina uwezo wa kuhudumia vijiji kadhaa na kama alivyoeleza kwa usahihi kabisa MM, kwa vile maji ni uhai masuala ya afya, lishe, elimu na kilimo yangestawi zaidi ya ilivyo sasa.
Utaalam ungetumika, kila palipo na uwezekano wa kutumia nguvu ya mserereko kungefanyika hivyo ili kupunguza ama kuondoa gharama za siku kwa siku zinazotokana na matumizi ya pump katika kuwasambazia wanavijiji maji. Ukiangalia nchi yetu fursa za kutumia mserereko ni nyingi sana lakini hazitumiki. Maeneo mengi ambayo yana maji ya uhakika kwa miaka mingi ni pale ambapo mfumo wa mserereko umetumika. Sehemu kama Moshi Vijijini mifumo tangu enzi za mjerumani inafaya kazi leo hii. Sehemu nyingi vijijini ambazo ziliwekewa mabomba na pump sasa hivi ni makumbusho ya vijiji husika.

Pakiwepo na nia ya dhati ya kuondoa matatizo ya maji vijijini, inawezekana kabisa ikabaki kuwa historia baada ya miaka michache. Kwa sasa visima vimeacha msiba mkubwa pindi wachimbaji wenye utaalam wanapoondoka. Mfumo unahitaji fedha na wataalam pia wanahitaji fedha kuhudumia mfumo wa visima. Ukichukulia kuwa maji yanahitajika siku zote inafika mahali miradi ya visima inakwama. Tutumie mifumo ambayo haihitaji uangalizi na gharama kubwa baada ya kuitengeneza. MM kama ungeweza kuishauri serikali yetu kutumia mabilioni ya uwanja wa mpira wa taifa na yale ya jengo la bunge pengine na yale ya miaka hamsini ya uhuru (bila kutaja ya ufisadi mbalimbali) kushughulikia kwa dhati maji, leo mathalani, mkoa wa Dodoma shida ya maji ingekuwa hadithi.
 
Unawezaje kuzungumzia upeo wa fikra bila kujua afya za hao wanasiasa?

In 1946 The World Health Organization stated ..... "a state of complete physical, mental, and social well-being and not merely the absence of disease or infirmity" Health - Wikipedia, the free encyclopedia

Ntatoka nje kidogo ya mtiririko wa mada ulivyo mpaka sasa.
Unapokuwa na wanasiasa aina ya Lusinde, Wassira nk je ni sahihi kutumia neno fikra na/au upeo? Wengi wao wapo kwenye ile red na hawakidhi hicho kigezo cha msingi.
 
Back
Top Bottom