Upeo wa Uwezo wetu kufikiri? - Kwanini suluhisho la tatizo la maji vijijini ni kuchimba visima?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Mara nyingi sana nimesikia wanasiasa wakitoa ahadi za kuchimba visima kama njia ya kutatua tatizo la maji - iwe mjini au vijijini. Hebu angalia vichwa hivi vya habari kisha usome swali langu tena:

Wamarekani kuchimba visima 20 Dakawa

Watumia Sh400 mil kuchimba visima

Dewji achimba visima kwa milioni 500 Singida

Abood aingiza mitambo ya kuchimba visima

Mbunge aanza kuchimba visima 60 jimboni

Ujenzi visima vya maji Morogoro, wakazi pembezoni mwa mji kunufaika.

Sasa kuna vitu najiuliza:

a. Kwanini mara nyingi suluhisho la haraka linalochukuliwa kukabiliana na tatizo la maji ni kuchimba visima na hivyo kuwasababisha wananchi kuyafuata maji kutoka majumbani mwao badala ya kufikiria mfumo wa kuwaletea maji hayo (yanayopatikana kwenye visima hivyo) kwa wananchi?

b. Je, kuna uwezekano wa kubuni njia ya kuunganisha visima kadhaa kutengeneza mfumo wa maji wa mahali (local water supply system) badala ya kuwa na visima kimoja kimoja? Kwa mfano, visima 50 (au hata kimoja tu) vinajaza maji kwenye tanki la jumuiya na kutoka kwenye tanki (lililoko uphill) mabomba yanarudishwa wa wananchi? Kinachohitajika ni kutengeneza pump ya upepo kusukuma maji mlimani.

c. Ni kweli kuchimba visima vingi yaweza kuwa ni suluhisho la sasa "hivi" la maji lakini ni visima vingapi ambavyo vimebakia kutumika baada ya miaka na viko katika hali gani na je ndilo suluhisho bora zaidi? Kuna namna nyingine yoyote ya kuweza kutumia maji yaliyoko ardhini kutengeneza mfumo wa maji safi katika jamii mbalimbali?

Ninajua kuna wataalamu wa mambo mbalimbali hapa ambao wanaweza kutusaidia kujibu swali hili: Je inawezekana kutumia maji ya visimani kuweza kuyafikisha kwenye nyumba ya kila mwanakijiji badala ya kila mwanakijiji kulifuata bomba au kisima kilipo?
 
Umesahau hii, mkuu. JOSHUA NASARE kuanza na kuchimba visima. mfuuuuuuuu. Kaz kweli kweli. au wachimbe malambo nini. acha siasa hapa ni jiografia ndiyo inapelekea visima kuwa suluhisho. Huwezi kusambaza mabomba kama chanzo cha maji hakiko karibu na eneo husika. au ulitaka wachimbo malambo? hayo yapo na ni kwa ajili ya mifugo.
 
mkuu kubali matokeo, hayo mengine makubwa tumeshindwa sasa tunajikita katika tunayoyaweza - yaliyo katika viwango vyetu: visima vya maji, vibajaji vya wagonjwa, vyuo vya kata n.k

You got it right companero... lakini ndio mwisho wa "upeo" wetu wa kufikiria?
 
Umesahau hii, mkuu. JOSHUA NASARE kuanza na kuchimba visima. mfuuuuuuuu. Kaz kweli kweli. au wachimbe malambo nini. acha siasa hapa ni jiografia ndiyo inapelekea visima kuwa suluhisho. Huwezi kusambaza mabomba kama chanzo cha maji hakiko karibu na eneo husika. au ulitaka wachimbo malambo? hayo yapo na ni kwa ajili ya mifugo.

Nani amesema ili mabomba yaweze kusambwazwa ni lazima chanzo cha maji kiwe kwenye eneo husika? umewahi kusikia vitu vinaitwa pampu?
 
Wazo hili ni zuri sana, na nilishawahi kulifikiria baada ya kumtembelea mwekezaji mmoja eneo la mbezi-Dar es Salaam aliyetumia mfumo huu. Wakati wa mahojiano yetu, nilimuuza ni kwa nini aingie gharama ya kuchimbia mabomba chini kwa umbali kilomita nne kutoka eneo lilipo tank la kuhifadhia maji yatokayo kisiman wakati anaweza akafuata maji hayo kwa gari?
Majibu yake ndiyo yaliyonithibitishia kuwa either upeo wa viongozi wetu ni mdogo au viongozi wetu hawana nia ya dhati ya kutatua matatizo yetu kikamilifu. Hivi mmeshawahi kujiuliza ni muda kiasi gani dada zetu wanautumia kufuata maji kwenye hivyo visima? Je muda huo hauwezi kuokolewa na kutumika katika shughuli nyingine za uzalishaji?
 
You got it right companero... lakini ndio mwisho wa "upeo" wetu wa kufikiria?

ndio mwisho, tuwe wakweli na nafsi zetu, tufanye yale marahisi yaliyo ndani ya uwezo wetu, hayo mengine watafanya vizazi vijavyo vilivyopevuka vya watoto na wajukuu zetu; badala ya kufikiria matrekta makubwa tuzidi kutumia power tillers, tutafika hata kwa kutambaa.
 
Mara nyingi sana nimesikia wanasiasa wakitoa ahadi za kuchimba visima kama njia ya kutatua tatizo la maji - iwe mjini au vijijini. Hebu angalia vichwa hivi vya habari kisha usome swali langu tena:

Wamarekani kuchimba visima 20 Dakawa

Watumia Sh400 mil kuchimba visima

Abood aingiza mitambo ya kuchimba visima

Mbunge aanza kuchimba visima 60 jimboni

Ujenzi visima vya maji Morogoro, wakazi pembezoni mwa mji kunufaika.

Sasa kuna vitu najiuliza:

a. Kwanini mara nyingi suluhisho la haraka linalochukuliwa kukabiliana na tatizo la maji ni kuchimba visima na hivyo kuwasababisha wananchi kuyafuata maji kutoka majumbani mwao badala ya kufikiria mfumo wa kuwaletea maji hayo (yanayopatikana kwenye visima hivyo) kwa wananchi?

b. Je, kuna uwezekano wa kubuni njia ya kuunganisha visima kadhaa kutengeneza mfumo wa maji wa mahali (local water supply system) badala ya kuwa na visima kimoja kimoja? Kwa mfano, visima 50 (au hata kimoja tu) vinajaza maji kwenye tanki la jumuiya na kutoka kwenye tanki (lililoko uphill) mabomba yanarudishwa wa wananchi? Kinachohitajika ni kutengeneza pump ya upepo kusukuma maji mlimani.

c. Ni kweli kuchimba visima vingi yaweza kuwa ni suluhisho la sasa "hivi" la maji lakini ni visima vingapi ambavyo vimebakia kutumika baada ya miaka na viko katika hali gani na je ndilo suluhisho bora zaidi? Kuna namna nyingine yoyote ya kuweza kutumia maji yaliyoko ardhini kutengeneza mfumo wa maji safi katika jamii mbalimbali?

Ninajua kuna wataalamu wa mambo mbalimbali hapa ambao wanaweza kutusaidia kujibu swali hili: Je inawezekana kutumia maji ya visimani kuweza kuyafikisha kwenye nyumba ya kila mwanakijiji badala ya kila mwanakijiji kulifuata bomba au kisima kilipo?

Inawezekana kabisa kuunganisha hivyo visima kwenye bwawa au tank na kuwa na mfumo mmoja wa usambazaji wa maji kwenye eneo kubwa. Resolute Gold Mine pale Nzega wanao mfumo wa aina hiyo. Wamechimba visima kadhaa ambavyo vina pump zenye kusukuma maji kwenye bwawa moja na hatimaye maji hayo kwenda kwenye processing plant. Kama unavyosema, tuko likizo ya kifikra.
 
ndio mwisho, tuwe wakweli na nafsi zetu, tufanye yale marahisi yaliyo ndani ya uwezo wetu, hayo mengine watafanya vizazi vijavyo vilivyopevuka vya watoto na wajukuu zetu; badala ya kufikiria matrekta makubwa tuzidi kutumia power tillers, tutafika hata kwa kutambaa.

Mbona kwenye mambo ya usafiri hatutilii mkazo pikipiki kwa viongozi wa juu na badala yake tunataka magari ya kisasa kabisa? Mbona kwenye nyumba hatujengi za makuti au mabati tu na sasa tunaenda majumba ya malumalu toka Uarabuni? Mbona hatutumii viti vya mbao maofisini na badala yake tunavyo vya kunesanesa vilivyotengenezwa kwa ngozi ambavyo ukikalia vinabonyea bonyea na kukubembeleza?
 
Umesahau hii, mkuu. JOSHUA NASARE kuanza na kuchimba visima. mfuuuuuuuu. Kaz kweli kweli. au wachimbe malambo nini. acha siasa hapa ni jiografia ndiyo inapelekea visima kuwa suluhisho. Huwezi kusambaza mabomba kama chanzo cha maji hakiko karibu na eneo husika. au ulitaka wachimbo malambo? hayo yapo na ni kwa ajili ya mifugo.

Shinyanga wanakunywa maji kutoka Ziwa Victoria ambalo liko mkoani Mwanza, zaidi ya km 200.

Lowassa amevuta maji kutoka Mlima Meru kupeleka jimboni kwake Monduli.

Sio lazima chanzo cha maji kiwe within a locality, ni swala la dhamira na priorities.

Tanzania tumezowea maisha ya kiswahili ya kununua unga wa kibaba au nusu na robo, just enough for today's meal. Mambo ya kesho yatajijua yenyewe.
 
Mbona kwenye mambo ya usafiri hatutilii mkazo pikipiki kwa viongozi wa juu na badala yake tunataka magari ya kisasa kabisa? Mbona kwenye nyumba hatujengi za makuti au mabati tu na sasa tunaenda majumba ya malumalu toka Uarabuni? Mbona hatutumii viti vya mbao maofisini na badala yake tunavyo vya kunesanesa vilivyotengenezwa kwa ngozi ambavyo ukikalia vinabonyea bonyea na kukubembeleza?

uchumi wa kukuza (economy of scale) ndugu yangu. kama tungekuwa na uwezo wa kuwa na vituo vya ndege vyenye lami nchi nzima mbona tungefanya hivyo. kwa sasa tunaweza tu baadhi ya viwanja - tumeweka pale mwadui irahisishe kusafirisha almasi tulizowekezwa ila kuweka pale uwanja wa ndege wa mkoa wa shinyanga (simiyu?) ilipo mwadui achilia mbali kigoma ni tabu, changarawe zinatosha-hapo ndipo uwezo wetu ulipoishia. naam na tungeweza kuwalipa walimu na madaktari wote mshahara mzuri mbona tungefanya hivyo ila kwa sasa tunaweza kufanya hivyo kwa viongozi wakuu na wabunge wachache tu. uchumi wa kukuza-economy of scale.
 
Je inawezekana kutumia maji ya visimani kuweza kuyafikisha kwenye nyumba ya kila mwanakijiji badala ya kila mwanakijiji kulifuata bomba au kisima kilipo?

Mkuu hiyo inawezekana Kabisa, Nchi kama Botswana (KANYE area) wamefanya hiyo kitu na nimeshuhudia hiyo project ikifanya vizuri tu

Kama ukipata aquifer nzuri, unachimba tu kisima na kunakuwa na pump kubwa na booster ya kupandisha maji kwenye reserve tank juu ya mlima au tower, kisha maji yanaingia mjini kutoka kwenye reserve tank kwa gravity tu
 
tatizo teknolojia mwanakijiji

ina maana hatuna watu wenye uwezo wa kubuni teknolojia ya kufikisha maji ya kisima kwa mabomba kwa wananchi au hatuna watu ambao wanaweza kutumia teknolojia iliyopo tayari kufikia lengo hilo hilo?
 
Mkuu hiyo inawezekana Kabisa, Nchi kama Botswana (KANYE area) wamefanya hiyo kitu na nimeshuhudia hiyo project ikifanya vizuri tu

Kama ukipata aquifer nzuri, unachimba tu kisima na kunakuwa na pump kubwa na booster ya kupandisha maji kwenye reserve tank juu ya mlima au tower, kisha maji yanaingia mjini kutoka kwenye reserve tank kwa gravity tu

nimeipenda hiyo kauli upeo; maana reaction ya baadhi ya watu ni "hatuwezi" halafu wanajaribu kutafutia visingizio vya kwanini haiwezekani. Ukianza na "tunaweza" ni rahisi kutafuta namna ya kufanya sasa.. thanks
 
Mkuu hiyo inawezekana Kabisa, Nchi kama Botswana (KANYE area) wamefanya hiyo kitu na nimeshuhudia hiyo project ikifanya vizuri tu

Kama ukipata aquifer nzuri, unachimba tu kisima na kunakuwa na pump kubwa na booster ya kupandisha maji kwenye reserve tank juu ya mlima au tower, kisha maji yanaingia mjini kutoka kwenye reserve tank kwa gravity tu

Tunaweza kufanya hivyo,ila hatujataka. Na kama hatujataka hatutaweza kufanya lolote hata iweje. Inanihuzunisha sana kuona jinsi tunavyopeleka mambo. Kweli hatuwezi kufika popote
 
sio kwamba wataalamu hakuna. mbona mpaka tuna chuo cha maji rwegarulila. tatizo ni uchumi wa kukuza. maendeleo ni kujitoa mhanga.
 
Mwanakijiji,

Kwenye swala la maji na haswa vijijini kuna utata mkubwa linapokuja swala la kuwasambazia maji majumbani. Kabla ya kufikiria kuwasambazia maji majumbani inabidi kuwa na uhakika kwamba wananchi wana uwezo wa kulipa bills za maji za kila mwezi kulingana na matumizi ya maji. Wananchi wa vijijini wana vipato vidogo kuna familia zilikuwa zinashindwa kulipa shilingi 30 kununua ndoo moja ya maji.

Nimeshiriki mradi wa kuchimba visima Mbeya na Iringa chini ya ufadhili wa NGO kutoka nje. Linapokuja swala la ku-run huo mradi wa visima sehemu nyingi tulizochimba visima baada ya muda fulani pump zinakufa au wanashindwa hata kununua mafuta ya ku-run pump. Ukichunguza sana visima vingi ni pump za mkono na sio zinazotumia mafuta. Hata hizo za mkono, zikiharibika ndo inakuwa imetoka.

Baada ya kugundua kwamba visima tunavyochimba havidumu, tukaamua kwamba kabla ya kuchimba kisima lazima tuhakikishe kuna meneja wa mradi wa maji ambaye kazi yake ni kuhakikisha kwamba wananchi wote wanaokuja kuchota maji wana nunua kwa bei ambayo wanakijiji wamekubaliana. Kwa hiyo makusanyo yote yanahifadhiwa kwa ajili ya kununua mafuta na pia kufanya matengenezo just in case pump ya maji ikiharibika.

Kuna baadhi ya vijiji, mameneja wa maji walianza kuwa mafisadi. Ikabidi kuangalia namna ya kuwadhibiti. Kwamba kunakuwa na Kamati/Bodi ya Maji ya Kijiji na pia kunafungwa mita ili kujua kwamba maji kiasi gani yameuzwa.. Kwa hiyo meneja wa mradi anapopeleka makusanyo ya mwezi, kamati inakagua reading ya kwenye mita.

Visima vinachimbwa kwa wingi kwa kuwa wachimbaji wengi wanaogopa kuingia gharama za kujenga infrastructure ya kusambaza maji na wengi wa wanaochimba visima wanajitolea kama msaada. Ili wazo la kusambaza maji lifanikiwe lazima kuwe na kampuni ambayo inafanya biashara ya kutoa huduma ya kusambaza maji majumbani. Nina amini kwamba wawekezaji wengi kwenye hilo eneo wanakwepa gharama za kuanzisha huduma hiyo, initial cost ni kubwa na itarudi baada ya muda mrefu.

Idea ya kusambaza maji inawezekana lakini kuna some pre-conditions ambazo zinatakiwa kuwa met.
1. Hali ya uchumi wa wasambaziwa maji kwamba waweze kulipa bills zao
2. Mipango Miji/Vijiji ili kuwa na ramani kwamba bomba kubwa la maji litapita, halafu mabomba madogo yatatandazwa wapi.
3. Huduma ya maji itolewe kwa misingi ya biashara, kwamba ama serikali ainzishe shirika la kutoa huduma hiyo au kampuni binafsi zifanye kazi hiyo. Kampuni binafsi wanaogopa kuingia kwenye hiyo biashara kwa sababu wanakwepa gharama za kujenga infrastructure ya kusambaza maji. Inachukua muda mrefu ku-recover gharama za kutandaza mabomba kwa watumiaji.
 
Kuna aina mbili ya visima vinavyo chimbwa huko vijijini kuna shallow wells(visima vifupi)vinavyo tumia pump za mkono na kuna visima virefu(bore holes)hutumia pump ya umeme au upepo ,pia hutegemea upatikanaji maji katika maeneo tofauti,kuna maeneo huwa kuna patikana maji mengi kutoka kwenye hivyo visima kwa hiyo usambazaji kutoka kwenye visima hivyo huwa rahisi .

Kwa mfano unaweza chimba kisima chenye kina cha urefu ma mita 100 ukapata maji lita 50000 kuna eneo unaweza chimba kisima mita 100 ukapata lita 2000 ,inategemea na eneo na jiografia yaliyopo hivyo visima.

Kwa Tanzania mfumo wa kusambaza maji kutoka kwenye visima hutegemea na uwezo wa visima hivyo vinazalisha maji kwa kiwango gani,wengi huona kuchimba visima na wananchi kuteka maji kutoka kwenye visima moja kwa moja ni njia rahisi na yenye gharama nafuu au njia ya kupata maji kwa njia ya dharura, kwa tulivyo sasa katika uzalishaji wa umeme hatujawa na mfumo wa kuzalisha umeme wa kudumu bado tunavyo vyanzo vya kuzalisha umeme wa dharura hali kadhalika ipo kwa katika mfumo wa maji.

Wana siasa wengi huona kuchimba visima vingi katika maeneo tofauti ni ufumbuzi wa haraka na wa gharama nafuu unaweza kuta kuna eneo mfumo wa usambazaji maji unahitaji shs 1 B ambazo kupaikana hizo bilioni ni ngumu jwa hiyo utakuta mwanasiasa anatafuta shs 200m anachimba visima kadhaa maji ya dharura yanapitakana.

Pia watanzania tuna tatizo la mfumo wetu,kwa mfano mtu hawezi kubali kule Mufindi ,Iringa kuna matatizo ya madawati ,hali ya kuwa ni misitu ya mbao ,halmshauri za Mufindi inaweza toa msharti kwa kila kampuni inayo vuna mbao azalishe madawati kadhaa kupeleka kwenye shule hizo lakini wapi!!hawan fikra hizo !
 
Back
Top Bottom